Thursday, 7 January 2016

[wanabidii] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. Jipu Necta lapewa siku 7 kutumbuliwa..

Hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza kwa mujibu wa mtandao waMjengwablog.com. Imeonyeshwa pia kwenye runinga Waziri wa Elimu alivyokuwa akisemezana na Katibu Mkuu Mtendaji wa Necta kuhusiana na sintofahamu ya mifumo ya upangaji matokeo. Imeandikwa leo, kuwa Waziri amesema inachangia kwenye kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

Elimu ni suala nyeti na inapohusu kutokuwepo kwa hakika ya mifumo inatia shaka zaidi kwa wanafunzi wenyewe na wazazi.

Mfumo mpya wenye kutiliwa shaka na Waziri ni GPA ambao haukuwepo hata wakati wake akiwa Katibu Mkuu Mtendaji Necta.

GPA ni Grade Point Avarage. Ni mfumo unaoangalia wastani wa alama alizopata mwanafunzi katika kipindi chote cha masomo yake. Inaweza kupangwa, kuwa A ni sawa na pointi 4, B ni sawa na 3, C, 2, na D 1.

Pengine kwa media kumtaja Katibu Mkuu Mtendaji Necta kama ' jipu' si kumtendea haki, maana, anatekeleza taratibu za mfumo ambao hakuupanga yeye kama Katibu Mkuu bali bila shaka, kama mifumo yote, kuna mahali imetoka na bila shaka, kwenye elimu kuna tafiti zimefanyika.. Na kama yeye mtekelezaji naye anauona kuwa haufai, na Waziri yupo wa kuongea nae, basi, zifanyike au ziangaliwe tafiti zilizofanyika kuonyesha udhaifu wa mfumo huu mpya wa GPA kulinganisha na uliopita. Kisha mabadiliko yafanyike, kama yatahitajika.

2. Meli yaibwa

Hii ni habari ya pili kwa ukubwa. Kimsingi inazungumzia kero ya ' panya' wanaotafuna kodi ya nchi kule bandarini kwa kupitisha makontena bila kulipiwa kodi. Nyaraka za mizigo ya meli nzima zimehujumiwa na hivyo vyote vilivyomo kwenye meli kutafunwa na panya kwa maana ya mafisadi. Mhariri anapoandika ' Meli imeibiwa' bila shaka amekoleza chumvi na kuwavuta wasomaji watakaostaajabia kuwa meli imeibiwa. Si jambo la kawaida. Tumezoea kusikia gari ikiibiwa, si meli. Na anayeiba meli anakimbilia wapi majini?

3. Afisa Biashara Ilala asimamishwa kazi

Habari hii inapewa nafasi ya tatu na mtandao wa Mjengwablog.com. Afisa Biashara wa manispaa ya Ilala amesmamishwa kazi kutokana na mambo mengine, kufanya urasimu katika utoaji wa leseni za biashara. Hii ni hatua njema na ya kpongezwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa kumsimamisha kazi afisa huyu. Katika wakati tulio nao wa kuhangaika kuinua uchumi wa nchi, jitihada zote zinazofanywa na watendaji wachache kuhujumu hata raia kufanya biashara ni za kupigwa vita.

Soma habari nyingine za ndani ikiwamo katuni bora ya leo. Ni kwenyehttp://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment