Monday 29 June 2015

Re: [wanabidii] prof. Mwandosya amjibu Zitto Kabwe

Salaam wote; Prof. Nadhani, kupitia majibu yako, umeweza kujitofautisha na wale wengine. Very good Prof. Umeweza kijibu hoja iliyotolewa na Zitto. Mimi binafisi siangalii ukweli juu ya kile kilichojibiwa au juu ya tuhuma zilizotolewa ila naangalia namna Pro. alivyoweza kutoa majibu bila kujali kuwa alishawahi kutoa majibu ya namna hii hapo nyuma. Swali langu la kwanza kwa Zitto ambalo pengine linaweza kuibua wasi wasi wangu wa kwanza juu ya Mhe. huyu ( Zitto K), swali langu ni amezigundua lini tuhuma hizi na kwa nini katika kipindi hiki cha uchaguzi. Zitto K. anataka kutuambia Pro. hafai kutokana na scandal hii, sasa kama yeye hafai nani ni msafi?, yule mwengine je,yule wa RICHMOND je, utasema ulijui swala lake?. Kuna nini hapa.......... Kama ni kweli Zitto ndie aliyeibua issue hii, napata wasi wasi. Katika viongozi watia Nia, kwa mtazamo wangu, Pro. ameonekana kuwa tishio kidogo kwa Mhe. Lowasa, nadhani baada ya kuliona hilo ndio mchezo fulani
ukafanyika...........


Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX 1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713 728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sun, 6/28/15, 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] prof. Mwandosya amjibu Zitto Kabwe
To: "fadhil fadhil" <fadhil.fadhil96@gmail.com>, wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, June 28, 2015, 2:39 PM

Fadhil, kama kweli una uchungu na
nchi hii nenda kamkamate PAC wa escrow ambaye unajua
alilipwa dola 75million isivyo halali........vipi unataka
Lowasa akuambie Richmond ni ya........kama escrow
ilivyodhaniwa ya pinda kumbe.....wananchi wakishajua huyu
jamaa anatuhumiwa na kupingwa bure tu...vituhuma ambavyo
mwisho wa siku vinaweza pelekea kupata wasanii tu kwa
kutafuta malaika ambaye hayupo....Ngupula

fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:

Safi sana prof: unapoulizwa unatakiwa kujibu sio
unambelwa mbelwa kama mgombea fulani ana maswali mengi
kuliko majibu.
Anabakia na safari ya matumaini badala ya kujibu shutuma
zilizomuandama za rushwa na ufisadi.
On Jun 27, 2015 11:24
PM, "'mpombe mtalika' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Kama
wengi tulivyosikia jana, kuna tuhuma hizi hapa chini ambazo
zilitolewa jana na Zitto Kabwe na kuandikwa na vyombo vingi
vya habari leo.



HOJA YA ZITTO



Zittokabwe : Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa
Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin
Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii
yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na
tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali.



Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya
na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es
Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi
sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza
kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi
ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na
Celtel International.



Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake
kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee.
Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati
ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya
umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa
na ufisadi.



MAJIBU YA PROF MWANDOSYA



Zitto, Salaam.



Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi
kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya Chama chako. Ni jambo
zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza
uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika
utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara
nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika
post yako.



Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini
nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa
hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate
ufafanuzi kutoka kwa mhusika.



Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana
ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha
mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa
hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa
yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi.
Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua
ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa
sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo.
Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na
shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na
Usimamizi wa ujumla wa uchumi.



Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa:



Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara,
idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya
kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na
kampuni za umma ilikubalika zirekebishwe na hatimaye
zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria
kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha Mashirika ya
umma.



Chombo hiki, Parastatal Sector Reform Commission (PSRC)
kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango.
Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na
vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo
sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii
wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na
mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Ni vema hili
likaeleweka.



Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa
TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa
pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL
yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya
hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya
teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na
kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land
lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika
msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani
uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.



Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika
TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa
kuigwa na nchi nyingi za Afrika. Katika mawasiliano Tanzania
imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza
tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha
kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili
kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi
hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana
uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo
vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment