Nimesoma makala yako Happyness na kuielewa kiasi cha kutoa maoni.
Sikubalianai na baadhi ya mambo na nakubaliana na mengine. Sijui kama ninayokubaliana nayo ndiyo mengi lakini nadhani ndiyo.
Moja kati ya mambo nisiyokubaliana nayo ni kuwaita\ wabunge waliokosa wWAHUNI. Sikubali kuwaita wahuni la sivyo na waliotunga kanuni zilizowaadhibu wanaweza kuitwa wahuni. Ninaamini kanuni zilitungwa na adhabu zake kwa sababu hiyo ilitarajiwa. Mfano siamini kuwa kuna sheria au kanuni inayomzuia Mbunge kuvua nguo bungeni. Kosa hilo halitarajiwe na likifanyika litakuwa la kihuni. Haya mengine yanatarajiwa na baada ya kutumikia adhabu watarudi bungeni na kuendelea kuitwa\ waheshimiwa wawakilishi wa wananchi.
Nakubaliana na wewe kuwa Bulaya kuhamia CHADEMA amekuwa mwana harakati badal\a ya kuwa mwanasiasa.
Moja katiya tofauti ya Mwana harakati na Mwanasiasa ni hii haitarajiwi kuwa mwanaharakati akikosoa atakabidhiwa madaraka kusahihisha anachokikosoa. Ukwseli upinzani unaoonekana Tanzania wapinzani wanaelekea kuwaaminisha kuwa kazi yao ni kukosoa serikali wala sio kujiandaa kuingia madarakani.
Jinsi wanavyotaka kuonekana live kwa wananchi; jinsi wanavyochukua hatua na kadhalika tutafikia mahala watakuwa wapinzani milele na CCm itakuwa chama tawala milele. Hii ni hatari.Watanzania wa sasa wanachambua. Kama chama cha siasa kitapiga kelele bila kuangalia kitapoteza heshima mbele za umma. Mfano kipindi kilichopita wabunge walipotoka Bungeni nwalikuta umma uko upande wao. Sababu kubwa wabunge hao walikuwa swanatoka nje kwa sababu ya matatizo ya wananchi na wananchiu walikuwa wanawaelewa. sasa wabunge kutoka nje kwa sababu ya Job Description ya waziri! Mtu mzima ukasusa kujadili bajeti ya waziri mkuu. Au kutoka bungeni kwa sababu ya bunge kutoonekana live. Bunge kuonekana imekuwepo toka 2005. lakini tulikuwa tunaliona bunge kwa vipindi na tuliwaelewa wabunge wetu. Tuliokuwepo tulimfahamu sana Tuntemeke Sanga, Njeru kasaka na wengine. Bunge halikuwa live. japo ipo haja kwa wabunge wetu kutetea hilo loakini lazima wajue si kiasi cha kususa bunge. Ni mjadala bungeni. Uanaharakati huo hautawapeleka tunakotaka.
Ninawashangaa hata wanaharakati wanaopinga adhabu iliyotolewa kwa wabunge. Sera ya awamu ya tano ni kubana matumizi. nani anapinga hilo? Sasa wabunge kuamua kusimama hamsini na kusema kwa pamoja kwa hiyo siku ikapita bila kuamua lolote na hivypo kupata posho ya bure inachangia nini katika mwelekeo wa kubana matumizi? Mtu anayewatetea kuwa ni kosa kuwaadhibu waliofanya hivyo ana akili gani? Uanaharakati mwingine unaweaa kutafsiriwa ili vyo kuwa watu hawa wanatumwa na wanaowafadhili. Mimi hao dnio najua wana nia mbaya na mataifa haya. lakini wabaya zaidi ni hawa wanaopokea fedha kokote bila kujali ni za nini. Zinawaaibisha wanaposimama na kutetea utumbo kama huo wa kuwalaumu waliowaadhibu wakosaji.
HIVI AKILI NI KUKOSOA SERIKALI TU? HAKUNA KUWAKOSOA WAKOSOAJI? HAKUNA KUIKUBLIA SERIKALI AU KUISHUKURU? HIVI NDIVYO VIKUNDI NA VINGO VYA KUFUTA.
--------------------------------------------
On Wed, 6/1/16, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] HEKO BUNGE KUWAADHIBU WABUNGE WAHUNI
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, June 1, 2016, 10:32 AM
HEKO BUNGE KWA KUWAADHIBU WABUNGE WAHUNI
Na Happiness Katabazi
MHUNI ni neno linalotumika wakati mwingine
kumtambulisha mtu Mfulani Kuwa mhuni kwasababu hadhi yake
haimruhusu kutenda matendo ya kihuni sehemu usiyostahili
Kutenda matendo ya kihuni yakiwemo matendo ya kuvunja
Sheria, ustaarabu, miiko na Kutenda matendo yanayothibitisha
kudharau mamlaka Fulani wakati kuna Sheria ,Kanuni, Taratibu
na busara azimruhusu Kutenda matendo ya kihuni.
Nimelazimika kutumia neno mhuni kwasababu
makala yangu ya Leo itajadili "Azimio la Bunge kuhusu
Adhabu kwa wabunge waliofanya vurugu na Bungeni na kudharau
mamlaka ya Spika Katika Kikao cha pili cha mkutano wa
pili wa Bunge ,27/1/2016"
Uamuzi huo wa Bunge uliotolewa Bungeni Dodoma,
Mei 30 Mwaka huu , chini ya Kifungu cha 30A(1) cha
Sheria ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296
na Kanuni ya 74(4) na (6).
Kwa mujibu wa nakala ya azimio Hilo la Bunge
linasomeka kama ifuatavyo;
" Na Kwa Kuwa ,Sheria na Kanuni hizo
zimeweka Masharti Kuhusu utaratibu Unatakiwa kufuatwa Katika
majadiliano Bungeni na kwamba Katika majadiliano hayo,
Wabunge wanapaswa kuheshimu na kutii mamlaka ya
Spika;
" Na kwa Kuwa siku ,Siku ya tarehe 27
Januari 2016 baadhi ya Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni
walifanya vurugu na kudharau mamlaka ya Spika ;
"Na kwa Kuwa , Mheshimiwa Spika alipeleka
suala la baadhi ya wabunge Hao kufanya vurugu na kudharau
mamlaka ya Spika Kwenye Kamati ya Haki ,Maadili na Madaraka
ya kuwataja wabunge wafuatao;
" Ester Bulaya ,Tundu Lissu waliudhurie
vikao vyote Vya mkutano wa Tatu wa Bunge la 11 vilivyobaki
kaunzia Mei 30 Mwaka huu pamoja na vikao vyote Vya mkutano
wa nne wa Bunge la 11 kwa Kuwa walipatikana NA makosa ya
ukiukwaji wa Kanuni na Kuonyesha dharau kubwa kwa Mamlaka ya
Spika na pia walihusika kwa kiasi kikubwa kuchochea vurugu
zilizotokea siku ya 27/1/
2016 ;
"Aidha Bunge limeadhimia wabunge Pauline
Gekul,GodblessLema,Kabwe Zitto na Halima Mdee ,waliudhurie
vikao vyote Vya Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11 vilivyosalia
kuanzia Mei 30 Mwaka huu ,kwa walifanya vitendo ambavyo ni
Vya utovu wa nidhamu na dharau kubwa kwa Mamlaka ya Spika.
Vitendo hivyo Vya vurugu walivyovifanya vilisababisha
kuvurugika kwa shughuli za Bunge."
Binafsi Naunga mkono azimio Hilo la Bunge la
kuwapatia Adhabu hiyo wabunge hao Saba waliopatikana
na hatia ya kuvunja Kanuni ya Bunge kwa Kutenda matendo Yao
ya kihuni ndani ya Bunge ya kudharau nafasi ya
Spika.
Nikiwa ni muumini wa Sheria ambaye nakerwa na
tabia ya watu wasiyo penda kutii Sheria bila shuruti
wakiwemo baadhi ya wabunge wetu ambao ni watunga Sheria
lakini wameamua kujifanya ni wahuni na bila aibu uhuni huo
wamekuwa wakiupeleka hadi ndani ya Bunge ambalo mambo mengi
ya mustakabali wa taifa letu yanajadiliwa humo .
Enzi za Utawala wa Spika Mstaafu Anne Makinda
enzi za utawala wa serikali ya awamu ya nne niliwahi
kuandika makala zaidi ya mbili za kukemea tabia chafu na za
kihuni zinazofanywa na baadhi ya wabunge wa CCM na
upinzani bila mafanikio yoyote Matokeo.
Lakini Mei 30 Mwaka huu, Bunge letu chini ya
Spika mpya Job Ndugai ' Mzee Kifimbo cheza' Mhadhiri
wa Sheria Naibu Spika Dk.Tulia Ackson wameamua kuacha kulea
wabunge wanaofanya matendo ya kihuni ndani ya Bunge na
imewapatia Adhabu ya Kifungo cha kutoudhuria vikao Kadhaa
Vya Bunge.Safi.
Ifike mahali baadhi ya wabunge mnajifanya sijui
mnawazimu vichwani Muweke pembeni huo wazimu wenu na mjue
kabisa hizi siyo zama zile mlizokuwa mmezoea kufanya uhuni
ndani ya Bunge Mnachekewa na kuachwa bila kuchukuliwa
Hatua.
Kila zama na kitabu Chake , mtambue kabisa kwanza
Watanzania wenye akili timamu Tunawafahamu kwa Majina baadhi
ya wabunge wanaofanya vitendo Vya kihuni bungeni licha Bunge
halionyeshwi Live ila kwa kuwa mhuni ni mhuni baadhi yenu
mmekuwa mkitumia simu Zenu kurekodi sauti Zenu mnapata
michango yenu bungeni na wakati huo kuna sauti za baadhi ya
wabunge wahuni wanaowaunga mkono wanatoa manasikika wakitoa
maneno ya kihuni ndani ya Bunge.Upuuzi mtupu.
Hivi hata siku Moja kwanini msijipe muda Mkae
chini mkatafakari ni Kwanini wanasiasa hasa wabunge
zama hizi mnadhaurika sana Mbele ya Jamii ya watu wastaarabu
, wasomi ?
Ni kwasababu baadhi yenu hamjiheshimu
,hamuheshimi Kanuni zinazowaongoza, mnatenda matendo ya ovyo
ndani ya Bunge tena wazi wazi .
Sasa kama Nyie baadhi ya wabunge tena ni watunga
Sheria mnakuwa wa kwanza kunajisi Sheria,Kanuni na
kudharau Kiti cha Spika mnafikiri huku nje watu
watawaheshimu?
Bunge limewekwa thamani nzuri za gharama
ukilinganisha na thamani za Hali ya chini zilizopo Katika
Mahakama zetu nchini.
Lakini wananchi,Mahakimu wanakuwa na heshima ya
Hali ya juu na hawatendi mambo ya kipuuzi wakati kesi
zikiendelea au wawapo nje ya viwanja vya mahakama licha
baadhi ya mahakama majengo yake ni mabovu.
Ni kwasababu mahakimu, majaji na watumishi wa
mahakama wanajiheshimu sana ndiyo maana hata wananchi
hawadharau huo mhilimi wa mahakama wanauheshimu na kuogopa
pia.
Bungeni kule kwasababu baadhi ya Maspika
walilegeza kamba sana wakaruhusu baadhi ya wabunge wafanye
matendo ya kihuni ndani ya bunge ya kuvunja kanuni,
kubwatuka ovyo matokeo yake leo hii wabunge mnasemwa vibaya
na kudharauliwa .
Mfano wanasheria wakutanapo wanapojadili mambo
yao wanamtaka mwanasheria mwenzao ajadili kama msomi wa
sheria azungumze kwa vielelezo aache kuwa kama mwanasiasa
ambao wanazungumza porojo .
Zitto na wabunge wenzake wamepewa adhabu hiyo kwa
mujibu wa Kanuni alali za Bunge na walistahili kupewa Adhabu
hiyo .
Kwasababu wametenda matendo ya kihuni
ambayo siyo tu yaliiletea rabsha bungeni pia Adhabu hiyo
imewashushia heshima Mbele ya Jamii kwasababu sasa tunahaki
ya kuwaita wabunge wahuni ambao wamevunja Kanuni za
Bunge kutoka na Adhabu hiyo ya Bunge.
Hivyo Napingana na wale wote wanaosema wabunge
walioadhibiwa yaani Zitto na wenzake wameonewa, eti ni kosa
Lao la kwanza hivyo Adhabu waliyopewa ni kubwa
halikustahili, ni mikakati wa serikali ya CCM kwa kumtumia
Naibu Spika Dk.Tulia Kuwafunga midomo wapinzani
bungeni,Adhabu hiyo inanyima Haki wabunge Hao kuingia
bungeni kuwawakilisha wananchi. upuuzi mtupu tena wa aina
yake.
Kama Adhabu hiyo kweli ina Lengo la Kufunga
midomo ya wapinzani bungeni ,Mbona haijatolewa kwa wabunge
wote wa upinzani?mbona bado wabunge wa upinzani Jana
Tumewashuhudia wakiendelea kutoa michango Yao ndani ya Bunge
bila kubughudhiwa?
Hoja kuhusu wabunge Hao walioadhibiwa Kuwa
Haki Yao ya kuwawakilisha wananchi bungeni imepotezwa
kutokana na Adhabu hiyo ya Bunge, haina mashiko kwasababu
kwanza kabla ya adhabu kutolewa ,walipewa haki zao zote
ikiwemo haki ya kuitwa, kuelezwa kosa na wakajieleza na
hatimaye hukumu imetolewa na wamepatikana na hatia na makosa
waliyotuhumiwa nao.
Katiba ya nchi yetu inatoa haki kwa wananchi wake
na pia Katiba hiyo hiyo inatoa wajibu kwa wananchi
wake.Huwezi kudai haki yako bila kutimiza wajibu
wako.
Wanasheria wanasema Haki yako inapoishia ndiyo
Haki ya mwenzake inaooanzia.Hao wabunge walikuwa wanatumia
Haki Yao ya kutoa mawazo Yao kwa mujibu wa a ibara ya 18 (a)
ya Katiba ya Nchi ya Mwaka 1977 lakini pia Haki hiyo
inaendana na wajibu .Na pia
Kwa Mujibu wa Kanuni ya 74(4)(6) ya Sheria
ya Haki ,Kinga Maadili ya Bunge Inawataka wabunge
wakati Katika majadiliano ndani ya Bung wanapaswa kuheshimu
na kutii mamlaka ya Spika.
Sasa hawa wabunge 'wafungwa,wahuni'
walishindwa kutimiza wajibu huo wa kuheshimu na kutii
mamlaka ya Spika walitenda matendo ya kihuni yaliyosababisha
wakashindwa Kutimiza wajibu wao ndiyo maana wameadhibiwa na
Bunge.
Kwa hiyo hoja ya Kudai Haki Yao ya kuwawakilisha
wananchi bungeni imeporwa,uamuzi huo ni ukandamizaji wa
kidemokrasia ni ya kipuuzi kabisa.
Wametenda makosa ,wakaadhiwa.Kama walikuwa
wanaipenda sana hiyo Haki yao ya kuwawakilisha wapiga
kula wao bungeni kwanini walishindwa kutimiza wajibu wao
kuheshimu mamlaka ya Spika ?
Na Ieleweke wazi Wapiga kura wa wabunge Hao
hawakuwatuma wabunge hao wahuni kwenda Bunge kuwasemea
matatizo Yao Kwanjia za kihuni ,kunajisi Kanuni za
Bunge.
Bali wananchi waliwatuma wabunge Hao
wakawawakilishe Wapiga kura wao kwa kufuata Sheria ,Kanuni
na Taratibu Wawapo ndani ya Bunge.
Tanzania ni Taifa linaloongozwa kwa mujibu wa
Sheria na siyo vinginevyo .Na Ibara ya 13 ( 1) ya Katiba ya
nchi inasomeka hivi ; " Watu wote ni sawa Mbele ya
Sheria Na wanayo Haki ,bila ya ubaguzi wowote kulindwa na
kupata Haki sawa Mbele ya Sheria".
Kwa Tafsiri ya Ibara hiyo wabunge
'wafungwa' hawakuwa juu ya Sheria licha ni watunga
Sheria wameadhibiwa kwa mujibu wa Sheria kwasababu Ibara
hiyo ya 13 (1) ya Katiba inatoa Usawa Mbele ya Sheria
.
Wameadhibiwa kwasababu wa mepatikana na hatia za
Kutenda kosa na kisheria huwezi kumshitaki mtu hadi ukamtia
hatiani bila kuwepo na kosa liloandishwa kwa mujibu wa
Sheria ,Kanuni.
Hivyo Adhabu iwe ni Funzo kwa wabunge '
Wafungwa 'kama wanapenda kujifunza lakini,na wabunge
wengine wawe wa CCM na vyama vya upinzani maana ndani ya
bunge pia kuna wabunge wa CCM na wamekuwa wakitoa maneno
yasiyo faa kwa wabunge wa upinzani licha hatujaona
wakichukuliwa Hatua kama hizo na kupewa Adhabu .
Tambueni Hilo Bunge ni Chombo kilichoanzishwa kwa
mujibu wa Ibara ya 62 (1)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977 nikasome sekta hiki
;
" Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
ambalo litakuwa na sehemu mbili,Rais na
Wabunge".
Na ibara 33(1) ya Katiba ya nchi inasomeka
;" Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
.
Ibara 33(2) ya Katiba hiyo inasema : " Rais
atakuwa Mkuu wa Nchi , Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi
Mkuu.".
Hivyo nyie baadhi ya wabunge na wanaharakati
uchwara mtambue vyema Kuwa Rais ni sehemu ya Bunge licha pia
ndiyo Mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali na Amir Jeshi
Mkuu.
Hivyo mtakayoyafanya humo bungeni Ana Haki ya
kuyafahamu kwasababu Na yeye ni sehemu ya Bunge
.
Na Rais Magufuli Katika Kipindi hiki anacho
endelea kuijenga serikali na kuakikisha ahadi zote
alizozitoa kwa wananchi Katika Kampeni za uchaguzi Mkuu
Mwaka 2015 wakati akiomba a chaguliwa Kuwa rais , nilazima
pia kuendane sambamba na yeye na safu yake kuisuka pia
mihimili mingine ambayo ni Bunge na Mahakama.Kwani yeye Rais
ni sehemu ya Bunge na hakatazwi kuwafanya mawasiliano
ya wazi,Siri na Spika na Naibu Spika wake.
Nchi haiendeshwi kihuni kama mnavyozani,huwezi
Kuwa na serikali imara halafu serikali hiyo ikubali Kuwa na
Bunge la ovyo ovyo .Nchi itayumba .
Tunataka Bunge imara ambalo lina wabunge
imara Ambao wanajua Kujenga hoja bila kufanya
vitendo vya kihuni ndani ya bunge ili Tujenge nchi
yenye uwajibikaji.
Kuwa mwanasiasa sio tiketi ya kufanya vitendo Vya
kihuni, kuvunja Kanuni kwa kisingizio Kuwa eti Naibu Spika,
Spika wanapendelea CCM au wanatumiwa na Mhimili wa Serikali
kugandamiza wapinzani .
Muunganwa asifiwi ushenzi, hata kama ni kweli
Spika, Naibu Spika wanatumika na serikali ,wanawagandamiza
wapinzani, wabunge wa upinzani mlipaswa mtumie njia sahihi
kupinga vitendo hivyo Vya Naibu Spika na Spika kuliko kuamua
kuvunja Kanuni Matokeo yake hata kama ni kweli hoja Zenu
zilikuwa ni za Msingi ,mmeishazipoteza,
mmeadhibiwa.
Mimi Mwenyewe siungi mkono Bunge kuto onyesha
Live lakini hata siku Moja sijawahi kufanya vitendo Vya
Uvunjifu wa Sheria Kuonyesha napingana uamuzi wa Bunge wa
kukataa Bunge lisionyweshwe Live.
Hakuna ubishi CHADEMA ya sasa baada ya uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2015 kumalizika siyo Chadema ya Kipindi kile
iliyokuwa imestawi, Chadema ya sasa tuwe wa kweli tu najua
baadhi ya wafuasi wengine wa Chadema wana Maradhi ya
kutokubali Chama chao kikosolewe watapinga , Chadema hivi
sasa ni kama imepoteza dira na Taratibu Umaarufu wake
utapungua.Huo Ndio ukweli mchungu.
Kambi ya upinzani Bungeni katika Utawala huu wa
serikali ya awamu ya Tano,chini ya Rais Magufuli ,imeyumba
sana .
Tazama Katika ukurasa wa Facebook wa Zitto
Kabwe utetezi wake kuhusu Adhabu hiyo waliyopewa ni sawa na
wa mtoto Mdogo ambaye ametega kwenda shule Akaamua kwenda
kinyemeleza ziwani kuvua SamakiWajinga wachache
ndiyo wanaamini utetezi wake wake Kwenye mitandao usiyo kuwa
na kichwa wa miguu.
Zitto hafai Kuwa kiongozi anafaha Kuwa
Mwanaharakati. Zitto na Chadema wapi na wapi?Kwanza sera za
Chama Chake cha ACT Wazalendo na Chadema ni tofauti.
Ajabu sana!
Mbunge wa Bunda (Chadema ) Esta Bulaya
namchukulia kama ni mwanasiasa kijana aliyepotea mwelekeo
.
Aiingii akilini haraka ,Bulaya Huyo Aliyehama CCM
Mwaka Jana akajiunga na Chadema licha ni Haki yake kwa
mujibu wa Ibara ya 20(1) ya Katiba ya nchi ya kujiunga
na Chama chochote anachokitaka .
Siasa za kiuanaharakati uchwara anazozifanya
Bulaya tangu ajiunge na Chadema zimeshindwa kumpambanua
Lengo lake analolitaka Katika ulingo wa siasa ni lipia zaidi
ya Kufanikiwa Mzee wa Steven Wassira na kufanikiwa kurudi
bungeni kwa awamu ya pili.
Bulaya ameshindwa kuleta Mageuzi
yanayowavutia wanawake vijana wavutiwe naye
zaidi ya kila kukicha kutoka nje ya Bunge na
Kulalamika Katika vyombo Vya Habari kwasauti ya juu
Mithili ya mtu aliyepandisha mashetani.
Mfano mzuri ni wa Mama Samia Suluhu alipokuwa
Mbunge, waziri alichaguliwa Kuwa Naibu Spika Bunge Maalum la
Katiba licha ni mwanamke alikuwa na staha ,unyeyekevu na
aliweza kushirikiana na Spika wake Samwel Sitta kuliendesha
Bunge lile lilokuwa lina vioja Vya kila aina .
Na mwisho CCM Mwaka Jana ikampendekeza Kuwa
Mgombea Mwenza wa kwanza mwanamke tangu CCM ianzishwe na
ndiyo amekuwa Makamu wa Rais wa kwanza Tanzania,tangu
Tanzania ipate Uhuru.
Leo hii wanawake tu namchukulia Samia kama mfano
bora wa wanawake wanaweza kwasababu wakati alipokuwa mbunge
,Naibu Spika hakufanya ufedhuli wa kudharau Kanuni kama Nyie
baadhi ya wabunge wanawake vijana Bulaya, Mdee
mnavyomfanya ufedhuli ndani na nje Bunge hadi
mmeadhibiwa.
Leo hii Nyie wanasiasa wanawake vijana mmeshindwa
Kujenga matumaini kwa wanawake vijana ili waige kutoka
kwenu zaidi zaidi hivi sasa Mara kwa Mara mmekuwa mkionekana
Kwenye Televisheni mkibwatuka tu ,kuropokaropoka hivyo
kujitengenezea sifa Mbaya ambazo hamstahili Kuwa
nazo kama wabunge wa kuchaguliwa wanawake
vijana.
Angalau hivi sasa Mbunge wa Arusha Mjini(
Chadema) , Godbless Lema Ukimtazama na kumsikiliza wakati
akitoa baadhi ya michango yake ndani ya Bunge
unapenda unamsikiliza licha U Lema wake bado
haujamtoka.
Lema angeweza kuandaliwa na Chama Chake angeweza
kuipeleka Mbele Chadema .
Hivi sasa Lema anaonekana ameanza kukomaa kisiasa
,ule uhuni wake wa zamani wa kuongea ovyo,umeanza
kumtoka.Hakika Godbles Lema amebadilika
kidogo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Freeman
Mbowe Leo hii Hana sauti zaidi ya wabunge wahuni .Simsikii
Mbowe akitoa matamko ya Kujenga Chama kama
awali.Kulikoni?
Ni hitimishe kwa Kulishauri Bunge hizo Kanuni
walizotumia wa kuwadhibu wabunge Hao Saba wa upinzani,
basi Mbele ya safari pia zitumike kuwaadhibu baadhi ya
wabunge wa CCM ambao nao wanalalamikiwa Kuwa wanawatolea
maneno yasiyofaha wabunge wa upinzani.
Pia Spika Ndugai na Dk.Tulia jiepusheni na tuhuma
zinazowaandama hasa wewe Naibu Spika Dk.Tulia Kuwa
unatumiwa na serikali Kwani msipojiepusha nazo kama ni kweli
hamtoaminika.
Mimi binafsi sina ushahidi na Hilo ila ukweli
mnaujua Nyie .Ila kama ni kweli wakati mkitekeleza majukumu
yenu ndani ya Bunge jaribuni Kuwa 'umpire' ,
yaani muwe katikati yaani refa ,msionyeshe Kupendelea upande
wowote .
Aidha na Nyie wabunge wakorofi, msiotaka
kuheshimu Kanuni,Sheria Mabadilike anze ni Kujenga
Utamaduni wa kuheshimu Kanuni na Kujenga Utamaduni wa
kuvumilia.
Sheria, Kanuni zipo tena mmezitunga wenyewe
,mziiti na mziheshimu mkishindwa kufanya hivyo Mkae mkijua
Naibu Spika Dk.Tulia ni Mhadhiri wa Sheria hivyo sidhani
atakubali kuona Kanuni na Sheria mnazivunja awache
bila kuwachukulia Hatua.
Wabunge Saba Tayari wameishaadhibiwa bila
kujali Umaarufu wao, na Bunge linaendelea vizuri bila
wao kuwepo na Matokeo yake Jamii hivi sasa inawachukulia ni
wabunge hao saba wahuni ambao wamepatikana na hatia ya
kudharau mamlaka ya Spika .
Mwisho nawashauri wabunge 'wahuni au wabunge
wafungwa,Tulieni mtu mike Adhabu Zenu kwa ni
dhamu.
Tabia ya baadhi yenu kukaa Kwenye mitandao
na kuwatafuta mazuzu huko mitaani wawatetee kwa Jamii
kupitia Mlango wa nyuma ili muonekane mmeonewa haitowasaidia
Kabisa maana Mimi Binfasi tangu Juzi nimekuwa nikipambana
vikali na baadhi ya watu tena wengine wakiwa waandishi
wakongwe ambao walikuwa wanajaribu kupotosha ukweli wa
hukumu hiyo ya Kamati ya Haki ,Madaraka ya Bunge
inayoongozwa na George Mkuchika kwasababu za kijinga tu kisa
wana mahusiano na wabunge Hao, waandishi Hao ni
wanachama wa baadhi Chama wanachotoka baadhi ya wabunge
wahuni .Na wamefyata Mkia.
Na Mbaya zaidi nakala ya uamuzi wa Bunge ipo
inayooelezwa makosa mliyotenda ,Kanuni iliyomtumika
kuwaadhibu, lini mlifanya makosa hayo.
Hivyo Tulieni Nyie wabunge wahuni mtumikie Adhabu
yenu iliyotokana na matendo ya kihuni mliyoyatenda ndani ya
Bunge Januari 27 Mwaka huu, mkavunja Kanuni na kudharau
mamlaka ya Spika wakati kwa hadhi yenu hamkumpaswa
kujivunjia heshima kwa kutenda uhuni ule wa kudharau mamlaka
ya Spika .Ifike mahala Utawala wa Sheria uheshimiwe kwa
vitendo.
Mungu ibariki Tanzania
Facebook: Happy KatabaziBlogg: www.katabazihappy.blogspot.com0716
7744941/6/2016.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment