Sunday 26 June 2016

Re: [wanabidii] Wasiomwelewa Magufuli wasiturudishe nyuma

Ningekuwa na uwezo wa maamuzi, na jinsi ninavyoona watu wazima wanaoingia bungeni kutoka daily na kuvaa vitambaa kusiba midomo na vurugu nyingine za kuudhi bungeni-ningeomba wanapofika vijijini kuhamasisha maandamano na migomo wanavijiji wachoke tabia hiyo na kuwashikisha adabu kuonyesha hasira zao kwa utendaji wao usiojali maslahi ya taifa ya wapiga kura wao na nchi kwa ujumla. Wananchi wakifanya hivi-wataacha tabia zao zisizo na taija kwa maendeleo ya nchi. Mtu mzaima baba na mama wa watoto unawaonyesha mfano gani wanao? Kila wakati ni kugoma tu, malumbano toka vyama vingi vianze. Mikutano na maandamano ya kupinga sereikali ndio imekuwa tija. Hawakuanza leo. Hivyo kila Rais mbaya. Kwa Maka Makinda na wengineo walifanya hivi wala hawajaanza kwa Dr Tulia tu. Kuongea kwa jazba ndio tija? Baada ya uchaguzi kuwe na mafunzo ya kuwaandaa wabunge kujitambua na kujua majukumu yao. Kama hakuna vitini vya miongozo-watengenezewe na vitumike kwa mafunzo. Tuna kila kitu nchi hii lakini utendaji na uwajibikaji finyu. Migomo, malumbano, maandamano na vibaka kuibia watu, misafara ya gharama badala ya kugharimia maendeleo jimboni kwa kutumia hizo hela ndio tumefanya tija. Wananchi watachoka, wakijakuchukua hatua mtakimbilia wapi na polisi hamuwaeshimu. Watakaa waangalie mnavyoumizwa. Hatuyataki ya Somalia, South Sudan, Syria, Boko Haram Nigeria na mengine ya vurugu. Tunapenda maongezi ya amani yenye tija na utendaji uliotukuka wenye positive outcomes.
Inakera!!
--------------------------------------------
On Sun, 26/6/16, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Wasiomwelewa Magufuli wasiturudishe nyuma
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 26 June, 2016, 15:31

MSAJILI wa Vyama
vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, juzi na jana
alikaririwa na vyombo vya habari nchini akitolea ufafanuzi
juu ya kauli
ya Rais, John Magufuli ya wanasiasa kuachana na porojo za
kisiasa,
akiwasihi wasubiri hadi mwaka 2020.

Amesema kiongozi huyo wa nchi hajazuia siasa, bali
anachohitaji ni
ushirikiano kutoka kwa wanasiasa wenzake ili kuwaletea
maendeleo
wananchi. Amelazimika kuyasema hayo baada ya wanasiasa wa
vyama vya
upinzani kuijia juu kauli ya kiongozi huyo wa nchi, wakidai
anaminya
uhuru wa kujieleza na kurudisha nyuma juhudi zilizopigwa
kidemokrasia.
Mara baada ya kupokea Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
25, mwaka
jana kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Alhamisi wiki
hii, Rais
Magufuli kwa unyenyekevu aliwaomba wanasiasa nchini kuacha
siasa kila
wakati na kuwataka kutumikia wananchi.
Kauli hiyo ilikuwa sawa na kuwakumbusha wabunge wa
upinzani juu ya
umuhimu wa kuwatumikia wananchi waliowachagua majimboni,
badala ya kila
mara kususia vikao vya Bunge na mambo mengine kwa madai
kuwa,
hawatendewi haki.
Katika siku za hivi karibuni, wabunge wa upinzani
wamekuwa na madai
kuwa wanabaguliwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na hivyo
kuamua
kususia vikao vyote anavyoviongoza, jambo linaloathiri
ushiriki wao
katika vikao vinavyoendelea vya Bunge la Bajeti kwa Mwaka wa
Fedha wa
2016/2017.
Aidha, kutokana na uonevu wanaodai kufanyiwa, na baada ya
baadhi yao
kutimuliwa bungeni kutokana na utovu wa nidhamu, walikusudia
kuzunguka
nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara, jambo lililopingwa
na Polisi,
ikielezwa kilichoonekana ni kama wanataka kuvuruga amani ya
nchi kwa
kuwachonganisha wananchi na serikali yao, kwani hawakuwa na
hoja ya
msingi.
Kwa kuona ushiriki wao duni katika kusaidia kusukuma
gurudumu la
maendeleo, pengine ndiyo maana Rais akazungumzia ubaya wa
siasa zisizo
na tija na jinsi zinavyowapotezea muda wanasiasa na
Watanzania kwa
ujumla.
Na katika kuonesha hana dhamira mbaya na wapinzani, Rais
alidiriki
kusema yuko tayari kushirikiana na wanasiasa hao ili
kufanikisha
maendeleo ya nchi yao. Ndiyo maana akawasisitiza kuachana na
siasa za
hivyo, ili wawainue kiuchumi wananchi waliowaamini na kuwapa
kura.
Ndivyo alivyokusudia Rais Magufuli, ndivyo walivyoelewa
wasomi
waliomwagia sifa kauli ya `kuachana' na siasa, lakini pia
ndivyo
walivyomwelewa wananchi walio wengi na ndivyo tulivyomwelewa
sisi.
Kwamba, siasa za kususa na kuvizia matukio ndiyo wengine
waibuke na
kuongea, zisipewe uzito kwa kipindi hiki cha mapambano ya
kuinua uchumi
wa nchi, bali kila mmoja alenge kuisaidia nchi kukua
kiuchumi kupitia
kaulimbiu ya `Hapa Kazi Tu'.
Wanachotaka kusikia Watanzania kwa sasa ni juu ya ustawi
wa nchi, si
malumbano na mipasho ya kisiasa inayoendelea hata baada ya
kumalizika
kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Nasi tunasema, kauli ya Rais ilikuwa na maana kubwa mno
kwa kuhimiza
ustawi wa nchi, tofauti na upotoshaji unaolazimishwa
kugeuzwa ukweli kwa
lengo la kutafuta umaarufu wa kisiasa. Kwa wakati tulionao,
ni vyema
tukaungana kuijenga nchi bila ya kujali itikadi za
kisiasa.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment