Saturday, 1 March 2014

[wanabidii] Ni mara ngapi tunakosa Baraka za MUNGU kwa sababu zinakuja tofauti na sisi tulivyotaka?

Binti mmoja ambaye aliolewa na kijana mmoja wa makamo na ambaye alikuwa na utajiri mwingi sana, alikuwa anategemea kupata zawadi kutoka kwa mmewe kwani alikuwa anakaribia kuadhimisha siku yake ya kusherehekea miaka yake ya kuzaliwa.

Kwa muda mrefu alikuwa akitamani pete moja ya almasi iliyokuwa katika showroom moja ya duka moja maarufu sana la kuuzia vitu vya thamani .Binti aliamini mmewe angeweza kuinunua kwani kwa utajiri wake ilikuwa ni fedha kidogo sana. Yeye aliitamani zawadi hiyo ya pete tu na sio nyingine kutoka kwa mmewe kipenzi.

Siku ya birthday ikawa inakaribia na yule binti akawa anasubiri kila dalili za kuipata ile zawadi, na hatimaye siku ikafika. Asubuhi ile yule mme akamwita mkewe chumbani mwao na akamwambia jinsi alivyokuwa na bahati kwa kuwa na mke mzuri na mwema kama yule na jinsi alivyokuwa akimpenda kwa dhati.

Baada ya maneno yale mme akachukua box dogo lililopambwa vizuri na kumpa mkewe .Mkewe akiwa na hamu ya kujua nini kipo mle ndani akaifungua bila kuchelewa na kukuta BIBLIA iliyofungwa vizuri ya yenye kava zuri la ngozi nje yake na lenye jina lake lilioandikwa kwa dhahabu.

Yule mke kwa hasira akapiga kelele na kumwambia, "yaani pamoja na hela zote ulizonazo, uliona BIBLIA hii ndio zawadi ya kunipa mimi katika siku muhimu kama hii???" kisha kwa hasira akachukua vilivyo vake na kuamua kuondoka pale nyumbani na kwenda kuanza Maisha ake akiwa na mwane.

Miaka mingi ikapita na yule mke akawa kajiimarisha ana nyumba yake nzuri na biashara zake na akiishi na mme mpya na familia yake wakati yule mme wake wa zamani alikuwa keshazeeka sana. Siku moja Yule mke akaamua apange kwenda kumtembelea mme wake wa zamani kwani hawajawasiliana nae kwa kipindi kirefu sana tangu aondoke.

Hata kabla ya siku ya kwenda akapokea ujumbe kuwa mme wake wa zamani amekufa kwa ajali mbaya ya gari na kwa kuwa walikuwa wameoana na wana mtoto mmoja mme aliandika urithi wote uende kwa yeye na mtoto wao. Hivyo mama akaamua awahi kwenda ili akachukue mali hizo.

Alipowasili katika nyumba yao ya zamani, ghafla huzuni na machozi yakaanza kumdondoka akakumbuka Maisha yao na kuamua kuzunguka vyumbani kuangalia vitu muhimu na kuiona ile BIBLIA bado mpya kama alivyoiacha miaka mingi iliyopita.

Huku machozi yakizidi kumtoka akaanza kuifungua ile BIBLIA kila ukurasa na kuona mmewe aliupigia mstari huu Matt 7:11, Ambao ulisomeka "Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?"

Akiwa anaendelea kusoma kabahasha kadogo kakaanguka na alivyofungua alilia kwa sauti kuona ni Pete ya almasi kama ile aliyoipenda ikiwa imeandikwa jina lake na maneno kwenye bahasha NAKUPENDA MKE WNGU KIPENZI.

Ni mara ngapi tunakosa Baraka za MUNGU kwa sababu zinakuja tofauti na sisi tulivyotaka?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment