Sunday 29 March 2015

Re: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!

Niliyosimuliwa mimi na mama mmoja ambapo alifukuzwa kazi kampuni ya Benz ofisi ya UK kwa kumwatukana wazungu yalinisikitisha. Pia nilishawahi kurudi ktk ndege moja na kijana aliyekuwa amerudishwa kwa nguvu toka nchi moja ya ulaya nikampa hata nauli ya bus alikuwa hana hapo airport. Huko UK 2009 huyo mama alieleza kudhalilishwa vijana wanaotoroka na kuhamia huko. Ili wapate kazi/ajira huko na kudumu ktk kazi hufanyiwa vitendo vichafu na hao wazungu. Nchi nyingine hunyang'anywa passport na hela hukaa na tajiri kwani hawezi kufungua account hana social security number. Akimkorofisha boss-hutoa siri, anakamatwa, anarudisha bila ya senti hata moja zilizokuwa zinakaa kwa boss. Maisha hayo magumu lakini bora yupo ulaya. Ukipita kona unaongea kiswahili wanaojibanza vijumbani wakikusikia wanakudandia kukusalimia na kutaka kujua unakaa wapi. Ukiwaonyesha hawabanduki kuja kuomba hiki na kile-njaa kali shida tupu. Wadada wanachafuliwa pia wakaka wengine wababa na
familia zao kwao. Bora ufie melini kuliko kulima na kuuza nyanya ngerengere mabonde ya mto Ruvu. Chunga pia hapa nchini kutafutia watoto wako wa kiume na kike wasio na ujasiri na uelewa kazi katika makampuni binafsi ya wageni na wenyeji. Hata kazi za kufagia barabara na kuzoa taka tumekuta simulizi ya ajabu ni chafu kama zilivyotakataka zenyewe. Rushwa ya ngono imepamba moto pamoja na HIV/AIDS kuwa janga la dunia. Ukubali au ukose kazi au utolewe kazini. Mungu anisamehe lakini nimefanya research na kutembea na wazoa taka na wafagiaji DSM mwaka 2003 jioni na usiku mpaka saa 8 nikajionea mengi. Pia utafiti wa sexual abuse umenionyesha mengi na utafiti wa mashoga-ni kioo katika maisha yangu wanapoeleza ilikuwaje, alianzaje, na nani na anapangiwa nyumba na mtu wake ni nani. Dunia imekwisha.
--------------------------------------------
On Sun, 29/3/15, 'Sylvanus Kessy' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, 29 March, 2015, 21:20

Ndugu wanabidii
Hivi karibuni nilikuwa safarini Nchini Ujerumani. Na moja ya
mambo niliyoyakuta ni kwamba siku hizi nchini humo
kumefunguliwa makambi sehemu mbali mbali ya wakimbizi. Wengi
wao ni kutoka nchi za Afrika. Nadhani mnasikia mara kwa mara
kuhusu wakimbizi hawa ambao huenda Ulaya kwa njia ya hatari
ya Meli. Wengi hufa bahari kwa hali mbaya ya hewa au hata
kwa kutoswa.

Nchini Ujerumani nilikuwa katika Jiji la Munich.
Nilibahatika kuona moja ya kambi hiyo, ila kwa bahati mbaya
sikuruhusiwa kuingia. Niliambiwa kadiri ya orodha yao kuna
WATANZINIA WAWILI. Nilipopata habari hiyo nilishituka sana.
Hata aliyenipa habari hiyo aliona sikuwa tena katika hali ya
kawaida. Ndipo akaniuliza nchini kwenu kuna matatizo gani
hata watu wakimbie huko? Hakika sikuwa na jibu.

Sababu za ukimbizi nchini mwako zinaweza kuwa za Kisiasa,
yaani kutokana na utawala mbovu watu wanaamua kukimbia
kuokoa maisha yao. Au hali hali nyingine yoyote
inayohatarisha maisha. Mimi ninajiuliza nchini Tanzania kuna
hali gani ya kuhatarisha maisha ya watu hadi wakimbie
wakaishi kwenye makambi Ugaibuni? Hakika nilisikitika sana.
Ila kwa vyovyote wanazo sababu zao za kimsingi kukimbia na
hata kujiorodhesha kama wakimbizi.

Wito wangu kwa vijana; hakika wengi wanadhania Ulaya ni
sehemu poa. Kuna fedha za kumwaga na maisha huko ni rahisi.
Kiukweli ni kujidanganya. Hapa Tanzania unaweza kwenda
sokoni ukaokota hata matunda au mbogamboga ukaponea.
Ukafanya kibarua chochote kitu hata kufanya usafi kwenye
zizi au bustanini au hata kuiba kwa wale wenye ujuzi huo.
Kwa wenzetu hayo hayapo. Hakuna cha kibarua. Hakuna
mazingira unayoweza kuiba kirahisi. Kila duka na soko kuna
makamera. Hali ya hewa ni mbaya. Muda mwingi katika mwaka ni
baridi kali. nk.

Witoa kwa vijana kama unataka kuteseka maisha yako yote
kimbilia Ulaya. Walioko kule wako makambini. Hawaruhusiwi
kusafiri, hawaruhusiwi kufanya kazi ila  wanafugwa tu
kwa kupatiwa chakula na mahitaji mengine ili waishi.
Wanangoja ufanyike utaratibu wa kurejeshwa makwao. Je huko
si kupoteza muda na kuhatarisha maisha zaidi.

Kinachoniuma zaidi ni je, hapa Tanzania kuna mazingira gani
magumu kiasi hicho hata wajiorodheshe kuwa wakimbizi? Kama
kuna mwenye maelezo ya sababu ningeshukuru.

Nawasilisha.

Kessy


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment