Monday, 18 July 2016

Re: [wanabidii] JPM malizia kiporo cha Mwalimu

Lesian. Wakati ya Nyerere kulikuwa na magazeti matatu: daily News; Uhuru/Mzalendo na Mfanyakazi likimilikiwa na NUTA. Ungejua wapi habari za Kufuta uchaguzi au uteuzi wakati hazitoi?
Ukisema tunaendesha nchi kwa mawazo ya CCM wakati wenzako wanasema Rais anatekeleza sefra zetu ninapendekeza mtuchagulie moja. CCM inasikiliza na wapinzani kiasi cha kutekeleza sera zao au haiwasikilizi? nchi inajengwa ndugu. na wote tunachangia. Hata wewe
--------------------------------------------
On Sun, 7/17/16, 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] JPM malizia kiporo cha Mwalimu
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, July 17, 2016, 1:52 AM

Sukari bado ni ishu jamani, acheni
kutoa sifa ambazo hazipo...,hv mpombe mfano mdogo niwape
wakuu'zangu toka nyerere nadhan mlikuwepo mlishawahi
kusikia nyerere amteue mtu hafu akatae,'au amteue mtu
kimakosa...binafs ktk records zangu sina za uandishi wangu
wa habar-tho ni kanjanja ila sina
Hv niulize tena inakuaje wakuu zangu na ujenz huu wa Taifa
japo linalojengwa kwa msingi wa ccm pekee,ccm yenyewe
isiioelewena ,Taifa tutajengaje bila kuzingatia misingi ya
utawala bora-asieelewa aulize
Hv mfano tumeamriwa tusachiwe majumbani eti kwamba
watanzania wa Dar es salaam tujuane tunafanya kaz
gani-sijawahi kusikia hii toka nazaliwa ipo ktk serikali
yetu hii makini sana mnaosema bw mkubwa mpombe na elisa
inajenga nchi, sijui tunajengaje kiivyo.....
Mmeandika kurasi kibao kumwaga sifa, kwa kweli siungi hoja
yenu hata moja despite the fact of roaming around tne bush
with so many refferences ambazo hazie dani na hoja mnaotaka
kujenga bw mpombe, am a bit optimistic sir
Nchi inajengwa kwa uelewano, utawala bora misingi ya sheria
na ushirikishwaji wa wote, hakuna haja ya kutumia miguuvu
kisa tunajenga nchi....

'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
KUTAFAKARI mambo kwa yakini na umakini kuna raha yake,
moja ikiwa
kuupa ubongo changamoto mpya hivyo kufanya kazi kwa kiwango
cha juu
kuliko kilichozoeleka. Hili hurahisisha ugunduzi mpya,
utatuzi tofauti
wa mikwamo na ukomavu wa fikra.Kutafakari ndiko kumefanya wanazuoni mahiri tena maarufu
kuyang'amua
mambo mengi ambayo hayakuwa katika mazingira yao wala vizazi
walivyoishi
havikuyaishi lakini yamekuwa muhimu miaka mingi baada ya
kufa kwao
kimwili.Hata kizazi kilichopo, kile kinachothamini ukuu wa fikra kwa
wingi wake
ndani ya jamii zilizoendelea kina gunduzi (innovations)
nyingi,
changanuzi za nadharia, tafiti na vinginevyo ambavyo
vitakuja kutumiwa
kwa uaminifu, weledi na mafanikio miaka mingi ya vizazi
vijavyo.Tukiacha hayo, fikra moto na uwezo wa kusoma katikati ya
mistari ndivyo
vinafanya kuihoji nadharia ya kujenga taifa kupitia siasa za
Bara la
Afrika, na kutoa jibu rahisi kueleweka kwa mtu aitwaye wa
kawaida.Ujenzi wa taifa kwa muktadha tofauti unaelezeka kwa upana na
urefu
usiokutanika, kwa maana kwamba tafsiri ni nyingi tofauti
zenye malengo
dhahiri na siri kukidhi mazingira na watu husika. Ukiachilia
mbali maana
zenye malengo ya kimaslahi yanayofanya ujenzi uitwao wa
taifa kukosa
ukomo, ujenzi mahiri wa taifa ni ule timilifu ndani ya muda
unaotokana
na kukamilika kwa utekelezaji wa mipango, malengo na matakwa
ya wananchi
kwa ujumla wao.Ujenzi wa taifa ni ukamilifu wa ahadi za wajenzi wakuu,
viongozi na
serikali wanazoziongoza kwa kipindi husika. Ujenzi wa taifa
ni ule
unaokamilika, wenye mafanikio yanayoakisiwa katika maisha ya
kila siku
ya mwananchi; si ule unaoendelea kila mwaka bila kikomo!Nchini Tanzania dhana ya ujenzi wa taifa imekuwa ikisikika
tangu Uhuru
hadi sasa ambapo baadhi ya wanasiasa wanajinadi kuendelea
kujenga nchi
licha ya msingi wa taifa kusemwa ulishajengwa kwa ukamilifu
na Baba wa
Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere enzi za uongozi
wake.Hapa ndipo naweka hoja mezani kwamba; kama Hayati Nyerere
alifanikiwa
kujenga na kukamilisha msingi imara wa taifa katika kipindi
chake cha
uongozi, kwanini sehemu ya ujenzi iliyobaki haikamiliki,
haimaliziwi na
muda unazidi kwenda!Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John
Magufuli nahisi
anayo fursa ya kuibeba changamoto hii na kujipa kila sababu
ya kuingia
kwenye historia kuu ya nchi kwa kuifanyia mambo muhimu na
makubwa
Tanzania likiwemo hili la kumalizia ujenzi wa taifa
unaoendelea zaidi ya
nusu karne sasa.Rais Magufuli ambaye kwa bahati nzuri amepata kuwa waziri wa
ujenzi
naamini anajua gharama za ujenzi zinavyoongezeka maradufu
pale ujenzi
unapochelewa kukamilishwa ndani ya wakati uliopangwa.Binafsi najua Rais anao uwezo wa kufanya mambo mengi kwa
nchi
yatakayokamilisha rasmi ujenzi wa taifa kwa kuzitimiza ahadi
za viongozi
na serikali tangu awamu ya kwanza hadi hii ya tano ya
uongozi wa
Tanzania ili serikali zijazo zikose kisingizio cha kudai
zinajenga nchi
hivyo kukwepa kuwapa wananchi maendeleo. Huko tuendako
tungependa
tusisikie hadithi zisizoisha za ujenzi bali ukarabati na
uboreshaji kwa
kuwa hayo ndiyo maendeleo.Mungu mwenyewe aliujenga ulimwengu kwa maana ya kuuumba
pamoja na viumbe
wote ndani yake kwa siku sita, na akapata muda wa
kupumzika; iweje nchi
yenye watu wengi wenye kila aina ya uwezo na maarifa
wakiwemo wasomi
nguli iendelee kujengwa tu bila kukamilika au kujua lini
ujenzi
unamalizika!Hata maisha yanajengwa kwa wakati, yanatimia kwa miaka na
kutamatishwa
kwa kifo hapa duniani sembuse ujenzi wa nchi ulio ndani ya
uwezo wa
wananchi na viongozi wao kupitia mipango mahsusi ya
maendeleo!Bahati nyingine nzuri Tanzania imeongozwa na chama kimoja
tangu uhuru,
yaani TANU iliyobadilika na kuwa Chama Cha Mapinduzi-CCM
hivyo kufanya
kazi ya kukamilisha ujenzi kuwa rahisi zaidi kwa kuwa
msimamizi mkuu wa
ujenzi ni yule yule. Itakuwa heshima kubwa kama ujenzi
ulioanzishwa na
chama tawala utakamilishwa nacho chini yake Rais Magufuli
mwenye nia ya
dhati ya kuibadilisha nchi kuifanya ijitegemee kupitia
uchumi wa
viwanda.Kama Rais Magufuli na serikali yake wameweza kumaliza tatizo
lililoonwa
sugu la madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini kwa

kuwashirikisha wananchi na kuwashawishi wadau mbalimbali
pasi shurti,
suala la kumalizia ujenzi wa taifa linawezekana kupitia
utekelezaji wa
miradi inayosuasua, ahadi na mipango ya serikali
zilizotangulia.Kwa mfano; ujenzi wa eneo mojawapo la mbele unaweza
kukamilika mapema
zaidi kwa kukamilisha miradi yote ya umeme na kulipa uwezo
zaidi Shirika
la Umeme (ugavi ukiwemo) Tanesco ili Tanzania iondokane na
tatizo sugu
la kukatika ovyo umeme na kuwezesha nchi kuwa na nishati ya
kutosha na
ya uhakika itakayowezesha uchumi tarajiwa wa viwanda.Ujenzi wa taifa usiokamilika una athari nyingi. Ndiyo
unafanya watumishi
wa umma kuendekeza urasimu, kufanya kazi kwa mazoea,
kupalilia rushwa
na u-hewa hewa mwingi unaogharimu mabilioni ya shilingi za
kodi za
wananchi, achilia mbali migogoro mingi ya kujitakia.Hebu fikiri mzee mstaafu serikalini anapolazimika kufuatilia
majibu ya
barua ya madai yake stahiki kwa zaidi ya mwaka mmoja halafu
ofisini yuko
mtumishi wa umma anayelipwa mshahara kwa kazi ya kumhudumia
kwa wakati
mwananchi kama huyu mstaafu! Kuendelea kwa ujenzi ndiko
kunafanya
kuandika tu barua ya majibu iliyofika ofisini, kazi
isiyozidi dakika 10
eti kugharimu miezi kadhaa ya kufuatilia!Nashawishika kwamba serikali hii haitaacha mambo yaende
kimazoea zoea mbele ya macho yake.Najishawishi kwamba Rais Magufuli atamalizia ujenzi wa taifa
wenye
msingi uliokamilishwa kitambo na hayati Mwalimu Julius
Nyerere.Watanzania wamejibana kwa zaidi ya miaka 50 ili ujenzi wa
taifa
wanaoambiwa na viongozi wao ufanikiwe. Nafasi kubwa na uwezo
vipo
mikononi mwake Rais Magufuli kukamilisha ujenzi huu wa muda
mrefu ili
hatimaye Watanzania waanze kula matunda ya kujitolea,
kujitoa kwao,
kujibana na kufunga mikanda wakati wote ujenzi unapotajwa
kuendelea.Inawezekana.
 

Chanzo Rai
--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment