Monday, 30 March 2015

RE: [wanabidii] Re:Urais CCM ni Lowassa au Mwigulu:positive Thinkers Tanzania.

Ningepewa nafasi ya kuchagua Raisi wangu angekuwa Augustino Ramadhani.  Lakini ikiwa wakubwa wamechagua basi afadhali Mwigulu kuliko Lowasa.  Mwigulu Sio kijana mbaya sana kwani hana uchafu wa kukithiri na anajiamini na yako makini.  Vile vile hana makundi na hamuonei mtu haya.  Nimekaa nae hoteli moja na kwenye mkutano wa wiki moja uliofanyika Arusha ambao alihudhuria bila kukosa na alikuwa anapanda basi moja na sisi watu wa kawaida.

Yetu macho kwani hapa Tanzania bado tuko kwenye siasa za kuchaguliwa viongozi.

Tafakari

Herment A. Mrema


Date: Sun, 29 Mar 2015 20:25:05 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Re:Urais CCM ni Lowassa au Mwigulu:positive Thinkers Tanzania.
From: tugutunm@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

BREAKING NEWS KUHUSU URAIS 2015, Urais ndani ya CCM ni Mwigulu Nchemba. (siri za vuja.)

Lile fumbo la nani atakuwa mgombea wa Urais kupitia CCM imeteguliwa baada ya SIRI kuvuja kuwa anayeandaliwa ni Mwigulu Nchemba. Taarifa za ndani tulizozipata toka kwa mjumbe mzito kwenye mfumo zinasema kuwa Mwigulu Nchemba ndio chaguo ndani ya CCM nakwamba sasa amekuwa akiitwa kwenye mikutano inayowaweka pamoja Marais wa Afrika na wengine Duniani ili apate kutambulishwa na kupata uzoefu wa mikutano mikubwa. Pia Mwigulu amepelekwa mataifa yote makubwa kwa siri kutambulishwa. Mwaka jana tarehe 25 May 2014 alipelekwa China na kuonana na viongozi wa juu wa CPC chama kinachotawala china akiwepo I PING na Rais wa China Xi Jing Ping.

Tar 10 August 2014 Mwigulu Alipelekwa Uingereza kwa Siri na kutambulishwa kwa chama Labor na kuandaliwa mkutano wa Watanzania. Tar 25 Nov 2014 Mwigulu alipelekwa Marekani majimbo 25 na baadae kuonana na Obama kutambulishwa kwa magavana wa majimbo yenye nguvu.

Alipotoka kule Mwigulu alipelekwa Ufaransa na Ujerumani tar 3 Mwezi wa kwanza kutambulishwa. Ziara za maeneo yote hayo Mwigulu Nchemba alikwenda na Msaidizi wa Rais wa Maswala ya Siasa Ndugu Rajabu Luhwavi. Taarifa zinasema kuwa ndg Luhwavi ndiye mtu anayesifika kwa mipango ya ushindi akiunganisha watumishi wote kumpigia Kikwete 2005. Taarifa za hivi karibuni zimesema Rais Kikwete amekuwa akiambatana na Mwigulu katika matukio mengi yanayowaleta marais wengi pamoja. Mfano tar 18 feb Mwigulu aliambatana na Rais Kikwete kule Rwanda na kutambulishwa kwa Marais wote wa Afrika Mashariki. Pia kabla ya hiyo Rais kikwente alikwenda na Mwigulu Marekani na China kumtambulisha kuwa ni kijanqa mwenye uwezo wa kufanya mabadiliko kwenye uchumi wa nchi.

Hivyo hivyo Mwigulu alikwenda Msumbiji kupata uzoefu wa kuapishwa kwa Rais Nyusi wa Msumbiji. Jana Mwigulu Nchemba alipelekwa Namibia kwa ndege maalumu akiwa na ma Rais wastaafu ndg  Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya Pili na ndg  Benjamin Willium Mkapa wa Awamu ya Tatu.

Jicho la ndani la chombo chetu linasema, Marais hao wastaafu walikabidhiwa jukumubla kumtengeneza Mwigulu kuijua miiko ya nafasi hiyo kubwa. Kila mtu anaamini kuhusu uwezo wa Mwigulu wa kuongoza. Pia hakuna ubishi kuhusubu uthubutu wake. Vile vile hakuna ubishi kuhusu vision yake. Jambo moja tu ni kumtengeneza kuwa na mkao wa nafasi hiyo jambo walilokabidhiwa wazee hao. Inasemekana wamekaa naye mara kadhaa kwa masaa kadhaa na wametoa taarifa kuwa Mwigulu ameiva kwa nafasi hiyo
Taarifa za Uchunguzi wa ndani zaidi zinasema Mwigulu alipelekwa kwa Mwalimu wa Siasa nayehusika na kufunda viongozi kuhusu hotuba na mwenendo wa kiuongozi na kwa kiwango kikubwa amefanikiwa kumbadilisha Mwigulu kwa uongeaji wake, mwenendo na mwonekano wake na kumfanya aonekane kiuongozi wake. Kwa nguvu aloyonayo Mwigulu ndani ya chama na ndani ya Umma ni dhahiri sasa anakwenda kupokea kijiti. Dalili hizi zinasemekana ndizo zilizowafanya wasaka urais wengine wapige kambi kwa Katibu Mkuu Kinana amzuie Mwigulu Nchemba kufanya mikutano. Sent as I received with no source

.....Duh....!  Makubwaaaaa....!

Nzweke Mussa Tugutu (Mr)
Cooler Executive Lake Zone
Nyanza Bottling Co Ltd
P.O.BOX 2086
Mwanza,Tanzania (EA)
Mobile: +255754 89 45 35
               +255784 89 45 35

On Mar 29, 2015 8:06 PM, "'ngupula' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kwa kadri ya tafiti nyingi zinazofuatilia hali ya kisiasa nchini zinaonyesha kama CCM ikitoa rais mwaka huu basi itakuwa ni Lowassa au Mwigulu Nchemba. Hata hivyo, maoni ya wengi yanaonyesha uwezo wa Mwigulu na kasi yake ya kuaminika katika jamii mpk kufikia May 2015 huenda ndiye ataibuka kidedea na kuipeperusha bendera ya chama chake. Kutokuwa na makundi katika chama, kutonunuliwa na matajiri, utendaji wake kazi wa wazi, uadilifu na uzalendo vinampa credit za kutosha Mwigulu Nchemba. Kila heri Mwigulu Nchemba...nikutakie kazi njema endapo utafanikiwa kushika madaraka hayo makubwa nchini. Nikuombe tu....kamwe usikubali kurubuniwa na yeyote linapokuja suala la bandari zetu kwani ni muhimu sana ziboreshwe na zitende kazi kwa ufanisi mkubwa. Suala la gesi ni tumaini kuu kwa tanzania yetu...kamwe usiangalie dini wala kabila la mtu katika mustakhabali mzima wa gesi. Madini yote tunayogundua yachimbwe na wachimbaji wadogowadogo ili kuleta tija kwa watu wetu...vijana wengi hawana ajira. Utalii ni nguzo ya uchumi wa Tanzania.Katika hilo usiweke siasa. Kwa bandari, madini, gesi na utalii azma yako.ya Tanzania kujitegemea inawezekana. Afya na elimu vishike kwa makini sana...Ngupula.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment