Elisa, umesema kweli tupu, tujiandae kuandika katiba upya baada ya 2015, hili genge la sasa hamna kitu, wiki sasa wala hawajui wanataka kufanya nini! Tunahitaji tanganyika yenye majimbo kumi, mawaziri wasiozidi nane.
----------
Sent from my Nokia phone
------Original message------
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, March 1, 2014 12:22:18 PM GMT-0800
Subject: Re: [wanabidii] Neno Fupi La Usiku: Afrika Safari Nyingine Huanza Na Njia Ya Panda..
Sijachelewa sana kutoa maoni yangu. Nikijielekeza kwa wazo la Mjengwa kuwa kwanini tume ya Katiba haikuandaa mpano 'B' nafikir kuwa Tume haikutegemea kuwa Tanzania ingekabiliana na upuuzi huu unaoendelea Bungeni. Lakini hata kama kubekuwa na Plan 'B' ni bunge gani lingeweza kuyachukua yale mambo na kuyaweka katika katiba ya sasa? Hawa wanaobishania Posho, siha na namna ya kupiga kura?
Mimi nafikiri bunge hili litaibuka na jambo moja kwa watanzania. Kujiandaa kuweka serikali madarakani itakayoliongoza Taifa kuandika Katiba mpya. Na hii itakuwa agenda ya uchaguzi 2015
On Friday, February 28, 2014 11:53 PM, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Ndugu zangu,
Jioni hii kupitia runinga nilimsikia Profesa Costa Mahalu, Mwenyekiti
wa Tume ndogo ya Bunge Maalum kwa kazi ya kuandaa rasimu ya kanuni
akitamka, kuwa swali la ama kura ya faragha (siri) au ya dhahiri ( wazi) wataachiwa Wabunge wenyewe waamue.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Mheshimiwa Kificho naye hakuficha
kuonyesha kwa sura na hata kauli, juu ya ugumu wa jambo hilo. Akatolea
mfano wa mpira, kwamba sasa uko kwa Wabunge.
Kwa kuziangalia
baadhi ya sura za Wabunge wale, hakika ni vigumu kuwaonea wivu kwamba
wamo ndani ya jengo lile. Wana wakati mgumu, maana, umma nao
unawaangalia.
Naam, nimepata kuandika, kuwa Afrika safari zetu
nyingi ni za bure tu. Na nyongeza hapa, ni kuwa , safari zetu nyingine
Afrika huanza na njia panda. Kwamba unapoianza tu safari unakutana na
njia panda.
Na ni kwenye njia panda ndipo mwanadamu unatakiwa
utumie hekima na busara. Njia panda inakutaka ufikiri kwa makini. Maana,
ukichagua njia kwa makosa, basi, safari yako itakuwa ni ya mwelekeo
mwingine. Si kule ulikotaka kwenda. Na kazi ya kuirudia njia sahihi huwa
ni ngumu sana.
Jioni hii pia nimesoma tena baadhi ya vifungu
vya Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza
nimeipitia rasimu hii kwa masikitiko, maana, mbali ya kwamba ina mambo
mengi sana mazuri kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake, kwa kizazi
hiki na vijavyo, nahofia, kuwa kinachoendelea Dodoma, ambapo, ni
dhahiri, kuwa zinaonekana dalili za mijadala kutawaliwa na ushabiki wa
vyama kuliko wa nchi na mustakabali wake. Ni dalili za kuwa njia panda
na pengine tumeshaanza kuifuata njia isiyo sahihi. Kwamba tunapotea kama
Taifa.
Na ninaposoma rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Warioba
na kupitia vifungu kama kile cha Sura ya Tisa, kinachohusu Bunge la
Muungano, sehemu ya Kwanza, Ibara ya 113 kifungu cha 3 kinachosema;
" Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za Ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme."
Kabla ya hapo wanawake wengi waliingia Bungeni kwa njia ya Viti Maalum.
Kwa rasimu hii ya Katiba, wanawake watapata nafasi ya kushindana
wenyewe kwenye majukwaa ya uchaguzi. Ni maendeleo ya kidemokrasia.
Najiuliza, hivi ni kwa nini Tume ya Jaji Warioba hawakuandaa Plan B
kwa maana ya mpango 'B' . Na plan B hapa ingelikuwa ni kuandaa
mazingira, kuwa endapo rasimu hii ya Katiba itakwama, basi, yale yote
mazuri yaliyomo kwenye rasimu na yanayokubaliwa na pande zote, na yenye
kuweza kuhamishiwa kwenye Katiba ya sasa bila kusababisha matatizo,
basi, yangefanyiwa utaratibu wa kuingizwa, kwa maana ya kuifanyia
marekebisho ya ' dharura' Katiba iliyopo. Najaribu kufikiri tu, kwa
uhuru.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.
0754 678 252
http://mjengwablog.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:
Post a Comment