Monday 29 June 2015

[wanabidii] KIZAA ZAA BAGAMOYO ALIYEDHANIWA MAITI APUMUA WAKATI AKIKOSHWA!

KIZAA ZAA  BAGAMOYO  MAITI APUMUA WAKATI AKIKOSHWA!

Hospitali ya wilaya Bagamoyo ilithibitisha kuwa mgonjwa ni mauti !

Jasho lilianza kumtoka na joto kali la mwili ! Maziko hakuna tena !

Bagamoyo,

Maajabu ya mwenyezi Mungu yametokea msibani huko mjini Bagamoyo katika eneo lijukanalo kama Majani Mapana jana baada ya mwanamama moja aletambulika kwa jina Bi.Hatujuani kuthibitishwa kuwa umauti umekuta au amekufa hatimaye amepumua wakati wakimkosha na kwa matayarisho ya kuvikwa sanda ambayo tayari ilikwisha shonwa,
Bi.Hatujuani aliugua kwa muda na kukimbizwa hosptilai ya wilaya Bagamoyo baadaye kumpata sijui tuite umauti wa muda mfupi au kupoteza fahamu ! lakini hospitalini hapo walithibitisha kuwa keshakufa, mkasa huo ulitokea tarehe 28.juni 2015 na wanandugu walishachukua maiti na matayarisho ya maziko yakiwa mbioni ,Turubai lilishafungwa,sanda tayari hadi siku 29 juni 2015 wakimkosha maiti  Bi.Hatujuani aka hatu mwenye umri wa miaka 30 ,waliokuwa wakimkosha walishtuka maiti kuwa anajoto kali,anatoka jasho na anakunja na kukunjua mikono na miguu ! lakini kusema wala kusimama hawezi !

Wanandugu waingia tafrani Msiba hakuna tena ! Turubai limeshaezuliwa !
baada ya wanandugu kutangazia umma kuwa msiba hakuna tena bali tuna mgonjwa maututi 
waliofika msibani na umati wa watu wagoma kuondoka mazikoni hadi kieleweke nini? kilichozua mtihani huu tena katika mwezi huu mtukufu wa
Ramadhani


Hivi unavyosoma habari na turubai limeshaezuliwa hakuna msiba.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment