Tuesday 31 March 2015

[wanabidii] TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI - 31, MACHI, 2015

                                                                                       31, MACHI, 2015

 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi  ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu. Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala  Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.

Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.

Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu ameenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.

Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frasser Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati Ilala, Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.

Kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi, mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.


Imetolewa na:

Advera Bulimba-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment