Sunday 29 March 2015

[wanabidii] Watanzania - Wakimbizi Ulaya!

Ndugu wanabidii
Hivi karibuni nilikuwa safarini Nchini Ujerumani. Na moja ya mambo niliyoyakuta ni kwamba siku hizi nchini humo kumefunguliwa makambi sehemu mbali mbali ya wakimbizi. Wengi wao ni kutoka nchi za Afrika. Nadhani mnasikia mara kwa mara kuhusu wakimbizi hawa ambao huenda Ulaya kwa njia ya hatari ya Meli. Wengi hufa bahari kwa hali mbaya ya hewa au hata kwa kutoswa.

Nchini Ujerumani nilikuwa katika Jiji la Munich. Nilibahatika kuona moja ya kambi hiyo, ila kwa bahati mbaya sikuruhusiwa kuingia. Niliambiwa kadiri ya orodha yao kuna WATANZINIA WAWILI. Nilipopata habari hiyo nilishituka sana. Hata aliyenipa habari hiyo aliona sikuwa tena katika hali ya kawaida. Ndipo akaniuliza nchini kwenu kuna matatizo gani hata watu wakimbie huko? Hakika sikuwa na jibu.

Sababu za ukimbizi nchini mwako zinaweza kuwa za Kisiasa, yaani kutokana na utawala mbovu watu wanaamua kukimbia kuokoa maisha yao. Au hali hali nyingine yoyote inayohatarisha maisha. Mimi ninajiuliza nchini Tanzania kuna hali gani ya kuhatarisha maisha ya watu hadi wakimbie wakaishi kwenye makambi Ugaibuni? Hakika nilisikitika sana. Ila kwa vyovyote wanazo sababu zao za kimsingi kukimbia na hata kujiorodhesha kama wakimbizi.

Wito wangu kwa vijana; hakika wengi wanadhania Ulaya ni sehemu poa. Kuna fedha za kumwaga na maisha huko ni rahisi. Kiukweli ni kujidanganya. Hapa Tanzania unaweza kwenda sokoni ukaokota hata matunda au mbogamboga ukaponea. Ukafanya kibarua chochote kitu hata kufanya usafi kwenye zizi au bustanini au hata kuiba kwa wale wenye ujuzi huo. Kwa wenzetu hayo hayapo. Hakuna cha kibarua. Hakuna mazingira unayoweza kuiba kirahisi. Kila duka na soko kuna makamera. Hali ya hewa ni mbaya. Muda mwingi katika mwaka ni baridi kali. nk.

Witoa kwa vijana kama unataka kuteseka maisha yako yote kimbilia Ulaya. Walioko kule wako makambini. Hawaruhusiwi kusafiri, hawaruhusiwi kufanya kazi ila wanafugwa tu kwa kupatiwa chakula na mahitaji mengine ili waishi. Wanangoja ufanyike utaratibu wa kurejeshwa makwao. Je huko si kupoteza muda na kuhatarisha maisha zaidi.

Kinachoniuma zaidi ni je, hapa Tanzania kuna mazingira gani magumu kiasi hicho hata wajiorodheshe kuwa wakimbizi? Kama kuna mwenye maelezo ya sababu ningeshukuru.

Nawasilisha.

Kessy


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment