Happy tunashukuru kwa mwangaza ulotupatia. Labda mimi kwa umbumbumbu wangu wa sheria nikisie walichokikusudia.....labda walitaka kutueleza kuwa ...Albino nao wana haki ya KUISHI katika eneo lote lilitotamkwa katika ibara /aya husika.....Labda ingalikuwa vema zaidi kama ungalienda kuwauliza kwanza kabla ya kutuwekea mtazamo huu....
On Wednesday, 25 March 2015 13:26:26 UTC+1, Happiness Katabazi wrote:
-- Labda ...mimi si mwanasheria nimeongelea tu kimtaaani mtaaani....
On Wednesday, 25 March 2015 13:26:26 UTC+1, Happiness Katabazi wrote:
CHANEL TEN,MAGIC FM TANGAZO LENU HILI LINAPOTOSHA KATIBA YA TANZANIA
N a Happiness Katabazi
BINAFSI ni mtazamaji na msikilizaji wa televisheni ya Chanel Ten na Magic Fm kwa lengo la kupata habari na kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa siku kadhaa nimekuwa nikilitazama,kusikiliza tangazo moja linalorushwa na vituo hivyo vya utangazaji .
Tangazo hilo ambalo linaonyesha picha za sura za ndugh zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
Maudhui ya tangazo hilo linataka mauji ya albino yakome kwani albino ni binadamu kama sisi na na tangazo hilo likasema eti ibara ya Ibara ya 2 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatoa haki ha kuishi.
Binafsi muda wangu mwingi utembea na kupenda kusoma baadhi ya Sheria ikiwemo sheria Mama ambayo ni Katiba ya nchi kwaajili ya kujifunza mambo mengi ya kisheria.
Baada ya kusikiliza tangazo hilo nimebaini tangazo hilo limefanya limekosea katika kunukuu jbara hiyo ya pili kwani ibara ya pili ya Katiba ga nchi haizungumzii kabisa haki ya kuishi.
Ibara ya pili ya Katiba ya nchi inazungumzia mambo haya ,naninanukuu kama ibara hiyo inavyosema:
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge:
Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo".
Na kwa faida ya vituo hivyo vya utangazaji niwarahisishie kazi kuwa haki ya kuishi inapatikana katiba ibara ya 14 ya Katiba ya nchi na siyo ibara ya pili kamamlivyoupotosha umma kupitia hilo tangazo lenu kuwa eti ya kuishi inapatikana katika ibara ya pili ya Katiba ya nchi.
Ibara ya 14 ya Katiba ya nchi inasomeka hivi,na ninanukuu: " Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake,kwa mujibu wa sheria".
Waswahili wanamsemo mmoja usemao ' Muungwana asifiwi ushenzi'.
Naaminj vituo kwa kosa hilo vitawaomba radhi watazamaji na wasikilizaji wake kwa makosa hayo ya kunukuu vibaya ibara ya Katiba ,kisheria tunaita ' wrong citation' , na kisha itaenda kulifanyia marekebisho tangazo hilo kwa kuweka ibara sahihi ya Katiba ili jamii isizidi kujifunza na watu waache kuua albino.
Wito wangu kwa vyombo vya habari yaani magazeti ,redio,telegisheni viwe makini katika hasa kunukuu baadhi ya vifungu vya sheria kwani vikinukuu kimakosa vikae vikijua umma ambao ni wavivu wa kutotaka kufanya utafiti yale yanayotangazwa na kuandikwa katika vyombo vya habari unaamini na kusadiki katika upostoshaji huo.
Nimejiuliza hivi Chanel Ten,Magic Fm haina Mwanasheria wake ambae hasa katika tangazo hilo angeusishwa kikamilifu atoe mchango wake wa kitaaluma ya sheria?
Lakini hata huyo naye aliyekubali kutia sauti yake katika tangazo lile naye kabla ya kwanza kukubali kuweka sauti yake katika tangazo lile ,alishindwa kabisa kutafuta Katiba ya nchi kuisoma ili ajilidhishe ibara ya pili anayoitangaza katika tangazo hilo kweli inasema hivyo?
Ikumbukwe kuwa makosa kama hayo yanashusha heshima ya vituo vya utangazaji na vyombo vya habari kuwa hampo makini na kazi zenu na kusababisha baadhi ya watu wapoteze imani na taarifa zenu.
Lakini hata hiyo Idara ya Katiba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina maana halilisikia au kuliona tangazo hilo ambalo limenukuu ibara isiyo sahihi?
Ikumbukwe kuwa kifungu cha 8 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , inasema kutofahamu sheria siyo kinga kutoa adhibiwa.
Nashauri katika habari au matangazo yanayo husisha taalamu kama udaktari, sheria na fani nyingine mbali na taaluma yenu ya uandishi wa habari basi wahusisheni kwanza wanataaluma hao ili wawape utaalamu katika eneo la fani yao ili msiendelee kuwa vichekesho au kupotosha jamii.
Mungu ibariki Tanzania.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Machi 25 mwaka 2015.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment