Saturday, 25 June 2016

[wanabidii] Kikwete apaa kimataifa, ateuliwa balozi wa heshima

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Balozi wa Hisani wa Taasisi ya Mafunzo ya Kilimo na Ushirika Vijijini (CTA) ya Nchi za ushirikiano wa Umoja wa Ulaya, nchi za Afrika, Caribbean, Pacific (ACP-EU).

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa CTA, Michael Hailu alisema uteuzi huo umetokana na mchango mkubwa wa Kikwete katika kusisitiza kilimo wakati wa utawala wake.

"Tunashukuru kwa kukubali kwake kuwa Balozi wa Hisani wa CTA, atatusaidia kufanikisha kazi zetu za kuhimiza kilimo endelevu kama injini ya ukuaji wa uchumi na mafanikio barani Afrika," alisema Hailu.

Alisema ana imani kwamba Kikwete atatoa mchango mkubwa kwenye taasisi hiyo ya CTA, na kuiwezesha kutekeleza kazi zake za kuhimiza kilimo chenye tija kwa ajili ya usalama wa chakula, uwepo wa lishe bora na kukuza uchumi kupitia sekta ya kilimo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment