Friday, 8 January 2016

[wanabidii] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. Chadema na CCM kwe vita ya Umeya Dar...

Hii ni habari namba moja kwa mujibu wa mtandao wa mjengwablog.com.
Umeya katika Dar na hususan Ilala na Kinondoni ni nafasi muhimu sana kisiasa. Unaposema Dar zaidi unazungumzia Ilala, na kisha inafuatia Kinondoni. Vita ya kuipigania Dar kwa maana ya Umeya itaendelea kuvutia wengi. Mahakama Kuu imeshatoa hukumu. Vita sasa itaendelea kupiganwa kwenye Mabaraza ya Madiwani katika wilaya hizo. Ni habari ya kuvutia na muhimu unapotafsiri siasa kubwa za nchi hii.


2. Afukuzwa kwa kuhalalisha hekalu la Rwakatare
Mwanasheria wa NEMC amefukuzwa kazi kwa kuhalalisha hekalu la Mch. Rwakatare lisibomolewe. Ni habari inayopewa nafasi ya pili na mtandao wamjengwablog.com


3. Chadema watathmini mpango kazi wa Mabadiliko ya Kweli

Imeripotiwa leo, kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, kimepiga kambi ya siku saba Moshi kutathmini mpango kazi utakaoleta mabadiliko ya kweli. Chadema inasema haya ya CCM ni ' cosmetic' kwa maana ya mabadiliko ya kupaka poda. Habari ya Chadema kukutana Moshi iliporipotiwa kwa mara ya kwanza, kuna waliodhani pia Chama hicho kinakutana kujipanga upya na hata kufanya mabadiliko ya ndani ya chama. 
Soma habari nyingine za ndani ikiwamo katuni bora ya leo. Ni kwenyehttp://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment