--Wakati Lowasa akitangaza nia katika uwanja wa sheikh Amri Abeid Arusha, akielezea sababu zake zake kutamani nafasi hiyo ya urais alikuwa na ndoto ya siku nyingi aliyoiita ndoto ya matumaini.
Katika safari hiyo ya ndoto ya matumaini Lowasa alikuwa akitoa ahadi mbalimbali huku akishangiliwa na umati uliojitokeza hapo uwanjani ktk kushuhudia utiaji nia wake na pamoja na mwanzo wa safari yakle ya ndoto ya matumaini huku akitoa ahadi kibao za kutatua kero za watanzania.
Lowasa alifika mbali zaidi kwa kusema kuwa ataondoa foleni katika jiji la Dar es Salam ndani ya mwaka mmoja tu akatapokaa pale ikulu ya magogoni ikiwa watanzania na chama chake cha ccm watampa ridhaa ya kuongoza watanzania katika awamu ya tano.
Napenda kumkumbusha Lowasa kuwa hii haikuwa ahadi yake ya kwanza kwa wakazi wa Dar es Salaam kwani huku nyuma alishawahi kutoa ahadi ya kumaliza kero ya maji katika jiji hili al maarufu bongo lakini hakuweza kutimiza ahadi yake hiyo kwa wakazi wa dare s salaam
Labda niwakumbushe kidogo, mwaka 2002 wakati lowasa akiwa waziri wa maji, serikali ilipokea mkopo wa jumla ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 136, kutoka benki ya dunia kwa ajili ya miundo mbinu na kusambaza maji katika jiji la Dar esSalalm, katika juhudi za serikali ya awamu ya tatu chini ya rais mstaafu Benjamini Mkapa.
Baada ya kupata mkopo huo, Lowasa aliwatangazia wakazi wa Dar es Salaam na umma wa watanzania kuwa ndani y miaka 3 ijayo yani kutoka mwaka 2003 mpaka 2005 tatizo la maji lingebakia historia kwa jiji la dare s Salaam, lakini hadi leo haijulikani fedh hizo zilifanya kazi gani, huku tatizo la maji likibakia kuwa ple ple kwa wakazi wa jiji hilo.
Pamoja na mika mitatu kupita na akaja akawa waziri mkuu lakini hakufanya jitihada zozote za kukumbuka ahadi yake ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam mpaka anatoka katika nafasi ya uwaziri mkuu, Swali langu ikiwa ameshindwa ahadi yake ya kuondoa maji ndani jiji la dare s Salaam kwa miaka mitatu ataweza kuondo kero ya foleni kwa mwaka mmoja?
Chanzo Tazama
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment