Sunday, 29 March 2015

Re: [wanabidii] Kesi ya Mtikila Mahakama ya Kadhi yapangiwa Jaji.

Suala hili linashangaza kwani kila dini ina mahakama yake na mfumo wake waumini wanaoufahamu wa kushughulikia masuala yote ya kesi za waumini. Kwanza waliowengi hawatumii mahakama za kidini wanakwenda serikalini kupata haki sawa kuogopa kubaguliwa kidini. Pale hasa mwanamke anaponyimwa haki ya miradhi au kuwa vigumu ndoa kuvunjwa ingawaje miaka kadhaa wanandoa hawaishi pamoja, kulala vyumba tofauti, kupigana, kutesana halafu dini haitambui talaka na mkitengana huzikwi, kuruhusiwi kukomunika, suala mpaka lifike kwa Baba mtakatifu kuamuliwa likishindikana TZ ktk vyombo vya dini vya mahakama ya RC. Ukifanywa utafiti-itaonekana dini ya kikristu na kiislamu wengi hutumia mahakama ya serikali sio ya dini. kama bill hiyo ipite-kesho wataingia madhehemu mengine na muswada iwe Hindu, Bohora, pentecoste, Katoliki na madhehebu mengi sana ambayo yanamgawanyiko pia. Serikali itaweza kugharimia mahakama hizi zote? Mbona tayari inazitabua na inapokea kesi
zilizoshindikana na kushughulikia masuala ya mirathi, watoto, talaka? inatoa vyeti vya ndoa vya aina moja pia ambapo Padri au Sheikh anatoa cheti kinachotambulika na serikali? Kuna nini hasa kinachotafutwa kwa nini Mahakama za kidini zisibaki huko katika mahekalu, ziendeshwe na hizo dini ila serikali izitambue inapopokea rufaa ya kesi na kutaka vidhibiti tu vya mahusiano, udugu, etc? Tunajitafutia balaa. Wengi hatuelewi chanzo cha suala hili hasa ni nini? Misikiti, Jamat na mahekalu yameshindwa kushughulikia masuala yao au kunatafutwa mchafuko hili liwe kisingizio? Mungu atusaidie.
--------------------------------------------
On Sun, 29/3/15, 'frank patrick materu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Kesi ya Mtikila Mahakama ya Kadhi yapangiwa Jaji.
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 29 March, 2015, 10:13



By Hellen
Mwango

26th March
2015

Mahakama Kuu
Tanzania, Kanda ya Dar
es Salaam, imepanga Machi 30, mwaka huu kusikiliza kesi
iliyofunguliwa na
Mchungaji Christopher Mtikila, akipinga kitendo cha Serikali
kupeleka Muswada
bungeni wa kutunga sheria ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi,
kwamba uko kinyume
na Katiba ya nchi.

 

Kesi hiyo
imepangwa kusikilizwa na
jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Richard
Mziray.

 

Katika kesi
hiyo, Mtikila ameiomba
mahakama itoe amri kwamba wale walio kwenye mamlaka ya
Serikali  akiwaemo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Mahusiano na
Uratibu), Mary Nagu; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.
Asha-Rose Migiro;
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Waziri wa
Kilimo, Chakula na
Ushirika,  Stephen Wasira na wenzao watoe sababu kwa
nini wasifungwe
kifungo kisichopungua miaka mitano endapo watashindwa
kujieleza.

 

Pia, Mtikila
kupitia hati yake ya
madai iliyopewa usajili namba 14 ya mwaka huu, ameomba
mahakama itoe amri ya
vigogo hao kufungwa kifungo hicho kutokana na kuchezea
Katiba ambayo ni sheria
mama ya nchi.  

 

Pia, Mtikila
anaiomba, Mahakama itoa
amri kwamba Mahakama ya Kadhi na Jumuia ya Kimataifa ya
Kiislamu (OIC) itangaze
ni haramu kwenye ardhi ya Tanzania.

 

Kadhalika,
anadai kuwa suala la
serikali kuandaa muswada wa Kiislamu na kuuwasilisha bungeni
na kitendo cha
Bunge kukubali ni sawa na uhaini.

 

Anadai kuwa
kitendo hicho ni sawa na
uvunjifu mkubwa wa viapo walivyoapa viongozi hao wakati wa
kushika madaraka ya
umma na ni kinyume cha ibara ya 19 ya katiba ya nchi
inayoeleza kwamba masuala
ya dini na kuabudu yatakuwa ni ya mtu binafsi na kwamba
uendeshaji wa mambo au
taasisi za kidini hazitakuwa sehemu ya mamlaka ya
nchi.

 

SOURCE:
NIPASHE






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment