Sunday 28 June 2015

Re: [wanabidii] (Lowasa maji yamekushinda utaweza foleni au porojo za kisiasa?)

Lowasa akatatue tatizo la maji kwa mwaka mmoja au muda mfupi ambapo mifugo ya kutoka kwao na Mwanza imejaa kwa mamilioni au maelfu hadi Milima ya Uluguru kwenye vyanzo vya maji? Kilombelo kwenye Ramsa Site kwa malaki, wetlands zinazopeleka pia maji Rufiji-kwisha; Ruaha imezagaa baada ya kuondolewa Ihefu Ruvuma, Tunduru, Rukwa, Kisarawe, Rufiji, Morogoro vijijini wanakoma kwa bakora sio wilaya Kilosa tu. Angemudu kusaidia jimboni kwake ufugaji na kilimo endelevu lakini hajafanya hivyo; kusaidia wananchi wake wawe na muono wa mbali wa mifugo katika kukuza kipato na kulinda mazingira na kuboresha ng'ombe na mbuzi wa kienyeji kwa value added products za kuingiza kipato. kuhamahama, kulimbikiza mifugo sio tija. Kisha, uharibifu wa mazingira ufwanyao na wananchi wennyewe ndio wa kuhangaika nao ili maji yapatikane. Kuacha tabia ya kuharibu na kuvamia vyanzo vya maji, uchafuzi wa mazingira ndio akazanie ili baada ya miaka kadhaa matokeo ya maji mengi (sio muda
mfupi tu) yaonekane kutokana na re-charge ktk mazingira. Ikiwa sisi watanzania hatutobadilika kiakili na kimatendo-tusitegemee kubadili maendeleo yakue ghafla. Tunatiana umasikini na kujifanya masikini wenyewe.

Cha kujiuliza-huko Monduli kuna land degradation, utata wa maji wananchi kuchota barabarani mvua ikinyesha maji huwa machafu, kuchangia maji na mifugo -amefanya nini miaka yote hiyo? Anaweza kuonyesha miradi ipi akigharimia yy binafsi au kutafuta donors kwa proposals zake na kushirikiza watumishi ugani? Kuna boreholes za toka ukoloni kwenye maeneo yaliyokuwa estate farms. Ni hivi basi wagombea wengine ambao walikuwa wabunge na mawaziri pia waulizwe walichokifanya miaka yote iliyopita.i Unaweza ukawa waziri lakini utendaji unategemea walio chini yako lakini mbunge upo jimboni. Jee kijiji chako pale ulipo wananchi wako wanatofauti gani na hao wa vijiji vingine vya mbali? Hapo ulipo-nyumba bora, choo bora, shule bora na ufaulu mzuri maji safi yapo na huduma ya mifugo na ufugaji na kilimo cha kisasa na endelevu. Huenda hivi vichache havipo hata kata na kijiji cha mbunge! Leo unadai taifa zima utabadili kwa sekunde? Jee, wabunge hufanyiwa evaluation ya
majukumu yao na kila mmoja kila baada ya miaka 5 kutoa taarifa ya utekelezaji ya mipango binafsi na ile ambayo anashiriki kupitisha ktk Halmashauri ya Wilaya chini ya O&OD na ile inayopita bungeni ya national vertical programs? Bila ya kutathiminiwa-kunawekwa uwazi wa kutumia hela, kuruhusu rushwa itumike kupitisha wagombea vilaza. Daima maendeleo yapo duni wakati kuna kila aina ya resources vijijini, wataalamu wa serikali, vituo vya mifugo na vya kilimo, uvuvi na VETA juu na bajeti inawekwa.Tubadilike ili tusonge mbele viongozi na wananchi mijini na vijijini tuwe na muono chanya wa mbali.

Ona malalamiko ya bandari huko Zinga-Mlingotini yanayoonyeshwa ktk TV. Inasikitisha na ilinisikitisha binafsi kuona jinsi wavuvi walivyojijengea nyumba nzuri sana kwa juhudi za karne; miembe na minazi inayowapa chakula na fedha. Iliwezekana kabisa kukwemba nyumba za wanavijiji, kuchukua eneo ambalo ni arable land ya kilimo pia kuweka bandari ambapo yapo maeneo mengine yasiyo makazi kama hayo. Ila hapo -inaonekana-lililengwa pia shamba kubwa la mheshimiwa mmoja liondoke ambalo ni maelfu ya ekari amepanda pamoja na maembe dwarf burunge ya kisasa ambaye ana kesi moja ambayoimeleta utata. Shamba hilo litakuwa bandari kavu. Inatokea sasa kukomoa wananchi. Ni muda mrefu hawakutakiwi kuendelezwa maeneo yao lakini hawajalipwa. fikiria historia ya eneo kutoka utumwa, fikiria ya kuwa population kubwa ya huko ni ya wazee ambao wanategemea nazi, embe, mihogo wauze wale. Miembe inaumri wa zaidi ya miaka 60+ licha ya hiyo mipya. Leo kibibi/kibabu kianze moja atafute
pa kuhamia, alime, apande na climate chage hii, nguvu za kilimo zimekwisha, utata upo ktk jamii zetu wa kuamini hata vijukuu vibaka kuvipa hela za mafao au za valuation na compensation watekeleze ujenzi-vinasepa navyo.

Ofisi ya kijiji cha Mlingotini (Mgotini) inaishinda hata ofisi ya RC au DC. Niliipiga picha mwenyewe wakati wa utafiti usiohusu uhamishaji mwingine kabisa mwaak 2010 nililikuta zahama hilo la kihamo hadi leo hawajalipwa na hawaendelezi makazi au mashamba! Hiyo ofisi imejengwa na mwekezaji kama mafao yao na ipo katika kubomolewa. Sijui huyo mwekezaji kama atapona. Nimeiambatisha ofisi ya kijiji hicho uone.Majumba ya tofari za simenti waliyojenga wavuvi yanaumiza sana kuona yatabomolewa. Mungu atusaidie.


--------------------------------------------
On Sun, 28/6/15, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] (Lowasa maji yamekushinda utaweza foleni au porojo za kisiasa?)
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 28 June, 2015, 20:16

Ni mwizi tu na
mwongo!em
2015-06-28 12:35
GMT-04:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:


Wakati
Lowasa akitangaza nia katika uwanja wa sheikh Amri Abeid
Arusha,  akielezea sababu zake zake kutamani
nafasi
hiyo ya urais alikuwa na ndoto ya siku nyingi aliyoiita
ndoto ya matumaini.


Katika
safari hiyo ya ndoto ya matumaini Lowasa alikuwa akitoa
ahadi mbalimbali huku
akishangiliwa na umati uliojitokeza hapo uwanjani ktk
kushuhudia utiaji nia
wake na pamoja na mwanzo wa safari yakle ya ndoto ya
matumaini huku akitoa
ahadi kibao za kutatua kero za watanzania.


Lowasa
alifika mbali zaidi kwa kusema kuwa ataondoa foleni katika
jiji la Dar es Salam
ndani ya mwaka mmoja tu akatapokaa pale ikulu ya magogoni
ikiwa watanzania na
chama chake cha ccm watampa ridhaa ya kuongoza watanzania
katika awamu ya tano.


Napenda
kumkumbusha Lowasa kuwa hii haikuwa ahadi yake ya kwanza kwa
wakazi wa Dar es
Salaam kwani huku nyuma alishawahi kutoa ahadi ya kumaliza
kero ya maji katika
jiji hili al maarufu bongo lakini hakuweza kutimiza ahadi
yake hiyo kwa
wakazi  wa dare s salaam


Labda
niwakumbushe kidogo, mwaka 2002 wakati lowasa akiwa waziri
wa maji, serikali
ilipokea mkopo wa jumla ya kiasi cha dola za kimarekani
milioni 136, kutoka
benki ya dunia kwa ajili ya miundo mbinu na kusambaza maji
katika jiji la Dar
esSalalm, katika juhudi za serikali ya awamu ya tatu chini
ya rais mstaafu
Benjamini Mkapa.


Baada ya
kupata mkopo huo, Lowasa aliwatangazia wakazi wa Dar es
Salaam  na umma wa watanzania kuwa ndani y
miaka 3
ijayo yani kutoka mwaka 2003 mpaka 2005 tatizo la maji
lingebakia historia kwa
jiji la dare s Salaam, lakini hadi leo haijulikani fedh hizo
zilifanya kazi
gani, huku tatizo la maji likibakia kuwa ple ple kwa wakazi
wa jiji hilo.


Pamoja na
mika mitatu kupita na akaja akawa waziri mkuu lakini
hakufanya jitihada zozote
za kukumbuka ahadi yake ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam
mpaka anatoka
katika nafasi ya uwaziri mkuu, Swali langu ikiwa ameshindwa
ahadi yake ya
kuondoa maji ndani jiji la dare s Salaam kwa miaka mitatu
ataweza kuondo kero
ya foleni kwa mwaka mmoja?


Chanzo
Tazama





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment