Sunday, 29 March 2015

[wanabidii] Fwd: Magandwa.



Subject: Magandwa.

                                           Magandwa.
                (Dkt. Muhammed Seif Khatib)
   Gwanda ni nguo kukuu iliyoanza kupauka.Mara nyingi gwanda  siyo lazima iwe kukuu bali
huwa  imeshonwa kwa kitambaa kipya. Gwanda haipaswi kuvaliwa kama nguo rasmi katika
 shughuli.Washonao nguo za aina hiyo hutumia aghlabu kitambaa kigumu..Kitambaa hicho  huwa cha kaki na hutakiwa kiweze kuhimili  uchafu, vumbi na mikwaruzo ya mimea na miti  Gwanda ni baba wa uvumilivu.Wavaao gwanda ni watu wanaosafiri kwa miguu au hata kwa
punda,farasi au magari.Ni kawaida kwa vikosi vya polisi na vya wanyama pori nao  kuvaa
magwanda.Hata majeshi ya mataifa mengi sare zao ni magwanda. Yakafanyika hivyo
kulingana na hekaheka, mchakamchaka na sulubu za kazi. Sare za vyama vya siasa
katika nchi zilizopata huru hazivai magwanda.Tuliweza kushuhudia  vyama vya Ukombozi
kadha kuwa na kawaida hiyo.Sababu zipo wazi.Vyama vimo misituni na mitatu ya bunduki
vinasaka uhuru wa nchi zao.Wapiganaji hawana muda wa kuvaa kanzu,suti, masharti au
suruwali zenye urembo.Nguo zao ni magwanda ili ziambatane na muktadha wao wa
kimapambano.
  Hapa kwetu chama kimoja cha siasa viongozi na wanachama wao huvaa magwanda.
Nchi yetu imepata uhuru mwaka 1961.Na kule Zanzibar waliopindua mwaka 1964
dhidi ya Usultani na vibaraka wake.Magwanda kama yalipaswa kuvaliwa ilikuwa
kabla matokeo hayo.Viongozi wakuu Karume na Nyerere walivua magwanda
baada ya kupata Uhuru na Mapinduzi.Vyama vya siasa viliendelea kuwepo lakini bila
wanachama wao kuvaa magwanda. Kazi iliyokuwa mbele yao baada ya kumtimua
mkoloni na sultani ni kujenga taifa jipya.Hakuna mapambano na mkoloni.Hakuna
mapigano misituni.Mavazi ya magwanda wameachiwa wavae polisi, magereza, askari
wanyama pori na jeshi. Hata wao hawapaswi kuvaa muda wote.Hutakiwa wavae katika
muda maalum wa kazi.
  Kiongozi mpiganaji aliyefukuzwa katika chama kimoja cha siasa kivaacho magwanda
hivi juzi alivua magwanda.Alivua baada ya kuvaa kwa miaka ishirini.Kama uvaaji wa
magwanda hayo unaendana na kupata cheo na nishani nadhani yeye asingekosa.Mabega
yake yangejaa vyeo. Kifua chake kingeng'ara nishani za ushujaa na upiganaji katika
medani za vita.Si kawaida kwa askari kuwa katika kikosi cha mapambano kwa miaka
ishirini na kukosa cheo hata cha Sajini au Koplo.Bila ya shaka magwanda hayo aliyovua
rasmi hivi majuzi hatoyavaa tena. Anaweza akayaweka na kuyahufadhi kama kumbukumbu
ama kuyatia moto kwa hasira kuwa aliyavaa kwa miaka ishirini kutetea sera ya chama
chake lakini shukrani aliyepewa na chama chake ni kufukuzwa kwa nazaa na aibu.Ama
anaweza akawapa watu kama mavulia - nguo zilizokwisha valiwa na kuwapa watu wengine
kama mitumba.Haitakuwa kosa akiamua kuzilimia michikichi au kuvulia migebuka.Lakini
tumeona wale waliochoshwa na magwanda hayo kuyavaa kwa muda mrefu siyo yeye
pekee.Wengi wamejitokeza kufata nyayo zake.Katika miezi michache ijayo hasa baada
ya muda wa uhai wa Bunge na Udiwani kumalizika, idadi ya wavao magwanda wataamua
kuyavua hadharani na kuonesha kuchoka kuyavaa.Wote hawa watafata nyao za
mtangulizi wao aliyefukuzwa chama.Kiongozi huyu aliyefukuzwa katika chama alichokitamalia kwa thuluthi moja ya uhai wake anatupa mafunzo mawili.Moja, kwa
kuvua magwanda ya chama chake na kujiunga na chama kipya,kichanga kinaashiria
kuwa vyama vya upinzani vile vidogo na vikubwa, vile vikongwe na vipya vyote havyo
havina sera nzuri na viongozi wao si lolote si chochote.Haviamini,havitaki na havina
ubavu wa kupambana na Chama cha Mapinduzi.Vyama vyote vya upinzani vipo kwa
masilahi ya viongozi hao binafsi.Yeye hajaungana nao kwa sababu alikuwa nao huko
kwa miaka ishirini anawajua sana sana tokea utandu hadi ukoko.Chama chake kipya
ndicho chama safi,chenye sera sahihi na uongozi uliotukuka!Pili, ameungama kuwa
yeye na chama chake ni wafuasi wa sera na misingi ya siasa za Mwalimu Nyerere!Bila
ya shaka kiongozi huyu katika mikutano yake ya siasa ataanza kwa kaulimbiyo.
'Zidumu Fikra za Mwalimu Nyerere'.



Sent from my iPad

0 comments:

Post a Comment