Saturday, 9 January 2016

[wanabidii] Habari 3 Kubwa Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. Umeya Dar Vurugu Mechi

Hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wamjengwablog.com. Kama tulivyochambua jana, umeya Dar uangaliwe katika picha kubwa. Ifahamike, Dar ni mkoa wa kitaifa na meya wa Dar ni nafasi kubwa sana kitaifa. Hii ni vita ya kuipigania Dar kati ya Upinzani na Chama tawala. CCM kupoteza nafasi za umeya kwa Ilala na Kinondoni kutatafsiriwa kama kupoteza nguvu zake za kisiasa ndani ya jiji kitovu cha siasa na biashara nchini.
Wakati huo huo, kuchelewa kupatikana kwa mameya wa Ilala na Kinondoni kunachelewesha kuidhinishwa kwa malipo ya miradi mingi ambayo huidhinishwa na Baraza la Madiwani. 
Huko tunakokwenda, kuna haja ya nafasi ya umeya kupigiwa kura na wananchi wakazi wa miji na manispaa husika. Meya isiwe suala la kuachwa kwa madiwani kujichagua wenyewe.

2. Rushwa ya ngono Masasi

Imeripotiwa kutoka Masasi kuwa Waziri wa Nchi, Tamisemi, Mh. Jaffo, amekemea vitendo vya rushwa ya ngono vinavyofanywa na watumishi. Tuonavyo sisi wa mtandao wa mjengwablog.com, ni kuwa, rushwa ya ngono ni moja ya kero kubwa zinazowasibu watumishi wanawake. Kama waziri Jaffo ameamua kuivalia njuga kero hiyo, basi, afanye kweli hasa kwa kuonekana adhabu zikitolewa kwa wenye kufanya matendo hayo ambayo kimsingi ni ya udhalilishaji wa kijinsia mahali pa kazi. Ifahamike hapa pia, kuwa rushwa ya ngono inayofanywa na watumishi wa Halmashauri Masasi iko iko kwenye sekta mbali mbali nchini. Ni habari inayopewa nafasi ya pili kwa ukubwa na mtandao wa Mjengwablog.com

3. Mahakama ya Mafisadi inasukwa

Hii ni habari yenye kuhusiana na moja ya ahadi za Rais Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi. Ufisadi bila shaka yeyote na hususan wenye kufanywa na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya umma ni moja ya sababu inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. Mahakama hii itakuwa ni ya namna gani ni mambo ambayo yanasubiriwa kwa hamu na umma.

Soma habari nyingine za ndani ikiwamo katuni bora ya leo. Ni kwenyehttp://mjengwablog.com

Maggid Mjengwa
Mhariri wa habari kwenye mtandao wa kijamii
http://mjengwablog.com/http://kwanzajamii.com
0754 678 252

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment