Wednesday, 25 March 2015

Re: [wanabidii] TAMKO LA JUMUIYA ZA KIISLAMU KUHUSU HATIMA YA MAHAKAMA YA KADHI – MARCH 2015

UPUUZI TENA WA HERUFI KUBWA

2015-03-24 16:36 GMT+03:00 Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com>:
MADNESS

2015-03-24 16:10 GMT+03:00 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU 11 KUHUSU HATIMA YA MAHAKAMA YA KADHI NA HALI YA AMANI YA TANZANIA – MARCH 2015

Hivi karibuni baada ya Serikali kuandaa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali, hususan sehemu ya muswada unaohusu Mahakama ya Kadhi kumekuwa na matamko toka kwa Maaskofu na Wachungaji kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania linaloundwa na taasisi za BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA (TEC), JUMUIYA YA KRISTO TANZANIA (CCT), BARAZA LA MAKANISA YA PENTEKOSTE TANZANIA (CPCT) zikiitaka Serikali na Bunge kuacha mara moja kuendelea na utaratibu wa kuwasilisha, kujadili na kupitisha sheria ya utambuzi wa Mahakama ya Kadhi Tanzania kwa hoja kuwa hilo ni jambo la kidini liachwe kwa wanadini husika. Imedaiwa na Maaskofu na Wachungaji hao kuwa muswada wa Mahakama ya Kadhi unakiuka katiba na ni rushwa iliyotolewa na Serikali kwa Waislamu ili kupata ridhaa ya Waislamu kuipitisha Katiba Pendekezwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

Sisi Waislamu chini ya mwavuli wa Jumuiya na Taasisi Kuu za Kiislamu Tanzania zipatazo 11 (ambazo ni Hay Atul-Ulamaa, Shura ya Maimamu, DUMT, BASUTA, AN-NAHL TRUST, BARAZA KUU, Jumuiya na Taasisi, JASUTA, TAMPRO, IPC, AL-MALID) kwa azimio la kikao cha dharura cha tarehe 21/03/2015 tunapenda kutamka yafuatayo:-

1. Kama inavyojulikana Tanzania ni nchi yenye kuongozwa kwa sheria za aina nne (sheria za Kiislamu, sheria za Kimila, sheria zilizorithiwa toka kwa waingereza (yaani common law) na sheria za kutungwa na Bunge). Hivyo basi Sheria za Kiislamu ni sehemu ya sheria halali za nchi hii. Sheria hizo za Kiislamu zimekuwa zikitumiwa na mahakama kabla ya uhuru na baada ya uhuru. Kwa kipindi chote hicho zaidi ya miaka 100 Maaskofu na Wachungaji hawakuwahi kupinga matumizi ya sheria hizo za Kiislamu katika mahakama za Serikali ilihali wamekuwa wakijua fika kuwa sheria hizo ni za kidini. Tunasikitishwa na hali hiyo kubadilika sasa. Hakuna mantiki yoyote kwa maaskofu na wachungaji kuipinga Mahakama ya Kadhi ambayo itaendelea kutumia sheria hizo za Kiislamu zinazotumiwa na Mahakama za kawaida.

2. Maaskofu na Wachungaji kulitaka Bunge kuacha kujadili muswada wa Mahakama ya Kadhi ni kuingilia uhuru na utawala wa Bunge jambo ambalo serikali na Bunge linapaswa kukemea bila ya kuwa na kigugumizi.

3. Serikali iwachukulie hatua za kisheria Maaskofu na Wachungaji kwa kutoa matamko yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia za kidini kwa Waislamu kinyume cha sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, ikiwemo kuwakamata, kuwafikisha mahakamani na kuzuia dhamana kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali.[AK1] 

4. Kwa kudai kuwa serikali imetoa rushwa kwa Waislamu kama kundi maalum kwa kukubali sheria itakayounda Mahakama ya Kadhi ili kuipitisha Katiba Pendekezwa ni kuidhalilisha dini ya Mwenyezi Mungu, kuwadhalilisha Waislamu na ni kuumiza hisia za Waislamu na kuhatarisha amani na utangamano.

5. Serikali isipofanya kama tulivyoeleza hapo juu utakuwa ni ushahidi MWINGINE kwetu Waislamu kuwa hakuna usawa mbele ya serikali kwamba iko tofauti katika kushughulikia kauli za masheikh na kauli za maaskofu na wachungaji Wakristo. Vile vile hatutokuwa na cha kuzuia imani za Waislamu kuwa maaskofu na wachungaji walitoa tamko lao kwa kushauriana na serikali na wengine kwenda mahakamani kuizima Mahakama ya Kadhi kama mpango maalum.

6. Serikali iendelee na mchakato wa uundwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge kwa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo:-

i. Serikali iache njama au hila za kuigeuza Mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA.

ii. Serikali iache njama za kutaka kutumia kisingizio cha uundaji wa Mahakama ya Kadhi kuihalalisha kupitia sheria ya Mahakama ya Kadhi BAKWATA kuwa chombo rasmi kwa mujibu wa sheria chenye kuwakilisha na kusimamia mambo yote ya Waislamu. Hii ni kwa sababu (a) BAKWATA imekosa uhalali (legitimacy) kwa ummah wa Waislamu (b) BAKWATA haiaminiki tena kwa Waislamu wa ndani na nje ya Tanzania (c) BAKWATA ni baraza lililosajiliwa kama taasisi ya kijamii, hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni marufuku kuwalazimisha watu kujiunga au kuwa wanachama wa jumuiya au taasisi bila ya ridhaa (d) Serikali itajiingiza katika mgogoro wa kikatiba na Waislamu kwa kuvunja Katiba ili kutimiza mapenzi yake kwa BAKWATA.

iii. Serikali iwache kufanya vikao na BAKWATA peke yake kwa upande mmoja na maaskofu kwa upande mwingine katika mchakato wa kuandaa muswada wa Mahakama ya Kadhi na itupilie mbali maafikiano yeyote yaliyofikiwa tokana na vikao hivyo, na badala yake izingatie maoni yaliyokwishatolewa mbele ya Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge.

iv. Endapo serikali itaendelea na kuwasilisha muswada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa mamlaka BAKWATA kuunda, kusimamia, kuteua makadhi nakadhalika kinyume cha maoni ya Waislamu walio wengi itakuwa imethibitika kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli kuunda na kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

v. Tunataka Mahakama ya Kadhi iliyo huru, inayoanzishwa na sheria na siyo kuanzishwa na taasisi au chombo binafsi. Mahakama hiyo iwe chini ya tume maalum itakayowajibika kwa mujibu wa sheria kuteua makadhi, kutengeneza kanuni za uendeshaji mashauri, kudhibiti maadili na nidhamu ya makadhi, nakadhalika

vi. Iwe na muundo kuanzia ngazi ya tarafa, wilaya, mkoa na taifa ambayo zaidi itashughulikia rufaa.

vii. Igharamiwe na serikali kama ambavyo serikali hivi sasa inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za Kiislamu ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa. Na pia igharimiwe na serikali kama ambavyo serikali hii hii inavyogharamia huduma za makanisa chini ya mkataba maarufu Memorandum of Understanding (MOU) mkataba ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya Waislamu (miongoni mwa wadau wakuu) ambao umeendelea kunufaisha wakristo fedha za walipa kodi.

viii. Hoja ambayo inaweza kuzushwa kuwa Waislamu wenyewe wanakhitilafiana kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi ni sababu tosha ya kuuodoa Muswaada huu, haina mashiko kwa sababu tulizozitaja hapo juu.

7. Iwapo serikali haitopeleka muswada bungeni unaokidhi matakwa ya Waislamu wengi kama ilivyopendekezwa kwenye Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge, Waislamu wataendelea na msimamo wao wa kususia kushiriki kwenye mchakato wa kuipigia kura katiba pendekezwa.

Imetolewa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania leo tarehe 23.03.2015

NAIBU KATIBU MKUU
SHEIKH RAJAB KATIMBA

Tunawashukuru sana na ahsanteni.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment