1. Mahanga amvaa Magufuli..
Ni habari inayopewa nafasi ya kwanza kwa uzito na mtandao wamjengwablog.com. Ni kauli iliyotolewa na Waziri wa Awamu wa Nne kuelekeza shutuma kwa Rais wa Awamu ya Tano.
Habari hii si kubwa kwa tafsiri ya kilichosemwa na Mahanga bali ni kubwa kutokana na aliyekisema. Haipaswi kuwa ya kushangaza wala kutiliwa maanani sana. Makongoro Mahanga ni muhanga wa harakati za kisiasa. Moja ya sababu zilizopata kutolewa kwa yeye kuhama CCM na kwenda Chadema ni kukaa kwa miaka kumi ndani ya Serikali ya JK kama Naibu Waziri. Mahanga hajapata kuwa Waziri Kamili, kama UKAWA ingeingia madarakani bila shaka ndoto yake ingetimia.
Makongoro Mahanga amekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira kwa miaka mingi. Wakati akisubiria kufanywa Waziri Kamili , hakuwa na mengi aliyoyafanya ya kuonyesha umuhimu wa uwepo wa wizara hiyo. Si jabu nayo ni moja ya wizara ambayo shughuli zake zimeunganishwa na wizara nyingine.
Makongoro Mahanga anajua, lakini, kwa makusudi anapotosha umma. Anajua kuwa kuna tofauti ya ukubwa wa Baraza la Mawaziri na ukubwa wa Serikali kwa maana ya watendaji Serikalini. Makatibu Wakuu na Manaibu wao ni watendaji wa shughuli za kila siku za Serikali, si mawaziri na manaibu mawaziri. Mfano, shughuli ambazo ziliwekewa wizara, kama kazi na ajira ambapo Mahanga alikuwa Naibu Waziri, sasa zimeunganishwa na wizara nyingine na ndio tafsiri ya baadhi ya wizara kuwa na makatibu wakuu watatu. Walau hawa watakuwa wanakwenda kila asubuhi kufanya kazi zenye kuhusiana , mathalan na kazi na ajira zilizounganishwa na wizara nyingine , badala ya kuundiwa wizara yake yenye Katibu Mkuu, waziri na naibu waziri wa aina ya Mahanga anayenung'unika kwanini hafanywi kuwa waziri kamili.
2. Wananchi 100 wavamia shamba la Sumaye
Hii ni habari inayochukua nafasi ya pili. Wananchi waliobomolewa nyumba zao na kuhamishwa maeneo ya mabondeni wamevamia ekari 33 za Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye eneo la Mabwepande. Habari hii inatukumbusha mgogoro unaoendelea kufukuta katika jamii kuhusiana na ardhi. Sumaye anaweza kabisa kuwa anamiliki eneo hilo kihalali, na kwamba wavamizi hawana haki kisheria kumuingilia. Lakini, ukweli huo hauondoi hoja ya msingi kuwa, baadhi ya viongozi, sio Sumaye tu, wamekuwa na hulka ya kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi katika sehemu za nchi, na mara nyingi, bila kuyatumia kwa shughuli za uzalishaji. Imefika wakati, wa kutunga sheria itakayowalazimisha, wale wote wenye zaidi ya ekari tano, walipie kodi kila ekari inayoongozeka, walau kwa kiwango kitakachowekwa kwa mwaka, kimfanye anayemiliki awe na mawili ya kuchagua, ama atumie kwa uzalishaji eneo alilohodhi, au arudishe kwa Serikali ya kijiji.
3. Darasa moja lajengwa kwa milioni 200
Hii ni habari inayopewa uzito kwa nafasi ya tatu. Huko Mbeya imetolewa ripoti kuwa kwenye shule za Sekondari zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi kuna darasa limejengwa kwa shilingi milioni mia mbili. Huo bila shaka yeyote ni ufisadi mkubwa, vinginevyo kama ni ' Darasa Ghorofa'!
Usikose kusoma habari hizi kwa undani , ikiwamo habari kubwa ya michezo na katuni bora ya leo. Ni kwenye http://mjengwablog.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment