Monday 30 March 2015

[wanabidii] Katibu wa Mbunge Selasini na Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Rombo ajiunga na CCM

Ndugu John O. Tarimo aliyekuwa Katibu wa Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Rombo na pia alikuwa ni Katibu wa Mbunge wa jimbo la Rombo Mhe. Joseph Selasini amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Tarimo amefikia uamuzi huo leo baada ya mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana uliofanyika eneo la Tarakea wilayani Rombo jioni hii.

Bwana Tarimo amekihama Chama hicho akitoa sababu mbalimbali ikiwemo ubabaishaji wa Mbunge na kitendo cha kurudisha maendeleo ya jimbo nyuma, Muenezi huyo alisema kuwa tangu kuchaguliwa ubunge, Selasini hajawahi kuhudhuria kikao hata kimoja cha council na kwamba hashiriki kazi zozote za maendeleo ya jimbo hilo kitu kilichofanya miradi ya umeme ichelewe kwa zaidi ya miaka 3, pamoja na kukwama miradi mbalimbali ambayo ilihitaji msukumo wa Mbunge.

Pamoja nae, Vijana zaidi ya 200 wamerudisha kadi za Chadema kwenye nkutano huo wa hadhara uliohutubiwa na Ndugu Kinana.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment