Sunday, 19 June 2016

[wanabidii] TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN KARATE 2018, NAHA CITY, OKINAWA, JAPAN.

Sensei Rumadha Fundi aliwakilisha bara la Afrika katika kongamano la wataalamu Karate !

TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN  KARATE 2018, NAHA CITY, OKINAWA, JAPAN.

Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza la OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" lenya makao Okinawa,Japan,juzi katika alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu magwiji wa karate lilifanyika Lisabon,Ureno.
 
 Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la  dojo iliyo jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato.

 Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.

Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate " European Jundokan  Gasshuku 2016".
Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" imefanya mabadiliko hivi karibuni yatakayo tofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayo kuwa katika michezo ya  Olympics.
 Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayo onekana katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.

  Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi,  zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  karate toka visiwani Okinawa duniania kote.
  Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayo tambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.

  Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu ( Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko Okinawa,Japan.

  Tunatumaini kwamba chama cha "JUNDOKAN SO HONBU" kitapata usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei Rumadha Fundi mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Afrika mashariki na Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza. Alimalizia hivyo; sensei Rumadha

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment