Wednesday 29 June 2016

[wanabidii] DKT. NDUGULILE ATAKA MABUNGE KUSHIRIKISHWA KWENYE MPANGO WA “AFYA MOJA” (ONE HEALTH)

Habari za jioni,

Tafadhali pokea CODES hapa chini

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile(Mb) ameyataka Mataifa kushirikisha Mabunge katika kufanikisha mpango wa Usalama wa Afya Duniani (Global Health Security Agenda).

Akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia,, Dkt Ndugulile alisema, "Mabunge yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kwenye utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani kwa kusimamia Serikali na kuhakikisha hatua zote muhimu zinatekelezwa; kutunga Sheria zitakazosimamia utekelezaji wa mpango huu pamoja na kuhakikisha mpango huu unapata fedha za kutosha kutoka kwenye Bajeti ya Serikali".

Dkt Ndugulile alisema kuwa muingiliano wa shughuli za kilimo, mifugo na shughuli nyingine za kibinadamu zimesababisha baadhi ya magonjwa ya wanyama kuleta athari kwa binadamu na pia usugu wa madawa ya aina ya antibiotiki. Hivyo, kuna haja ya wadau wa sekta hizi kuwa na ushirikiano wa karibu chini ya mpango wa "Afya Moja" (One Health).

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile (Mb) (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia.

Alisema kuwaIli mpango wa "Afya Moja" ufanikiwe in lazima maboresho yafanyike kwenye uratibu wa sekta mbalimbali ndani ya nchi na pia kuandaa mpango wa pamoja wa udhibiti na kushughulikia majanga.

Dkt Ndugulile aliyasema hayo kwenye mkutano wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani unaofanyika mjini Bali, Indonesia. Mkutano huu ulioanza tarehe 27 Juni unatarajia kuisha tarehe 30 Juni.

Dkt Ndugulile mbali ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mabunge Duniani (Inter Parliamentary Union) kuhusiana na masuala ya UKIMWI, Afya ya Wanawake, Vijana na Watoto.

Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
+255714940992.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment