Dada Kiwasila umesema kweli. Vijana hawataki kufanya kazi za kuzalisha. Wanataka kazi za kutoa huduma tu, kama kuuza vocha, juice, sigara na majani ya chai, kucheza kamari na pull! Kimsingi katika haya uzalishaji ni 0.
Nilipotembelea kijijini kwangu, nimekuta kesi moja. Kijana alioa na Mungu akamjalia watoto 3. Kutokana na kulewa pombe na kumpiga mkewe, Mke akaondoka zake. Hakuacha nyuma watoto kwani alijua watateseka maana Bwana hana mpango wa kutunza familia.
Bwana baada ya kuona mke ametoka, akauza shamba lote na kibanda cha nyumba kilichokuepo akabomoa na kuuza bati chakavu kwa bei poa ili kupata hela ya kulewea. Hivyo Bwana huyo wa umri wa kati (47) ametokomea mjini. Hana mawasiliano yoyote na ndugu wala mkewe.
Nadhani huyu atakuwa mkimbii mpaka mwisho wa maisha yake. Atakakofia Mungu anajua.
--------------------------------------------
On Mon, 3/30/15, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, March 30, 2015, 8:19 AM
Foundation For Civil Society imegharimia Youth Empowerment
na kuzipa NGO hela ambazo zilitoa mafunzo, kuwasaidia vijana
miradi ya kuzalisha mali kama ufugaji kuku, mbuzi na ng'ombe
wa maziwa, mbegu za mashamba ya kilimo kama mahindi, mbaazi,
mpunga, vitunguu; ushonaji; ufugaji nguruwe walipotaka;
mizinga ya nyuki. Walipotaka kuanzisha kukopa na kupeana
hela mzunguko-hawajarudisha toka 2008 walipopewa hela laki 1
revolving funds kopa ulipe na faida mwingine akope.
uzalishaji mali, kilimo kimekufa, wapo ktk bajaji na
pikipiki, udalali ktk taxi, mabasi malori kupakia watu
wasichana wamerudi bar vizee ndio vinalima, vinafuga,
vinatumia irrigation pamoja na drip irrigation. Wao (vijana)
kwenda kuiba mazao usiku kupakia ktk mafuso kupeleka mijini
kuuza. Mijini ni hivyo-vikundi ufisadi kugombea madaraka,
kufisadi hela walizopewa kufanya ujasiriamali.
walikoanzishiwa miradi na SACCOS kuna story za kukopa na
kutoroka mpaka familia hulipi deni unaogopa kuporwa
vigodoro. tusaidie vikundi vinavyojiunda vyenyewe sio vya
kuundwa kimradi wana ubadhilifu. Miradi mingi ay vijana
imejaribu kuwafanya wajasiriamali michache imefanikiwa.
Hatupendi kujituma ni tabia na hulka yetu.
Serikali kuahidi ajira wakati ni ujuzi, elimu, skills zako
zikuuze nawe interview inakutupa-italaumiwa bure. Hebu
matajiri wafungue mashamba, wajenge nyumba na kufungua
wiwanda EPZ wawape ajira wenye elimu wasiojiweza. Wasichukue
viwanda kugeuza godowns za mitumba kuuza jumla, store za
spare used za magari etc. Kila kona kila duka mitumba, nguo
toka china, spare za magari; chips na bar. Huku tutoke.
Wenye uwezo wachukue mashamba ya GVT tufanye kweli ili
vijana wakatoe nguvu kazi. Wageni wanakuja wanawekeza kisha
tunawavamia kuchoma moto mali zao. Sisi wenyewe mashamba ya
akina babu tuliyorithi tunayauza, tunalewa hakuna la maana
tufanyalo tunahamia mijini. GVT ikigawa maekari ya mashamba
kwa wanavijiji-tunauza. Hati zipigwe muhuri-hakiuzi, kuuzwa
ni illegal. hii isaidie kuzuia ujinga tufanyao sisi wenyewe
kuuza ardhi zetu.
--------------------------------------------
On Mon, 30/3/15, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!
To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 30 March, 2015, 2:05
Kessy,
Tatizo linalowakimbiza vijana wa nchi za
Kiafrika ikiwemo Tanzania katika nchi za Ulaya ni
unemployment na maisha yasiyo na matumaini tuliyoletewa na
sera za CCM.
em
Sent from my iPhone
> On Mar 29, 2015, at 2:20 PM,
"'Sylvanus Kessy' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
>
> Ndugu
wanabidii
> Hivi karibuni nilikuwa
safarini Nchini Ujerumani. Na moja ya mambo niliyoyakuta
ni
kwamba siku hizi nchini humo kumefunguliwa makambi sehemu
mbali mbali ya wakimbizi. Wengi wao ni kutoka nchi za
Afrika. Nadhani mnasikia mara kwa mara kuhusu wakimbizi
hawa
ambao huenda Ulaya kwa njia ya hatari ya Meli. Wengi hufa
bahari kwa hali mbaya ya hewa au hata kwa kutoswa.
>
> Nchini Ujerumani
nilikuwa katika Jiji la Munich. Nilibahatika kuona moja ya
kambi hiyo, ila kwa bahati mbaya sikuruhusiwa kuingia.
Niliambiwa kadiri ya orodha yao kuna WATANZINIA WAWILI.
Nilipopata habari hiyo nilishituka sana. Hata aliyenipa
habari hiyo aliona sikuwa tena katika hali ya kawaida.
Ndipo
akaniuliza nchini kwenu kuna matatizo gani hata watu
wakimbie huko? Hakika sikuwa na jibu.
>
> Sababu za ukimbizi nchini mwako
zinaweza kuwa za Kisiasa, yaani kutokana na utawala mbovu
watu wanaamua kukimbia kuokoa maisha yao. Au hali hali
nyingine yoyote inayohatarisha maisha. Mimi ninajiuliza
nchini Tanzania kuna hali gani ya kuhatarisha maisha ya
watu
hadi wakimbie wakaishi kwenye makambi Ugaibuni? Hakika
nilisikitika sana. Ila kwa vyovyote wanazo sababu zao za
kimsingi kukimbia na hata kujiorodhesha kama wakimbizi.
>
> Wito wangu kwa
vijana; hakika wengi wanadhania Ulaya ni sehemu poa. Kuna
fedha za kumwaga na maisha huko ni rahisi. Kiukweli ni
kujidanganya. Hapa Tanzania unaweza kwenda sokoni ukaokota
hata matunda au mbogamboga ukaponea. Ukafanya kibarua
chochote kitu hata kufanya usafi kwenye zizi au bustanini
au
hata kuiba kwa wale wenye ujuzi huo. Kwa wenzetu hayo
hayapo. Hakuna cha kibarua. Hakuna mazingira unayoweza
kuiba
kirahisi. Kila duka na soko kuna makamera. Hali ya hewa ni
mbaya. Muda mwingi katika mwaka ni baridi kali. nk.
>
> Witoa kwa vijana
kama unataka kuteseka maisha yako yote kimbilia Ulaya.
Walioko kule wako makambini. Hawaruhusiwi kusafiri,
hawaruhusiwi kufanya kazi ila wanafugwa tu kwa kupatiwa
chakula na mahitaji mengine ili waishi. Wanangoja ufanyike
utaratibu wa kurejeshwa makwao. Je huko si kupoteza muda
na
kuhatarisha maisha zaidi.
>
> Kinachoniuma zaidi ni je, hapa Tanzania
kuna mazingira gani magumu kiasi hicho hata wajiorodheshe
kuwa wakimbizi? Kama kuna mwenye maelezo ya sababu
ningeshukuru.
>
>
Nawasilisha.
>
>
Kessy
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email
kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the
sole responsibility for any legal consequences of his or
her
postings, and hence statements and facts must be presented
responsibly. Your continued membership signifies that you
agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules
and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are
subscribed to the Google Groups "Wanabidii"
group.
> To unsubscribe from this group
and stop receiving emails from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment