Monday, 18 July 2016

Re: [wanabidii] KUWAFUNGIA MATABIBU CLINIC ZAO: NI mkakati wa kukuza ubunifu au tunafanya tusichokijua?

Naungana nawe Elisa kwa maoni yako. Kinachotusumbua watanzania wengi naweza sema ni 'ushamba' uliopitiliza ukawa 'ujinga'.. Ujinga uliotusukuma wengi kuwa na wivu wa kipuuzi uliozaa roho mbaya.

Enzi ya Mwalimu, utawala wake na hasa yeye mwenyewe alikuwa na moyo wa kuwainua watanzania. kuwaonyesha wazungu kwamba ngozi nyeusi sio laana wala kukosa akili, ujuzi na maarifa. Yeye katika umri mdogo aliwahenyesha na wanalijua hilo. Kitendo cha kumteua kijana mdogo kwa umri wakati huo, Salim Ahmed Salim kuwa balozi kilishangaza wengi. Au alipomtuma kijana mdogo wakati ule kwenda israel kusomea uhandisi, marehemu Beda Amuri kilikuwa ni kitendo cha kuutambulisha ulimwengu kuwa ipo siku tutakwenda huko kwa weupe kuwafundisha kazi.
Mzee kaondoka na ujasiri huo. Nyuma wakabaki wasaidizi wake waliohusudu sana, wageni. Jambo likifanywa na mtanzania mwenye uchu wa kuchuma mali za halali kwa bidii yake, atakwamishwa sana. Reginard Mengi hata kama ana matatizo yake, kama sio kusimama imara asingefika hapo alipo. Serikali iseme imeweka mkono gani kwake kufika hapo? Dk Masau, mtaalamu bingwa wa magonjwa ya moyo alitendewa unyama wa kutisha na waliotakiwa kumuunga mkono kwa nguvu zote. Nina uhakika Dk Masau angekuwa mweupe, angelambwa hata miguu na kupewa kila ambacho angetaka. Lakini mswahi wa Majita, wapi na wapi.
Mzee wa kikombe cha Loliondo, alikimbiliwa kwa sababu aliegemea mambo ya Imani na Kanisa lake akiwemo askofu wake, wakamuunga mkono.
Kumbe akina Mwaka walitakiwa kusaidiwa pale walipokosea, kusudi waweze sasa kutenda vyema. sio kufungia bila kuangalia mtu huyu kasota vipi kufanikisha kazi yake


On Saturday, July 16, 2016 6:40 PM, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:Kuna dreva mmoja wa chuo kikuu Dar (UDSM) katibiwa cancer ya mguu kwa dawa ya miti shamba. Maisha yake yamekuwa mapya kwani hata kutembea alikuwa hawezi wakati Muhimbili na Ocean road wanatumia miale na mbinu sa kisasa. Hebu fikiria ni raha na furaha kiasi gani Tiba Asili imemponya! Full doze ni 450,000/= kwa matibabu ya miezi 3.

Cha kufanya ni Wizara ya Afya na Jinsia kutafuta mwekezaji au hela kujenga kiwanda cha kufyatua dawa ziwe katika unga, maji, mafuta etc na kuwa packaged kama inavyotakiwa. Mbona zinafanyiwa utafiti na kuthibitishwa na Muhimbili na Taasisi ya Utafiti wa Tiba asili kuthibitishwa na NIMR na TFDA? Zipo za kutoka nchi mbali mbali zinauzwa kariakoo. Baadhi ya tabibu hawakusoma kabisa wamerithi kutoka wazazi, bibi na babu na watu wanatibiwa wanapona. Madaktari wa Tanzania walipelekwa China kusomea barefoot doctors na kujua masuala ya Tiba Asilina Mbadala na ndio wapo wizarani kitengo cha Tiba Asili. Ulaya unanunua dawa asili packaged. Wajenge kiwanda kifyatue dawa kiusalama zaidi. Badala ya kushindana na kufungiana-dialogue inahitajika. Mbona Baraza la Wizara la Tiba Asili lipo na Vyama vya Waganga au Tabibu Asili vipo na vimeandikishwa kisheria. Wanakutana na Wizara kupitia wawakilishi wao ktk Baraza-dialogue inashindikana kivipi.

Kwenye waganga wa Tiba Asili kuna specialization pia-kutibu magonjwa mbali mbali na wengi wamesaidiwa kwa bei nafuu badala ya kwenda India kutibiwa  matibabu ya kisasa. Wanaotibu  pumu, malaria, parkinsons, uzazi, kupooza, kichwa kuuma etc kwa miti shamba/miti dawa na madini asilia au dawa asilia.

Tutatue matatizo kwa majadiliano na makubaliano kabla ya wahusika wa kuwafungia hawajaanza kwenda mwendo kazi barabarani na kuyapita magari ya sasa ya jiji ya mwendo kasi ili Tiba Asili aje kuonyesha mfano wa kumtibu ili apate kuheshimiwa!

Kama Kawa

--------------------------------------------
On Sat, 16/7/16, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] KUWAFUNGIA MATABIBU CLINIC ZAO: NI mkakati wa kukuza ubunifu au tunafanya tusichokijua?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 16 July, 2016, 16:53

Elisa,Nakuunga mkono. We are our own worst
enemy.em
2016-07-16 3:30 GMT-04:00
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Zamani
fulani niliwahi kuandika makala katika moja ya magazeti
iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: Wabunifu wetu wa
magobole wamo magerezani wakilindwa na magobole ya wabunifu
wenzao kutoka India.

Nilichosema ni kuwa Tanzania imewakamata watengeneza
magobole ambayo (magobole) yalikuwa hayakutengenezwa kwa
kibali. Na India hivyohivyo. Sisi watengenezaji hao wa
magobole tukawashtaki kwa kutengeneza magobole hayo bila
kibali cha serikali. India wa kwao ikawatafutia nyenzo
wakaendelea kutengeneza magobole na (India) kuanza kuyauza
nje. Sisi kwa kuwa tulikuwa tunatafuta bunduki za kulinda
magereza yetu tukagundua kuwa zile zinazouzwa India
zinatufaa. Tukazinunua na zikasaidia maaskari magereza wetu
kulinda wafungwa wetu wakiwemo wabunifu wetu wa magobole.
Nilipokuwa naandika makala hiyo kulikuwa na kesi mahakamani
na watu hao walihukumiwa vifungo kweli. Siyo India peke yake
inayogeuza 'uhalifu' kuwa Fursa. Uganda enzi za Obote
ilikuwa na shida ya waganda kutengeneza gongo wakati gongo
hilo ni haramu. Baadaye uongozi wa Obote ukachemsha kichwa
(okufumba omutwe). Wakawageuza wapika gongo kuwa wakala wa
'Uganda Waragi'. (kwetu ni Konyagi) hivyo Uganda waragi
ikawa inanunua Gongo na kulichuja na kuliweka kwenye chupa
hivyo tatizo likapungua, (halikuisha).

Tanzania ina dira yake sasa. Tunataka kujenga uchumi wa kati
ifikapo 2025. Njia moja wapo ni kukuza viwanda. Huo ni
mpango wa Taifa. Si serikali peke yake inayotekeleza pango
huo. La! Serikali, Taasisi za kidini, Wananchi, wataalamu wa
kila sekta, wanasiasa-wote tunatekeleza hilo. Ndiyo maana
wanaoona; vyama vya siasa walipofungiwa kufanya mikutano ya
kikampeni-tuliunga mkono. Tunaona wanataka kutupotezea muda
kwa kisingizio cha demokrasia.

Moja kati ya mikakati ya kutekeleza lengo hilo la taifa
wakajitokeza watanzania wenzetu wasomi wa mambo ya afya
katika ngazi ya kati (Matabibu) wakafanya utafiti kwa
kuoanisha magonjwa wanayoyajua kitabibu; na matibabu ya
kienyeji (Kiasili). Serikali kwa kutambua hilo ikawawekea
utaratibu. Waitwe watoa tiba ya asili au tiba mbadala.

Dawa ya kutibu malaria (kwa mfano) kwa dawa ya kienyeji, ni
bakuli moja ya lita moja mara mbili kwa siku. Wao kwa
kuangalia ukubwa wa lita na uwezo wa kuitumia wakajitahidi
wakaiweka katika unga na sasa wamefikia hatua ya kutumia
unga wa kijiko kimoja kwenye glass ya maji. Ni hatua
hiyo.

Watu hawa wameendelea na sasa wana clinics nyingi na
zinatibu magonjwa ambayo baadhi yameshindikana katika
hospitali zinazoitwa za kisasa.

Dawa zao zimepiga hatua kutoka kibakuli cha lita moja mpaka
glass moja. Wamepiga hatua kiasi cha kutengeneza vifungashio
vizuri tu vya kisasa. Wakasema sasa huduma zao ni za
'kisasa'. Kwa neno hilo wakafungiwa.

Majuzi rais wetu amewakaribisha wahindi kuja kuwekeza katika
viwanda vya madawa, badala ya kuendelea kutuuzia dawa.
Ukienda India baadhi ya viwanda vinavyotuuzia madawa hayo
viko uwani mwa nyumba za kuishi. Wanachofanya ni kutumia
majina ya viwanda vikubwa na luweka 'label' zao na
kuwalipa kamisheni. Ndizo tunazotumia na huwezi kujua labda
Mwijage (waziri wa viwanda) akienda huko. (Namuamini ana
uwezo wa kugundua hilo. Wengine hamna).

Miti inayotumika kutengeneza dawa ya Malaria ni Cinchona na
imezagaa na ndiyo Bukoba wanatengeneza dawa za
'Omushana' lakini China wanatuletea Malaraquine. Dawa za
Dr Mwaka tunasema za asili na akisema za kisasa tunamfungia
lakini za Mchina tunazikubali na kuziita za kisasa. Tofauti
ya dawa hizi ni moja: za wachina hatujui wanakozitengenezea.
Ndiyo tofauti. Kumbe akina 'Dr. Mwaka' wa China
walisaidiwa na serikali yao na sasa wanatuuzia dawa na sisi
tumefaulu kuwanyamazisha wabunifu wetu sasa tunataka 'Dr.
Mwaka' wa kichina na wetu tunaua. Dr. Mwaka akikosea
akaenda china na kuanzisha kiwanda akaiita 'hwa ngwi
chi', dawa zake zitanunuliwa tena kwa garama kubwa na
kutumika katika hospitali zetu za kisasa.

Hivi muda tunaotumia kumlaumu Dr. Mwaka na wenzake kwa
kutumia neno 'matibabu ya kisasa' badala ya
'asili/mbadala' kwa nini tusiutumie kumsaidia kuzifanya
dawa zake za kisasa? Kama tumehakikisha zinatibu; kama
tumehakikisha zinaboreshwa kutoka bulkiness mpaka small
packages; Kama amefikia hatua ya kuzifungasha
vizuri-tunashindwa nini kumpeleka mbele akawa wa kiwango cha
kisasa?

Kwa kuzima ubunifu Tanzania inaweza kusifika. Ukiondoa swala
la magobole, tunakumbuka jinsi Mafuta ya Ubuyu ulivyozimwa.
Ukienda Dodoma vijijini kukutana na mzee wa myaka 120
anakimbizana na mbuzi kama kijana ni jambo la kawaida.
'Watafiti' wa kyenyeji/asili/mbadala wa kitanzania
wakahusishaa matumizi ya mbegu za ubuyu na uzee mwema huo.
Wakafanya utafiti; wakayakamua na yakaanza kuwasaidia
watanzania kiafya na kiuchumi. Akakurupuka huko mtu na
kusema mafuta hayo ni 'hatari kwa binadamu'. Kulikuwa na
uvumi kuwa kuna mtu mmoja alitaka kuhodhi soko la mafuta
hayo na akaanza kwa kuzima wanaoyauza. Kwamba ni kweli au
sio hiyo siri kubwa.

Sipendi kuamini kuwa katika amri hii ya matibabu kufungiwa
ina swala la mahusiano ya mtu na mtu kwa makusudi ya
kukomoana. Tunafahamu kuwa kuliwahi kutokea mzozo kati ya
uongozi mpya wa wizara ya Afya na Clinic ya Dr. Mwaka.
Lakini nadhani hakuna mahusiano na si kusudi la makala hii
kulijadili. Kalamu imeteleza tu.

Ninachosema ni kuwa Tanzania inahitaji kufanya zaidi ili
kukuza sayansi. Lazima tujipe nafasi ya kutumia akili
zetu.

Nimesikia habari za uanzishwaji wa ''Jiji la sayansi'.
Nilisikiliza sana nikahofu tunaanza jiji hilo na kosa la
msingi ambalo litatupoteza njia. Mpango wa jiji hilo ni kuwa
Mtu mwenye degree akiwa na wazo la ubunifu atapeleka wazo
hilo. Wataalamu wenzake watalipitia na lifanyiwe kazi.
Najiuliza Wasomi wetu wenye degree wamewahi kubuni nini
kinachosaidia jamii. Waliofungiwa wote wako ngazi ya kati.
Matabibu; yaani Clinical officers (au Clinical Assistants).
Kama tutajikita kuwatumia wenye degree tu basi kukwama kwa
kutimiza lengo la kuanzisha jiji hilo kutaanzia hapo.Elisa Muhingo

0767 187 507-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya

 kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility

 for any legal consequences of his or her postings, and
hence

 statements and facts must be presented responsibly.
Your

 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to
the

 Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving
emails

 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.comKujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment