Monday 29 June 2015

[wanabidii] NGOMA AFRICA BAND KUTINGISHA MAMLING FESTIVAL- AUSTRIA




NGOMA AFRICA BAND KUTINGISHA MAMLING FESTIVAL- AUSTRIA


Mzimu wa Ngoma Africa band kuibukia Mamling Festival Jumapili 5 Julai 2015-Austria


Mining City,Austria,

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni,yenye makao nchini Ujerumani,inatarijiwa kutumbuiza katika maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni Mamling Festival  siku ya jumapili 5 Julai 2015 alhasiri katika viwanja vya Schlosspark,Mamling 3, Mining nchini Austria. watayarishaji wa onyesho hilo wameitaja bendi hiyo ya Ngoma Africa band kuwa muziki wake ni sawa na mzimu unawapeleka puta washabiki katika maonyesho ya kimataifa na washabiki nchini Austria wanameisubiria kwa muda wa mwaka mzima. Kikosi kazi hiko chenye tabia ya kuwatia kiwewe washabiki wake kila waendako na kujizolea washabiki lukuki kote duniani,kinaupeleka muzimu wa Bongo Dansi nchini Austria .Ziara ya bendi hiyo imeingiliana na mwezi wa Ramadhani wakati baadhi ya wanamuziki wapo katika swaumu lakini
watatekeleza wajibu wao.
Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja ni bendi iliyobatizwa majina mengi ya kiusanii kutoka kwa washabiki majina kama FFU-Ughaibuni, "Watoto wa Mbwa",Viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien' na mengi mengineyo. ni bendi yenye utajiri ya wanamuziki waliojaa vipaji, na kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbili
mpyakatika CD " La Mgambo" za kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda .

wasiliana nao at ngoma4u@gmail.com



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment