Saturday 1 March 2014

Re: [wanabidii] HAKI ZA BINADAMU KWA JAMII NDOGO KAMA MASHOGA

Nafikiri ili mjadala unoge ni lazima yeyote anayeleta hoja yoyote aende zaidi ya kuanza kutetea. Ni vema kwanza tutafsiri maana ya neno haki za binadamu. Hakuna hakina za kibinadamu ambazo ulimwengu wote huamini hata kama UN imesema maana UN nayo ni jamii fulani na wala siyo ulimwengu mzima na siyo nchi zote ni wanachama wa UN. Kwa hiyo lazima tujadili haki za binadamu kwa mtazamo fulani. Kuna mitazamo mingi na yote ni sahihi kabisa. Mfano kila mtu anapenda asidokolewe na kibaka na kibaka naye anayo haki ya kuishi na siyo kupigwa hadi afe. Mwenye mali anapenda kulindwa na vibaka na ila kibaka anastahili kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria na siyo na mob hadi kufa. Hapo tunazungumzia haki za aina mbili.
 
Sasa haki za mashoga ni lazima kwanza tukubaliane neno shoga kwa lugha ya Tanzania. Kwa ufupi hakuna hata neno shoga kwenye katiba maana ni utamaduni mgeni wa Magharibi. Kwetu sisi Wtz na Waafrika ukiacha A. Kusini wengine wote hawana huo utamaduni mchafu. Kwa hiyo ni sawa kabisa ushoga katika nchi za Magharibi na Marekani maana wenyewe wanajali mtu mmoja kuliko jamii kama ilivyo kwetu. Inanikumbusha mgongano kati ya utamaduni wa Magharibi na Afrika katika fasihi. Ni kawaida kwa ulaya watu kujali mtu mmoja badala ya jamii. Huko mmwanaume anaweza kuwa na artificial vagina na mke wake na mwanamke anaweza kuwa na artificial penis na kuwa mume wake au kumtafuta mwanamke mwingine amwingilie kama mwanaume. Kwao ni sawa. Kwao ni sawa kutokiwa na watoto ila sisi watoto bado ni muhimu. Kwa wenzetu ukiwa mzee utatunzwa na serikali hadi ufe ili kwetu watoto ndio wa kukutunza hivyo umuhimu wa kuzaana na familia au kuwa jamii.
 
Kwa msingi huo, Wazungu hawana haki ya kutufundisha namna ya kuishi bali sisi tunajua namna ya kuishi kama apendavyo Mungu. Sisi kwetu tunahitaji jamii maana jamii bado na msingi wa jamii ya Kiafrika na kwingine ukiacha Magharibi. Wanaotaka kama Wazungu ni vema wakaenda kwa na siyo kuishi kama Wazungu hapa kwetu Afrika. Ila wakitaka kuishi hapa lazima waishi kama wengine. Ukienda kwa Waroma uishi kama Mroma. Ili ukija kwetu Arusha lazima uishi kama Maasai vinginevyo jamii inaweza kukupoteza kama kibaka! Kwa hiyo haki za binadamu kwa mashoga Magharibi ila kwetu hamna kwa sasa ijapokuwa wanaolawitiana wapo na wanawake wanaotumia uume wa mpira wako ila wasifanye public show maana haikubaliki na kama kibaka akikamatwa mbele kwa mbele!

On Friday, 28 February 2014, 20:35, nyaronyo kicheere <kicheere@yahoo.com> wrote:
haya ni maneno ya magweiga ninayemfahamu au mtu fulani anajifanya magweiga?
ningependa kumwona magweiga akihubiri ujumbe huu wa haki ya mashoga tarime mjini au bunda mjini au mugumu mjini au nyamongo mjini au kule kiagata na si jijini dsm kwenye mtandao!
kicheere, tungi, kigamboni tanganyika territory

On Friday, February 28, 2014 11:40 AM, leonard magwayega <bobittz@yahoo.com> wrote:
we unayetetea haki za mashoga kaungane nao wewe mfanye ushoga, usituletee mambo ya kipuuzi katika katiba mpya.
Bob Leo.

On Tuesday, February 25, 2014 4:08 PM, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
HAKI ZA BINADAMU KWA JAMII NDOGO KAMA MASHOGA

Ndugu zangu ,

Nimeona nisikae kimya , nisiwe mnafiki na nisimamie kile ninachosimamia siku zote , suala la haki za binadamu kwa raia wote bila kujali mapungufu au matatizo yoyote aliyokuwa nayo .

Kabla sijaanza kuandika ujumbe huu nimesikitishwa na kiongozi mmoja akiandika kwenye ukurasa wa kijamii kufurahia kitendo cha Rais wa Uganda Kusaini GAY BILL kwa kufuata mkumbo tu bila kujua hawa ni miongoni mwa wapiga kura wake .

Tukirudi kwenye suala la jamii za watu wenye jinsia moja yaani mashoga kwa upande wa wanaume na wasagaji kwa wanawake , kuna mambo kadhaa inabidi jamii ijue nitaweza wazi kwa ufupi .

Katika katiba mpya haki zao zitakuwa kwenye kipengele cha jamii ndogo ndogo .

1 – Ndani ya jamii hizi kumekuwa na magonjwa mbalimbali , kutokana na hawa watu kutokujulikana waziwazi wamekuwa wanajificha ndani hata mahospitali hawaendi hata watoa huduma hawawafikii matokeo yake ni kuathirika zaidi na kupoteza watu wengi zaidi .

2 – kuna wale washauri nasaha na wengine watoaji wa huduma za afya haswa zinazohusiana na ugonjwa wa ukimwi , wamekuwa wanapata tabu kumaliza gonjwa hili na mengine yanayohusiana na hili kutokana na kutokuwa wazi .

3 – Kuna ushahidi wa wazi wa vitendo vya mahusiano ya jinsia moja haswa katika nyumba za ibada au kwenye huduma za ibada na taasisi za kidini haswa kwa watu wazima na watoto wadogo wanaopelekwa kujifunza na matokeo yake ni kuificha jamii hii ambayo imelelewa na kufichwa kwenye nyumba za ibada .

4 – Kwenye katiba mpya inayokuja kinachopiganiwa ni haki ya jamii ndogo ndogo kama hizi za Mashoga , wasagaji , Hadzabe na nyingine nyingi zilizopo nchini ambazo rais ameapa kuzilinda na kuzitetea bila ubaguzi wowote .

5 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe Jakaya Mrisho Kikwete alichaguliwa na watu mbalimbali na aliapa kulinda watu wote na kuongoza nchi hii wakiwemo hawa ambao sasa hivi wanatengwa na kuonekana si mali kitu na si chochote  .

Kwa kumalizia napenda kusema na kusisitiza tena , Kwamba hii ni  nchi yetu wote , basi haki za wote ziheshimiwe bila kuingilia mambo ya faragha ya watu wengine , sasa tuko kwenye mchakato wa katiba mpya hili suala liangaliwe na tunakaribia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 natumai viongozi wetu watatumia hekima katika kuangalia na kusimamia haki za jamii ndogo ndogo .

--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment