Saturday 30 July 2016

[wanabidii] HUU NI MGONGORO?? KUJICHANGANYA?? AU KWELI KUNA NAFSI YA TATU??

Jana Rais alitangaza msimamo wake kuhusu kusudio la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuitisha maandamanoo nchi nzima ifikapo Tarehe 1 September
Sababu kubwa ya CHADEMA kuitisha maandamano na mikutano nchi nzima ni kutetea demokrasia. Chama kinataja sababu kumi na moja nadhani nisizitaje
Baadhi ya sababu zinatafutiwa ufumbuzi katika vyombo husika. Mifano: Nakumbuka kuna kesi mahakamani kupinga zuio la polisi kuendesha mikutano ya siasa. Kuna wabunge wametuma rufaa kwa Spika kumshtaki Naibu spika. Hizi ni taratibu za kawaida kutatua migogoro inayojitokeza.
Kuitisha maandamano nchi nzima na mikutano ni kitu ninachosikia wengine wakisema ni kuleta 'Civil Disobedience'. Yaani kuwafanya watu wasitii mamlaka kama namna yao kutokubaliana na kinachofanywa na mamlaka. Mbinu hii imetumiwa mara nyingi. Misri ilifanikiwa kumuondoa Hosni Mubaraka kwa njia hiyo. Chauchesku wa Romania aliondolewa kwa njia hiyo. Watu walichoka na kila njia ilishindwa ndipo watu wakaingilia njia hiyo. Kwa hiyo CHADEMA imeona udhalimu unaofanywa na serikali Tanzania hauna mfano katika eneo hili la dunia ndipo wanaona watumie njia hii ya Civil Disobedience.

Rais anasema; Kulikuwa na kipindi cha uchaguzi. Kampeni ziliambatana na ahadi. Baada ya myaka mitano atapimwa. Ahadi zake zilitegemea kila mtu kufanya kazi pale alipo. {***Mkulima akilima. Muwekezaji atapata maligafi hivyo atajenga kiwanda. Nchi itakuwa ya viwanda. Katika kufanya hivyo atakusanya kodi. Hivyo atatumia kodi hiyo kutoa huduma za jamii}. Anasema hatavumilia kuona watu wanazuiwa kufanya kazi maana 2020 hatakuja kueleweka pale atakapokuwa anaulizwa ''kiko wapi kisima cha maji, Iko wapi Barbara ya lami". Anasema asiingiliwe katika kutekeleza ahadi zake. Bila shaka inajulikana kuwa atatumia vifaa tulivyompa kujihakikishia mazingira mazuri kutimiza wajibu wake kwa kibarua chake cha myaka mitano. {***Maana yake ni kwamba anayeona utaratibu huu haufai asubiri 2020 ajieleze kwa wananchi}.
Sipendi kuwa upande wowote kati ya pande mbili. Inawezekana kwa sababu na mimi nina upande wangu. Kuhakikisha Napata nilichokitaka wakati wa uchaguzi. Nao ni upande na ni upande mwingine.
Lakini najiuliza:
1) Ni kweli kuwa ili Rais atimize wajibu wake anahitaji watu kufanya kazi zao? Kama mimi nikiamua kutopalilia shamba langu la kahawa inamhusu nini Rais? Si akusanya kodi kwa watakaofanya kazi tu ili atujengee zahanai na barabara za lami?
2) Kama mtu akiona ni sahihi kutopalilia shamba lake la kahawa kwa hiyo hatafaidi bei-tarajiwa kujiendeleza kwa hiyo hali yake ikawa mbaya kiuchumi, 2020 atamlaumu rais na kwa hiyo kumnyika kura?
3) CHADEMA kama chama cha siasa kilichokuwa kikitafuta ridhaa ya watanzania kuongoza nchi, na kswa hiyo kinajitahidi kujionyesha kinaweza zamu nyingine; sasa kinaona ni wakati wa kuwakusanya watu saa za kazi ili kuigomea serikali-kimejihakikisha kuwa hayo ndiyo matakwa ya watanzania? Kinaona kina sababu za kitanzania na za watanzania wa sasa kuwashawishi waziache kazi zinazowalipa?
4) Hatua hizi za CHADEMA zinawiana na CHADEMA tuliyoizoea ambayo kati ya 2005 na 2015 ilionekana kuwavuta watanzania kwa hoja? Walipoibuka na hoja ya Ufisadi kila mtanzania alielewa. Walipoibuka na kashfa za Richmond, escrow na nyingine Watanzania waliwaelewa. Sasa wana hoja gani ya kitanzania? Watanzania wamepiga kura na wameridhisha na matokeo. Watanzania wana kero na sasa wanaona zinashughulikiwa. Watanzania wanajulishwa kila kinachofanywa na serikali. CHADEMA wanataka demokrasia gani na wanataka itusaidie kwenda wapi ili maisha yetu ya kila siku yaboresheke? Yaani wameona watanzania tumekosa nini kiasi wanaona watumie civil Disobedience kutupatia tunachokosa?
5) Kuna mamlaka yoyote nyuma ya mpango huu (nafsi ya tatu)? Ukosefu wa majibu sahihi hapo juu kunabakiza dhana moja kuwa huenda CHADEMA wanatumikia mamlaka fulani ndiyo maana wanafanya hata wasichokijua.
Kikundi cha wanaharakani enzi zile huko ufaransa kilipomwajili 'The Jackal' ili kumuua Charles Di-go kilitumia watu kubomoa BENKI ILI KUPATA FEDHA za kumlipa the Jackal. Walipokamatwa wezi walisema tunatumwa na viongozi wa kikundi hicho cha wanaharakati. Mmoja wa wanaharakati alipokamatwa akaulizwa fedha mlizotumwa kukusanya ni za nini akakutwa hajui. Kwa maelekezo ya jasusi huyo ilibidi siri iwe ya watu wachache. Swali Rais kusema 'kama kuna aliyewatuma -----' alikuwa sahihi au alisema tu? Yawezekana kuna mkakati ama wa kuivuriga CHADEMA au kuvuruga amani ya Tanzania na hii haijulikani kwa wengi?


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment