Wednesday 27 July 2016

Re: [wanabidii] 01.09.2016 Kosa jingine la kimkakati la Mbowe na CHADEMA

Maendeleo = kupanuka kwa uhuru na uchumi. One cannot be to the detriment of the other!

2016-07-27 16:34 GMT+03:00 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Nilifikiri nakutarajia kuwa kuwa Mbowe atatangaza kuwa kuanzia tarehe 01-09-2016 ni siku ya kwenda katika kila kona ya majimbo ya Chadema yote na kata na mitaa walizoshinda katika uchaguzi mkuu uliopita kushiriki na wananchi masuala ya maendeleo ikiwemo kuendeleza na kukusanya nguvu ya pamoja katika kuboresha na kujenga miundombinu mipya ya kuchochea maendeleo.

Ikiwa ni pamoja kupiga vita umasikini kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata vyumba vya madarasa, vyoo safi, vifaa vya mashuleni ili waweze kusoma na kuelewa vizuri katika kuleta maendeleo na demokrasia zaidi ndani ya chama ambayo bado ipo chini sana katika chadema ili kukifanya chama kije kuwa na wanamainduzi na viongozi wazuri wa baadaye.

Badala yake Mbowe anataka kuendelea kupambana na polisi na serikali ya Rais Magufuli jambo amabalo litakipotezea muda mwingi chadema na mwisho wa siku hakuna jipya ndani ya chama na kubakia kuitwa chama cha vurugu na maandamano nyasiyo na tija kwa wananchi.

Mwisho niwahusie Mbowe na chadema, wanachotaka kufanya ni kosa la pili la kimkakati badala ya kosa la awali walilolifanya la kukimbia bungeni amabalo halina tija kwa wananchi wala waoi wenyewe.

Mbowe na chadema badala ya kuendelea kufanya makosa ya kimkakati zaidi amabayo hayana tija kwa wananchi waliowachagua na badala yake wanataka kuendelea na maigizo wanayotarajia kuyafanya, Chadema haiwezi kufanikiwa kwa kutunishiana misuri na jeshi la polisi pamoja na serikali, watafanikiwa kwa kuleta mabadiliko katika majimbo na kata wanazoziongoza ili mradi tu kuonekanane tofauti ya kiuongozi baina yaoi na ccm tu.

Katika hili wanalotarajia kutaka kufanya, hakika sasa pengo la Dr. Slaa limeanza kuonekana live ndani ya chadema na ni bora Lowassa akatafuta njia ya kutoka humo kwa kuwa hawezi kuizuia chadema na siasa za uhanaharakati na hilo litamletea heshima zaidi kuliko kubaki ndani ya chama ambacho hawataki kubadilika.
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment