Mrema Umesema vizuri. Mimi nafikiri siyo sahihi kusema kuwa CCM haina ridhaa ya wananchi. Huenda niulize ni kipimo gani mnatumia kusema hivyo? Mimi naamini CCM wana ridhaa ya wananchi kwa kipimo cha hivi karibuni tu cha Uchaguzi wa madiwani. Kwa mantiki hiyo wanayoridhaa ya watanzania kiongoza na kiwasemea wananchi wao ambao wanataka kuporwa haki zao kuongia mikononi mwa wachache kwa kuwapaka mafuta kuwa wanawakomboa kumbe wanataka kuwabomoa, hiyo no moja. Pili kama umenisoma vizuri mwanzo nimesema kila mtu au kikundi kina haki ya kutoa mawaxo yake. Sasa hapa kosa li wapi? Kila mtu anatetea hoja yake ili ashinde. Hii ndiyo demokrasia Mrema. Maamuzi yatakayokubaliwa na wengi ndiyoo yatakayoheshimiwa. Hakuna mtu anayeweza kulala hadi pale maamuzi yatakapofanyika. Tatizo litakuja pale maamuzi yakitolewa halafu wewe unaendelea kuvuruga, tutasema wewe una lako jambo. Hoja hii inaweka msisitizo wa kuacha unafiki wa kuvaa ngozi ya kondoo wakati wewe ni mbwa mwitu. Kama wewe unataka kura ya siri unalako jambo. CCM hailazimishi mtu kukubaliana na msimamo wake kama kikundi au chama. Hata hivyo wapo wabunge ambao wameonesha kutokukubaliana na msimamo huo, hapa tatizo liko wapi? Tatizo sisi unafiki ndio asili ya watanzania, tuache. Utakuta mtu anakwenda kukopa benki mchanganuo kaandika vizuri kwamba atajenga nyumba au ataendesha biashara yake vizuri na itatoa faida, akipata mkopo tu mara ananunua vitu ambavyo havikuwemo kwenye andiko la kukopea. Matokeo yake atazalisha sababu nyingi kwa nini anashindwa kurejesha mkopo lakini yote ni kutokuwa wawazi na unafiki tu. Kuna hoja pia inatolewa kwamba wakijulikana kuwa hawakubaliana na upande wa chama chao eti watawadhuru. Kwangu hizi ni propaganda mfu. Ukweli ji kwamba kila kikundi au jamii inapenda kuwa na mwelekeo wa jambo moja katika hoja za msingi. Mfano mzuri juzijuzi CDM ilitofautiana na makada wake ikawaondoa sasa hata hao wa CCM wanaodhani kuw wanatofsutiana na chama chao waondoke tu wasiendelee kujificha nyuma ya wenzao. Huu ndio ninaouita unafiki mimi. Mwisho CCM ndio wanaridhaa ya watu mru asikudanganye. Kama huamini subiri uone Jimbo la Kalenga, utashangaa na kubakia mdomo wazi. Watu walionunuliwa hass vyombo vya habari nawashauri wasituharibie nchi. Bado tunahutaji nchi yetu iwe moja na tuendelee kuishi kwa amani hata kama tuna tofauti ya mitizamo kama ilivyo kwa sasa. |
From: Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: RE: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR
Sent: Sun, Mar 2, 2014 11:22:22 AM
Kura ya siri imekuwa ni lazima kwa sababu ya CCM. CCM kama chama tawala hakikutakiwa kuwa na msimamo kichama kwenye swala hili la katiba kwani wataonekana na wanaonekana kuvutia upande wao ili waendelee kutawala hata pale hawana ridhaa ya wananchi. Hivyo ili kuinusuru nchi na kuhakikisha vyama kama vyama havipewi nafasi ya kuendeleza agenda zao kwa nguvu zote kama wanavyofanya CCM inabidi warudi nyuma waachie wanachama na nafsi zao waamue ni lipi lililo jema. Kuwa na cocas za kichama ni dalili za kuigawa nchi. Hii inajenga taswira ya kukiona chama cha CCM kama chama gandamizi ambacho kipo tu pale kwa maslahi ya watawala na wala sio maslahi ya wananchi. Wasitake kulazimisha mambo kwani mwisho wake itakuwa mbaya kwani binadamu naye atafika mahali atachoka na akichoka amani itapotea. Hatutaki hilo litokee. Kama CCM inaamini ina sera nzuri basi wawaache wanachama wao wafanye wanayotaka kufanya kwa hiari yao na sio kuburuzwa. TUNAOMBA TUDUMISHE AMANI Herment Date: Sun, 2 Mar 2014 11:10:45 +0000 From: ekunyaranyara@yahoo.co.uk Subject: Re: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR To: wanabidii@googlegroups.com
From: Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>; To: <wanabidii@googlegroups.com>; Subject: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR Sent: Sun, Mar 2, 2014 9:20:38 AM
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment