Sunday, 3 January 2016

Re: [wanabidii] Elimu ya Awali-Chekechea

Kwangu Elimu ya Chekechea ni muhimu sana. Elimu hii huanzia miaka 3 hadi 4 na inafuata mtindo wa Montessori. Yaani mtoto anajifunza kufanya kitu kadiri ya mazingira yake. Na ndio maana mtindo wa montessori ni vitendo zaidi. Mtoto anawekewa vitu vingi mbele yake. Kuchora, kupanga vitu, kuunganisha picha au vitu mbali mbali, kuhaulisha maji  kwenye chupa bila kumwaga chini, kucheza nk. Hapa mtoto anaanza kufikiri kufanya kitu. Darasa hili kipaji cha mtoto hujulikana kirahisi. Pia hujifunza silabi rahisi na kuhesabu. Kwa mfano kuruka na kuhesabu 1,2, 3... Kuanzia miaka 5 hadi 6 mtoto anafundishwa kusoma na kuandika na kuhesabu. Mwaka wa 7 aende moja kwa moja darasa la kwanza. 

Mtoto akiwa na shule nzuri ya chekechea darasa la awali halihitajiki. Naona Darasa hili ktk shule zetu, halina mwalimu wala chumba. Mara nyingi watoto hufundishwa chini ya mti. 

Mie napendekeza Darasa la awali lifutwe kama tuna shule nzuri za chekechea. Sababu ya msingi ya kufuta darasa la awali, hakuna waaalimu wala vifaa vya kufundishia wala vyumba vya madarasa. 




From: 'Athanas S. MACHEYEKI' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: Mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; "mabadilikoforum@googlegroups.com" <mabadilikoforum@googlegroups.com>
Sent: Sunday, January 3, 2016 6:20 PM
Subject: [wanabidii] Elimu ya Awali-Chekechea

Wana Mabadiliko,

Mimi huwa ninafikiria sana juu ya umuhimu wa kuwa na elimu ya chekechea hasa ktk nchi yetu. Hivi ni kweli kwamba tunaihitaji elimu hii kwenye sekta ya elimu? Je, ikiondolewa itaadhiri nini kitaaluma kama Elimu ya Msingi itatolewa ipasavyo?

Naomba kuwasilisha.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment