Monday 30 March 2015

Re: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!

Mifano ni mingi pamoja na huo wako. Saa mbili asubuhi vitoto vimetoroka au haviendi shule vinacheza hiyo pool table. Mwenye hiyo ni mzazi hapo kijijini. Hapo ni kijijini porini. Wenye dish ya satellite na music system za betri za gari ndio wanaonyesha video mpaka za mapenzi, watoto wanatoroka au hawaendi shule wapo ktk video na anayemiliki ana uwezo wengine ni viongozi wa kijiji. Kilabuni kila mtu anakwenda na radio ni kelele za music wengine kanda za nyimbo watu wanacheza mpaka dansi za matusi ya nguoni. Watoto wapo pale kuuza karanga, mihogo etc kupata hela zao na za familia wanaona yote wazazi au watu wazima wanavyopapasana, kucheza kimatusi, kwenda haja hovyo utupu nje-amelewa. Hili ndio taifa tunalolijenga. Vilabu na video, pool table etc ndio sehemu za kijiji kupata mapato. huwezi kuzuia na mmiliki atakushughulikia kiana. Machimboni ni balaa. Wanachafua mazingira na watoto wanaajiriwa kuchavanga unga wa dhahabu kutumia mercury ambayo ni
neurotoxin. Hivyo tutakuwa miaka ya mbele taifa la zombies.


Viongozi wanaona uchafuzi wa maji ktk machimbo ambako wapo juu milimani katika chanzo cha maji, au wanakoshea ktk mto tegewewa na kijiji, mji, miji kwa maji ya bomba ya halmashauri, kijiji; pia mito huingia ziwani kama lake victoria au kwenye bwawa ambako pia hufuga na kuvua samaki au kuingia mabwawa ambayo malambo ya kunywa watu na mifugo hutegemea kama chanzo cha maji au maji yenye madini hatarishi kufurika wakati wa mvua na tunayakajana na kuingia katika vyanzo vya maji ytuogayo, tunywayo. Tunaiona, tunafumba macho-usiwaondoe wapiga KURA. Na kipindi hiki ndio uvamizi maeneo nyeti, hatarishi yataongezeka na pia majengo ktk maeneo yanayokatazwa kwa tumefikia uchaguzi. Huwezi ukabomoa au kuhaondoa kwa nguvu unaogopa kukosa KURA. Lakini madhara yake ni ya kudumu kimazingira na kimwili, kiuzawa, ongezeko la gharama na majeti ya matibabu, vilema. Pita Jangwani Dar uone hapo bondeni jangwani mijengo ya gharama inavyoongezeka-Waheshimiwa wanapita hapo
wanaona. Morogoro-wanapima viwanja katika wetlands, wanafukia wetland na kujenga maviwanda, majumba. Madhara yanaonekana. Mbona South Africa-Capetown, Switzerland wamejenga milimani kwa uangalifu na utunzaji mazingira. Tunajenga wetlands tunafanya wananchi wapande milimani kunakokatazwa -kulima, kuchimba madini ili wapate kula/kuishi. Vyuo vya ardhi kazi yake nini? Vyuo vya Ustawi jamii, maendeleo, Environmenta engineering vinapeleka wanafunzi wapi kufanya field practice kama sio vijijini, mijini na kushauri upangaji matumizi ardhi. Bibi/Bwana Maendeleo Kata, Afya Kata, DMO, Katibu Tarafa na Diwani wapo-uharibifu, upotovu maadili unaendea wanaona. Nao hao wa Kata, tarafa utawakuta wanapita kukusanya kodi huko ktk uharibifu na uchafuzi mazingira migodini. Tumboni street na siasa-vinatumaliza. Viongozi wa mila wanaona wafanyayo vilabuni, kijijini-nao wapo hapo kilabuni wanalewa. Kila kiongozi anatembea na mhuri wa ofisi anagonga hapo alipo unampa
chake.Anagawa mpaka ardhi za ukoo ambazo zi zake. Migogoro ya ardhi inakua na atahonga na kuchaguliwa tena-anao anaokula nao.


Serikali ihakikishe tunaondoka hapa tulipo ujingani mpaka kufanya monitoring ya mashamba au ardhi ya wawekezaji itakayogawiwa kwa wananchi. Kwani, watatoa maelfu ya ekari kwa wananchi, waliowengi watauza, watahamia mijini au watakuwa squatters barabarani. Sehemu nyingi walipopewa ardhi wamefanya hivi na baadhi hawalimi hujenga vilabu vya pombe, migahawa, lodging, modern bars. Tunabaki pale pale kulalamika na kuvamia wawekezaji. Wamevamia maeneo ya Wazo hill yenye hati, ya Benaco kampuni ya ujenzi-wameuza; wameuza Tegeta, Salasala, wapo mashimoni kunakojaa maji kunduchi na huko biashara ni pombe, vitafunwa. Ni hivyo ardhi yenye rutuba nzuri na misitu ya wahenga Mkuranga, Rufiji itakavyoisha mchele tuagize kutoka China na kisha tulalamike. Mbona ulaya kuna Town and Cities with Farms why not Africa tunashindwa nini??? Inakera. Tumewekeza katika kununua rahisi na kuuza ghari vya China, Dubai, India, Uk, Germany. Viwanda tumegeuza stoo za vyuma chakavu.
iteni Wachina waje kufufua Viwanda, wanunue bidhaa za waannchi, watoe ajira ili mkulima na mfugaji, mvuvi auzie hivyo viwanda tule, tuivae vinavyozalishwa nchini. Mawaziri na Wabunge hawaoni haya ya waliochukua viwanda kupangisha wenye biashara za mitumba, maduka ya jumla ya pombe na kuweka magunia ya used items toka nje ya nchi? Hivi sisi watu weusi hata tusome akili zetu na macho yetu yanakuwa taahira na vipofu vipi?

Cha aibu cha mwaka-Ni pale wenzetu wenye ualbino tunaowatetea na dunia kuwatetea walipopigana hadharani kugombea madaraka na mengineyo bila hata ya aibu-Ya mwaka hii. Aibu ilioje-Africa, kichwa cha mwendawazimu.

Kwenda ulaya sio jawabu-yote ni hano hano yanatatulika. Tuvae njuga, tufanye kweli.



On Mon, 30/3/15, 'Sylvanus Kessy' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, 30 March, 2015, 21:09

Dada Kiwasila umesema
kweli. Vijana hawataki kufanya kazi za kuzalisha. Wanataka
kazi za kutoa huduma tu, kama kuuza vocha, juice, sigara na
majani ya chai, kucheza kamari na pull!  Kimsingi katika
haya uzalishaji ni 0.

Nilipotembelea kijijini kwangu, nimekuta kesi
moja. Kijana alioa na Mungu akamjalia watoto 3. Kutokana na
kulewa pombe na kumpiga mkewe, Mke akaondoka zake. Hakuacha
nyuma watoto kwani alijua watateseka maana Bwana hana mpango
wa kutunza familia.

Bwana
baada ya kuona mke ametoka, akauza shamba lote na kibanda
cha nyumba kilichokuepo akabomoa na kuuza bati chakavu kwa
bei poa ili kupata hela ya kulewea. Hivyo Bwana huyo wa umri
wa kati (47) ametokomea mjini. Hana mawasiliano yoyote na
ndugu wala mkewe.

Nadhani
huyu atakuwa mkimbii mpaka mwisho wa maisha yake. Atakakofia
Mungu anajua.



--------------------------------------------
On Mon, 3/30/15, 'Hildegarda Kiwasila'
via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Subject: Re:
[wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!

To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, March 30, 2015, 8:19 AM


Foundation
For Civil Society imegharimia Youth Empowerment
na kuzipa NGO hela ambazo zilitoa mafunzo,
kuwasaidia vijana
miradi ya kuzalisha mali
kama ufugaji kuku, mbuzi na ng'ombe
wa
maziwa, mbegu za mashamba ya kilimo kama mahindi, mbaazi,
mpunga, vitunguu; ushonaji; ufugaji nguruwe
walipotaka;
mizinga ya nyuki. Walipotaka
kuanzisha kukopa na kupeana
hela
mzunguko-hawajarudisha toka 2008 walipopewa hela laki 1
revolving funds kopa ulipe na faida mwingine
akope.
uzalishaji mali, kilimo kimekufa,
wapo ktk bajaji na
pikipiki, udalali ktk
taxi, mabasi malori kupakia watu
wasichana
wamerudi bar vizee ndio vinalima, vinafuga,

vinatumia irrigation pamoja na drip irrigation. Wao
(vijana)
kwenda kuiba mazao usiku kupakia
ktk mafuso kupeleka mijini
kuuza. Mijini ni
hivyo-vikundi ufisadi kugombea madaraka,

kufisadi hela walizopewa kufanya ujasiriamali.
walikoanzishiwa miradi na SACCOS kuna story za
kukopa na
kutoroka mpaka familia hulipi
deni unaogopa kuporwa
  vigodoro. tusaidie
vikundi vinavyojiunda vyenyewe sio vya

kuundwa kimradi wana ubadhilifu. Miradi mingi ay vijana
imejaribu kuwafanya wajasiriamali michache
imefanikiwa.
Hatupendi kujituma ni tabia na
hulka yetu.

  Serikali
kuahidi ajira wakati ni ujuzi, elimu, skills zako
zikuuze nawe interview inakutupa-italaumiwa
bure. Hebu
matajiri wafungue mashamba,
wajenge nyumba na kufungua
wiwanda EPZ
wawape ajira wenye elimu wasiojiweza. Wasichukue
viwanda kugeuza godowns za mitumba kuuza
jumla, store za
spare used za magari etc.
Kila kona kila duka mitumba, nguo
toka
china, spare za magari; chips na bar. Huku tutoke.
Wenye uwezo wachukue mashamba ya GVT tufanye
kweli ili
vijana wakatoe nguvu kazi. Wageni
wanakuja wanawekeza kisha
tunawavamia
kuchoma moto mali zao. Sisi wenyewe mashamba ya
akina babu tuliyorithi tunayauza, tunalewa
hakuna la maana
tufanyalo tunahamia mijini.
GVT ikigawa maekari ya mashamba
kwa
wanavijiji-tunauza. Hati zipigwe muhuri-hakiuzi, kuuzwa
ni illegal. hii isaidie kuzuia ujinga tufanyao
sisi wenyewe
kuuza ardhi zetu.


--------------------------------------------
On Mon, 30/3/15, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
wrote:

 
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!
  To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
  Date: Monday, 30 March, 2015, 2:05
 
  Kessy,
  Tatizo linalowakimbiza vijana wa nchi za
  Kiafrika ikiwemo Tanzania katika nchi za
Ulaya ni
  unemployment na maisha yasiyo na
matumaini tuliyoletewa na
  sera za CCM.
  em
 
 
Sent from my iPhone
 
 
> On Mar 29, 2015, at 2:20 PM,
 
"'Sylvanus Kessy' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
  wrote:
  >
  > Ndugu
  wanabidii
  > Hivi karibuni nilikuwa
  safarini Nchini Ujerumani. Na moja ya mambo
niliyoyakuta
ni
  kwamba
siku hizi nchini humo kumefunguliwa makambi sehemu
  mbali mbali ya wakimbizi. Wengi wao ni
kutoka nchi za
  Afrika. Nadhani mnasikia
mara kwa mara kuhusu wakimbizi
hawa
  ambao huenda Ulaya kwa njia ya hatari ya
Meli. Wengi hufa
  bahari kwa hali mbaya ya
hewa au hata kwa kutoswa.
  >
  > Nchini Ujerumani
 
nilikuwa katika Jiji la Munich. Nilibahatika kuona moja
ya
  kambi hiyo, ila kwa bahati mbaya
sikuruhusiwa kuingia.
  Niliambiwa kadiri
ya orodha yao kuna WATANZINIA WAWILI.
 
Nilipopata habari hiyo nilishituka sana. Hata aliyenipa
  habari hiyo aliona sikuwa tena katika hali
ya kawaida.
Ndipo
 
akaniuliza nchini kwenu kuna matatizo gani hata watu
  wakimbie huko? Hakika sikuwa na jibu.
  >
 
 
> Sababu za ukimbizi nchini mwako
 
zinaweza kuwa za Kisiasa, yaani kutokana na utawala mbovu
  watu wanaamua kukimbia kuokoa maisha yao. Au
hali hali
  nyingine yoyote inayohatarisha
maisha. Mimi ninajiuliza
  nchini Tanzania
kuna hali gani ya kuhatarisha maisha ya

watu
  hadi wakimbie wakaishi kwenye
makambi Ugaibuni? Hakika
  nilisikitika
sana. Ila kwa vyovyote wanazo sababu zao za
  kimsingi kukimbia na hata kujiorodhesha kama
wakimbizi.
  >
  >
Wito wangu kwa
  vijana; hakika wengi
wanadhania Ulaya ni sehemu poa. Kuna
 
fedha za kumwaga na maisha huko ni rahisi. Kiukweli ni
  kujidanganya. Hapa Tanzania unaweza kwenda
sokoni ukaokota
  hata matunda au
mbogamboga ukaponea. Ukafanya kibarua
 
chochote kitu hata kufanya usafi kwenye zizi au bustanini
au
  hata kuiba kwa wale
wenye ujuzi huo. Kwa wenzetu hayo
  hayapo.
Hakuna cha kibarua. Hakuna mazingira unayoweza
kuiba
  kirahisi. Kila duka
na soko kuna makamera. Hali ya hewa ni
 
mbaya. Muda mwingi katika mwaka ni baridi kali. nk.
  >
  > Witoa kwa
vijana
  kama unataka kuteseka maisha yako
yote kimbilia Ulaya.
  Walioko kule wako
makambini. Hawaruhusiwi kusafiri,
 
hawaruhusiwi kufanya kazi ila  wanafugwa tu kwa kupatiwa
  chakula na mahitaji mengine ili waishi.
Wanangoja ufanyike
  utaratibu wa
kurejeshwa makwao. Je huko si kupoteza muda

na
  kuhatarisha maisha zaidi.
  >
  > Kinachoniuma
zaidi ni je, hapa Tanzania
  kuna mazingira
gani magumu kiasi hicho hata wajiorodheshe
  kuwa wakimbizi? Kama kuna mwenye maelezo ya
sababu
  ningeshukuru.
 
>
  >
 
Nawasilisha.
  >
 
>
  Kessy
  >
  >
  > --
  > Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
  >
  > Kujiondoa Tuma
Email
  kwenda
  >
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
  >
  > Disclaimer:
  > Everyone posting to this Forum bears
the
  sole responsibility for any legal
consequences of his or
her
  postings, and hence statements and facts
must be presented
  responsibly. Your
continued membership signifies that you
 
agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
  and Guidelines.
  > ---

  > You received this message because
you are
  subscribed to the Google Groups
"Wanabidii"
  group.
  > To unsubscribe from this group
  and stop receiving emails from it, send an
email to
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
  > For more options, visit
  https://groups.google.com/d/optout.
 
  --
 
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
  Kujiondoa Tuma Email
kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
  Disclaimer:
  Everyone posting to
  this
Forum bears the sole responsibility for any legal
  consequences of his or her postings, and
hence statements
  and facts must be
presented responsibly. Your continued
 
membership signifies that you agree to this disclaimer
and
  pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
  ---
  You
received this message
  because you are
subscribed to the Google Groups
 
"Wanabidii" group.
  To
unsubscribe
  from this group and stop
receiving emails from it, send an
  email
to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
  For more options, visit
 
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed to the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails

from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit

https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment