Saturday, 27 June 2015

Re: [wanabidii] prof. Mwandosya amjibu Zitto Kabwe

Safi sana prof: unapoulizwa unatakiwa kujibu sio unambelwa mbelwa kama mgombea fulani ana maswali mengi kuliko majibu.

Anabakia na safari ya matumaini badala ya kujibu shutuma zilizomuandama za rushwa na ufisadi.

On Jun 27, 2015 11:24 PM, "'mpombe mtalika' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kama wengi tulivyosikia jana, kuna tuhuma hizi hapa chini ambazo zilitolewa jana na Zitto Kabwe na kuandikwa na vyombo vingi vya habari leo.

HOJA YA ZITTO

Zittokabwe : Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali.

Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International.

Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.

MAJIBU YA PROF MWANDOSYA

Zitto, Salaam.

Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya Chama chako. Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika post yako.

Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi kutoka kwa mhusika.

Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi.

Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa:

Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma ilikubalika zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha Mashirika ya umma.

Chombo hiki, Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Ni vema hili likaeleweka.

Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.

Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika. Katika mawasiliano Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi, Regulatory Bodies. Nimebahatika kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA,TCAA, na EWURA.

Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, niliacha Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka, safari za abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku, na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.

Tuhuma za mtoto wa Profesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawasiliano ya simu aliomba kazi ya muda na akapewa.Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais mwaka 2005. Sasa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo huo mwaka 2015! Inaeleweka.

Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika!Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.

Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya ACT. Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba " Akili ni nywele, kila mtu ana zake"
Ramadhan Kareem. Wakatabahu,

Mwandosya.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment