Sunday, 2 March 2014

Re: RE: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR

Mrema

Umesema vizuri. Mimi nafikiri siyo sahihi kusema kuwa CCM haina ridhaa ya wananchi. Huenda niulize ni kipimo gani mnatumia kusema hivyo?

Mimi naamini CCM wana ridhaa ya wananchi kwa kipimo cha hivi karibuni tu cha Uchaguzi wa madiwani.

Kwa mantiki hiyo wanayoridhaa ya watanzania kiongoza na kiwasemea wananchi wao ambao wanataka kuporwa haki zao kuongia mikononi mwa wachache kwa kuwapaka mafuta kuwa wanawakomboa kumbe wanataka kuwabomoa, hiyo no moja.

Pili kama umenisoma vizuri mwanzo nimesema kila mtu au kikundi kina haki ya kutoa mawaxo yake. Sasa hapa kosa li wapi? Kila mtu anatetea hoja yake ili ashinde. Hii ndiyo demokrasia Mrema. Maamuzi yatakayokubaliwa na wengi ndiyoo yatakayoheshimiwa. Hakuna mtu anayeweza kulala hadi pale maamuzi yatakapofanyika. Tatizo litakuja pale maamuzi yakitolewa halafu wewe unaendelea kuvuruga, tutasema wewe una lako jambo.

Hoja hii inaweka msisitizo wa kuacha unafiki wa kuvaa ngozi ya kondoo wakati wewe ni mbwa mwitu. Kama wewe unataka kura ya siri unalako jambo.

CCM hailazimishi mtu kukubaliana na msimamo wake kama kikundi au chama. Hata hivyo wapo wabunge ambao wameonesha kutokukubaliana na msimamo huo, hapa tatizo liko wapi?

Tatizo sisi unafiki ndio asili ya watanzania, tuache. Utakuta mtu anakwenda kukopa benki mchanganuo kaandika vizuri kwamba atajenga nyumba au ataendesha biashara yake vizuri na itatoa faida, akipata mkopo tu mara ananunua vitu ambavyo havikuwemo kwenye andiko la kukopea. Matokeo yake atazalisha sababu nyingi kwa nini anashindwa kurejesha mkopo lakini yote ni kutokuwa wawazi na unafiki tu.

Kuna hoja pia inatolewa kwamba wakijulikana kuwa hawakubaliana na upande wa chama chao eti watawadhuru. Kwangu hizi ni propaganda mfu. Ukweli ji kwamba kila kikundi au jamii inapenda kuwa na mwelekeo wa jambo moja katika hoja za msingi.

Mfano mzuri juzijuzi CDM ilitofautiana na makada wake ikawaondoa sasa hata hao wa CCM wanaodhani kuw wanatofsutiana na chama chao waondoke tu wasiendelee kujificha nyuma ya wenzao. Huu ndio ninaouita unafiki mimi.

Mwisho CCM ndio wanaridhaa ya watu mru asikudanganye. Kama huamini subiri uone Jimbo la Kalenga, utashangaa na kubakia mdomo wazi.

Watu walionunuliwa hass vyombo vya habari nawashauri wasituharibie nchi. Bado tunahutaji nchi yetu iwe moja na tuendelee kuishi kwa amani hata kama tuna tofauti ya mitizamo kama ilivyo kwa sasa.



From: Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: RE: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR
Sent: Sun, Mar 2, 2014 11:22:22 AM

Kura ya siri imekuwa ni lazima kwa sababu ya CCM.  CCM kama chama tawala hakikutakiwa kuwa na msimamo kichama kwenye swala hili la katiba kwani wataonekana na wanaonekana kuvutia upande wao ili waendelee kutawala hata pale hawana ridhaa ya wananchi.

Hivyo ili kuinusuru nchi na kuhakikisha vyama kama vyama havipewi nafasi ya kuendeleza agenda zao kwa nguvu zote kama wanavyofanya CCM inabidi warudi nyuma waachie wanachama na nafsi zao waamue ni lipi lililo jema.  Kuwa na cocas za kichama ni dalili za kuigawa nchi.

Hii inajenga taswira ya kukiona chama cha CCM kama chama gandamizi ambacho kipo tu pale kwa maslahi ya watawala na wala sio maslahi ya wananchi.  Wasitake kulazimisha mambo kwani mwisho wake itakuwa mbaya kwani binadamu naye atafika mahali atachoka na akichoka amani itapotea.  Hatutaki hilo litokee.  Kama CCM inaamini ina sera nzuri basi wawaache wanachama wao wafanye wanayotaka kufanya kwa hiari yao na sio kuburuzwa.

TUNAOMBA TUDUMISHE AMANI

Herment


Date: Sun, 2 Mar 2014 11:10:45 +0000
From: ekunyaranyara@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR
To: wanabidii@googlegroups.com

Wnabidii
Naomba kidogo hebu tujadili kidogo hii hoja ya maslahi ya nchi.
Mimi ninavyoona kila mtu au kikundi cha jamii kinayo haki ya kutoa hoja yake na mawazo yake na pia kina haki ya kusikilizwa.
Hoja ninayoiona hapa kila hoja ikitoleww na CCM lazima ipingwe tena kikundi kidogo tu cha watu alimradi inatumia media kwa nguvu ma kwa fedha nyingi ili ionekane inapinga.
Kama ni kwa maslahi ya taifa tusiache wengi waamue hii ndiyo demokrasia tunayotaka ya wengi wape lakini na wachache wasikilizwe.
Binafsi sioni mantiki ya kungagania jambo linaloweza kuamuliwa na wengi hata kama wachache hawattaki. Kichaa kilichomo ndani ya demokrasia ni kuwa wengi wanaweza kuamua jambo baya hata kama wachache wanqona kuwa ni la hatari. Hatari kubwa ni kulazimisha ambako sasa kumeingia kwenye media ambazo sasa kwa nguvu zote wanalazimisha wanavyotaka wao.
Mimi mtizamo wangu ni kwamba jambo liamuliwe kwa uwazi kisha tusonge mbele. Kuna watu wanafiki tu ambao siku zote wanataka kufanya mambo kwa kificho. Hawa ni wabaya sana wanaweza kuuza nchi kwa vile wanapenda mambo ya kisiri.
Kwa nini tuamue jambo kwa siri wakati jambo linalofanyika ni la wazi na kwa maslahi ya nchi. Mimi siono mantiki ya msimamo huu wa kura ya siri.
Nadiriki kuwaita wahuni na wanafiki wanaopenda kujifichaficha. Hawa ndio wanaaoyumbisha nchi. Hata katika maamuzi yao huwa wana kauli mbili hawa. Hawaaminiki.
Hoja nyingine ni kwamba kama hupendi msimamo fulani ni vizuri ukawa wazi tu kwa nini utake kupinga kwa siri? Nani unataka aendelee kukuamini wakati haunae pamoja katika mambo ya msingi?
Kama haukubaliani naye achana naye kuliko kuendelea kumdanganya kuwa mko pamojja wakati wa usiku unamchoma. Nawapenda wazanzibari, wakati ule wa CUF na CCM kabla ya serikali ya umoja wa kitaifa ilijulikanα.


From: Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR
Sent: Sun, Mar 2, 2014 9:20:38 AM

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUTOKA ZANZIBAR NENDENI MKATETEE MASLAHI YA ZANZIBAR SIO YA VYAMA VYENU VYA SIASA

Hivi sasa tunaingia katika hatua nyengine muhimu ya mchakato huu wa kutafuta Katiba mpya ya nchi yetu. Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshakamilisha kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo imeshatangazwa.

Wale wote waliopata fursa hii ya kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba kutokea Zanzibar, kutoka katika chama chetu, katika vyama vyengine na makundi mbali mbali hawana budi kuweka maslahi ya nchi kwanza na kuweka pembeni itikadi zao za kisiasa ili wende katika Bunge la Katika kuyatetea maslahi ya Zanzibar. 

Wajumbe hao hawana budi wafahamu kwamba wazanzibari kwa muda mrefu wamekuwa wakililia suala la kutotendewa haki ndani ya Muungano huu, hivyo hii ni fursa pekee adhimu kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kupigania hadhi, haki, heshma na usawa baina ya pande mbili za Muungano na hatimae kutoka na Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliyo bora na yenye kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Tunawaomba sana mnaokwenda katika Bunge la Katiba, nendeni mkaitetee Zanzibar na sio vyama vyama vyenu vya siasa. Wala sio kutetea maslahi ya Tanzania kwanza kama inavyosisitizwa na baadhi ya viongozi na wanasiasa wasioitakia mema Zanzibar. Tanzania ni mtoto wa Tanganyika na Zanzibar. Haiwezekani hata siku moja mtoto awe na uwezo na mamlaka ya kuweka misingi na kuwapangia mambo wazee wake, badala yake mtoto apangiwe na wazee wake. Ndio hivyo hivyo Katiba ya Shirikisho la Tanzania, mamlaka yake na mipaka yake ilitazaliwa ikiwa ni mtoto atokanae na maamuzi ya watanganyika na wazanzibari kwa namna ambavyo wanataka, na sio Tanzania ikasimu mamlaka na iweke mipaka kwa Tanganyika na Zanzibar.

Nawatakia kila la kheri na afya njema wajumbe wote wa Bunge la Katiba, wende wakaifanye kazi yao kwa uadilifu na warejee wakiwa na afya njema na Katiba bora kwa watanzania wote.

Amin.


Wasiliana na Maalim Seif: https://www.facebook.com/pages/Maali...63084730502824


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment