[caption id="attachment_72766" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-72766" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/06/OTH_6916.jpg" alt="Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun.PICHA NA MICHUZI JR." width="640" height="412" /> Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR.[/caption]
[caption id="attachment_72767" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-72767" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/06/OTH_6900.jpg" alt="Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma." width="640" height="426" /> Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma.[/caption]
[caption id="attachment_72765" align="aligncenter" width="640"]<img class="size-full wp-image-72765" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/06/OTH_6925.jpg" alt="Mratibu wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini." width="640" height="426" /> Mratibu wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini.[/caption]
<strong>KAMATI</strong> ya Maandalizi ya tukio la Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.
Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati ya Maandalizi ya harambee inajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari chini ya Uenyekiti wa Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda, inaomba ushirikiano wakaazi wa Dodoma pamoja na Wabunge. Mtakumbuka kwamba kamati hii ilifanya tukio kama hili viwanja vya Leaders, Jijini Dar es Salaam July 4, 2015, ambapo zaidi ya 30m/-, zilichangishwa.
Fedha hizo zilisaidia gharama za matibabu ya waandishi watatu waliokuwa mahututi wakati huo, mmoja wao akiumwa kansa. Lengo la mwaka huu limebadilika ambapo tumekusudia kuhakikisha kuwa wengi wao wanakatiwa bima ya afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi. Aidha, kwenye changizo hili tutakuwa na kadi maamlum za kuomba michango ya mfuko huo, ambazo tutazigawa kwa Wabunge kupitia ofisi ya Bunge. Tutaomba ushirikiano mzuri kutoka kwa Wabunge na wakazi wa Mji wa Dodoma ili kufanikisha zoezi hili.
Pia tumeandika barua kwa Spika tukimwomba awajulishe Wabunge ili wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi hili. Waratibu wa Harambee ile ambayo ni Kampuni ya Media Assistant, imefanya utaratibu wa kumleta Miss Tanzania Ms Lilian Kamazima pamoja na wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva kuja kushiriki zoezi hilo.
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment