Monday 29 June 2015

Re: [wanabidii] (Lowasa maji yamekushinda utaweza foleni au porojo za kisiasa?)

Ngulupa,
Sema linakuudhi wewe and the likes. Mimi hainiudhi kwa sababu nisingependa kuona fisadi mwingine ndani ya Ikulu. I am speaking for myself lakini nitafarijika kuona kuna Watanzania wengine wenye msimamo huu.
em

Sent from my iPhone

> On Jun 29, 2015, at 2:52 PM, "'ngupula' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Kama kuna jambo linaudhi watu kwa kiasi kikubwa ni hili la kumpinga Lowassa kila kukicha....hivi hao wengine hawahaidi? Mbona Lowassa tu? Inawezekana hili ndio jiwe wanalolikataa waashi? ....swali langu bado ni lilelile....kumbukeni, mnapompinga Lowassa mtupe na jibu nani anafaa na kwa lipi?........kwa kuwa ni kwel wananchi wanampenda, nashauri tu ni vema kuwa makini na huyu jamaa..... bila kumungunya maneno...nasema Tanzania watu wanaoweza kuisadia ni Lowassa na Mwigulu tu hawa ndio wenye muarobaini wa shida za watz......hawa hawaamin katika misaada ni ni watenda kazi hodari........na mtu akitaka kuzungumzia Richmond asisahau kuwa...ipo escrow na mwenyewe wanamjua...
>
> 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
>> Lowasa akatatue tatizo la maji kwa mwaka mmoja au muda mfupi ambapo mifugo ya kutoka kwao na Mwanza imejaa kwa mamilioni au maelfu hadi Milima ya Uluguru kwenye vyanzo vya maji? Kilombelo kwenye Ramsa Site kwa malaki, wetlands zinazopeleka pia maji Rufiji-kwisha; Ruaha imezagaa baada ya kuondolewa Ihefu Ruvuma, Tunduru, Rukwa, Kisarawe, Rufiji, Morogoro vijijini wanakoma kwa bakora sio wilaya Kilosa tu. Angemudu kusaidia jimboni kwake ufugaji na kilimo endelevu lakini hajafanya hivyo; kusaidia wananchi wake wawe na muono wa mbali wa mifugo katika kukuza kipato na kulinda mazingira na kuboresha ng'ombe na mbuzi wa kienyeji kwa value added products za kuingiza kipato. kuhamahama, kulimbikiza mifugo sio tija. Kisha, uharibifu wa mazingira ufwanyao na wananchi wennyewe ndio wa kuhangaika nao ili maji yapatikane. Kuacha tabia ya kuharibu na kuvamia vyanzo vya maji, uchafuzi wa mazingira ndio akazanie ili baada ya miaka kadhaa matokeo ya maji mengi (sio muda
>> mfupi tu) yaonekane kutokana na re-charge ktk mazingira. Ikiwa sisi watanzania hatutobadilika kiakili na kimatendo-tusitegemee kubadili maendeleo yakue ghafla. Tunatiana umasikini na kujifanya masikini wenyewe.
>>
>> Cha kujiuliza-huko Monduli kuna land degradation, utata wa maji wananchi kuchota barabarani mvua ikinyesha maji huwa machafu, kuchangia maji na mifugo -amefanya nini miaka yote hiyo? Anaweza kuonyesha miradi ipi akigharimia yy binafsi au kutafuta donors kwa proposals zake na kushirikiza watumishi ugani? Kuna boreholes za toka ukoloni kwenye maeneo yaliyokuwa estate farms. Ni hivi basi wagombea wengine ambao walikuwa wabunge na mawaziri pia waulizwe walichokifanya miaka yote iliyopita.i Unaweza ukawa waziri lakini utendaji unategemea walio chini yako lakini mbunge upo jimboni. Jee kijiji chako pale ulipo wananchi wako wanatofauti gani na hao wa vijiji vingine vya mbali? Hapo ulipo-nyumba bora, choo bora, shule bora na ufaulu mzuri maji safi yapo na huduma ya mifugo na ufugaji na kilimo cha kisasa na endelevu. Huenda hivi vichache havipo hata kata na kijiji cha mbunge! Leo unadai taifa zima utabadili kwa sekunde? Jee, wabunge hufanyiwa evaluation ya
>> majukumu yao na kila mmoja kila baada ya miaka 5 kutoa taarifa ya utekelezaji ya mipango binafsi na ile ambayo anashiriki kupitisha ktk Halmashauri ya Wilaya chini ya O&OD na ile inayopita bungeni ya national vertical programs? Bila ya kutathiminiwa-kunawekwa uwazi wa kutumia hela, kuruhusu rushwa itumike kupitisha wagombea vilaza. Daima maendeleo yapo duni wakati kuna kila aina ya resources vijijini, wataalamu wa serikali, vituo vya mifugo na vya kilimo, uvuvi na VETA juu na bajeti inawekwa.Tubadilike ili tusonge mbele viongozi na wananchi mijini na vijijini tuwe na muono chanya wa mbali.
>>
>> Ona malalamiko ya bandari huko Zinga-Mlingotini yanayoonyeshwa ktk TV. Inasikitisha na ilinisikitisha binafsi kuona jinsi wavuvi walivyojijengea nyumba nzuri sana kwa juhudi za karne; miembe na minazi inayowapa chakula na fedha. Iliwezekana kabisa kukwemba nyumba za wanavijiji, kuchukua eneo ambalo ni arable land ya kilimo pia kuweka bandari ambapo yapo maeneo mengine yasiyo makazi kama hayo. Ila hapo -inaonekana-lililengwa pia shamba kubwa la mheshimiwa mmoja liondoke ambalo ni maelfu ya ekari amepanda pamoja na maembe dwarf burunge ya kisasa ambaye ana kesi moja ambayoimeleta utata. Shamba hilo litakuwa bandari kavu. Inatokea sasa kukomoa wananchi. Ni muda mrefu hawakutakiwi kuendelezwa maeneo yao lakini hawajalipwa. fikiria historia ya eneo kutoka utumwa, fikiria ya kuwa population kubwa ya huko ni ya wazee ambao wanategemea nazi, embe, mihogo wauze wale. Miembe inaumri wa zaidi ya miaka 60+ licha ya hiyo mipya. Leo kibibi/kibabu kianze moja atafute
>> pa kuhamia, alime, apande na climate chage hii, nguvu za kilimo zimekwisha, utata upo ktk jamii zetu wa kuamini hata vijukuu vibaka kuvipa hela za mafao au za valuation na compensation watekeleze ujenzi-vinasepa navyo.
>>
>> Ofisi ya kijiji cha Mlingotini (Mgotini) inaishinda hata ofisi ya RC au DC. Niliipiga picha mwenyewe wakati wa utafiti usiohusu uhamishaji mwingine kabisa mwaak 2010 nililikuta zahama hilo la kihamo hadi leo hawajalipwa na hawaendelezi makazi au mashamba! Hiyo ofisi imejengwa na mwekezaji kama mafao yao na ipo katika kubomolewa. Sijui huyo mwekezaji kama atapona. Nimeiambatisha ofisi ya kijiji hicho uone.Majumba ya tofari za simenti waliyojenga wavuvi yanaumiza sana kuona yatabomolewa. Mungu atusaidie.
>>
>>
>> --------------------------------------------
>> On Sun, 28/6/15, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
>>
>> Subject: Re: [wanabidii] (Lowasa maji yamekushinda utaweza foleni au porojo za kisiasa?)
>> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
>> Date: Sunday, 28 June, 2015, 20:16
>>
>> Ni mwizi tu na
>> mwongo!em
>> 2015-06-28 12:35
>> GMT-04:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:
>>
>>
>> Wakati
>> Lowasa akitangaza nia katika uwanja wa sheikh Amri Abeid
>> Arusha, a
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment