Friday, 1 January 2016

[wanabidii] Habari 3 Kubwa Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com


1. Kiapo kwa Makatibu Wakuu

Hii ni habari kubwa kwa siku ya leo ambayo mtandao wa mjengwablog.cominaipa nafasi ya kwanza.

Unaposema Makatibu Wakuu ina maana ndio Serikali yenyewe. Hawa ni watendaji wa shughuli za kila siku za Serikali. Hata Baraza la Mawaziri lisiwepo kwa nusu mwaka, bado nchi inaweza kwenda kwa uwepo wa Rais na Makatibu Wakuu.

Tunapozungumzia uadilifu wa viongozi, basi, Makatibu Wakuu na Manaibu wao wanapaswa kuwa kielelezo cha kutolea mfano kwa viongozi wengine, maana, ni Katibu Mkuu anayeratibu na kusimamia kinachotoka Hazina Kuu kwa utekelezaji wa mipango ya Wizara husika. Huyu hapaswi hata kidogo kuchezea shilingi ya Serikali. Na yeye akiwa mfano, watendaji walio chini yake watajipanga tu, kuhakikisha kila shilingi ya Serikali inatumika vema kwa kusaidia kusukuma maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Bahati njema, mara nyingi Makatibu Wakuu na Manaibu wao wengi wao wamekuwa na uzalendo mkubwa kwa nchi lakini wamekuwa wakikwazwa sana na wanasiasa kuingilia utendaji wa kazi zao, ama, kwa wanasiasa hao kutanguliza maslahi yao binafsi ya kisiasa ikiwamo hata kushinikiza kinachotoka Hazina Kuu kigawiwe kwenye majimbo yao kwa upendeleo na kusahau kuwa Tanzania ni zaidi ya majimbo yao. au kutanguliza maslahi ya kichama.

Inahusu maadili ya uongozi, John Magufuli ameanza na utaratibu mzuri katika hili la kuwalisha viapo watendaji wake wakuu Serikalini. Lakini, katika kuwasaidia zaidi watendaji hao, angeweza kwenda mbali zaidi kwa kuwalisha kiapo cha namna hiyo Mawaziri wake na manaibu wao. Iwe hivyo kwa Ma- RC na Ma -DC wake. Na mihimili mingine kama vile Bunge na Mahakama ifuate kwa kuiga hiki cha Magufuli.

Maana, tumeshuhudia baadhi ya viongozi wetu kuanzia Bungeni hadi Serikalini, wamekuwa ' Criminally rich'- Ni wenye utajiri wa kihalifu na wa wazi wazi. Haiwezekani Mbunge au waziri akae Bungeni kwa mihula miwili, na kwa mshahara wa Mbunge au waziri , na posho zake aweze kwa kipindi cha miaka kumi kuwa na utajiri wa kushangaza ikiwamo kujenga mahekalu ya kustajaabisha jamii. Ni kwa kipato gani kama si cha uhalifu kwa maana ya mtu kama huyu atakuwa ni mla rushwa mkubwa kupitia nafasi yake ya kiuongozi. These are criminals- Hawa ni wahalifu. Hivyo utajiri wao wa haraka ni wa kiuhalifu. Hakuna namna nyingine ya kuwaelezea.

Na Katika nchi ni vema kukatafutwa njia mbadala na za nyongeza za kupima, kufuatilia utendaji kazi na mienendo ya kimaadili ya viongozi na watendaji wake; iwe ndani ya baraza la mawaziri, mikoani na hata wilayani. Na kama kuna watu wenye kuwajua vema viongozi na watendaji wao, basi ni wananchi wanaowatumikia. Wananchi wanafahamu mienendo ya viongozi wao ndani na nje ya ofisi zao.

Hakika, ukiwapa fursa kufikisha maoni yao kwa njia za siri , basi, wananchi wana uwezo wa kuwachambua watumishi wao kwa maana ya viongozi, kwa mazuri na mabaya. Watakwambia ni viongozi gani wanaowajibika kwao, wachapakazi na wenye kufuatilia maagizo waliyoyatoa. Watakwambia pia ni viongozi gani ambao hawastahili hata kupewa cheo cha utendaji wa kijiji.

Ni imani yetu, kwa ari hii aliyoionyesha, John Magufuli katika ufuatiliaji wa watendaji wake, basi, anaweza kubuni njia ya kupata maoni ya moja kwa moja ya wananchi juu ya mienendo ya viongozi na watumishi wao katika ngazi zote. Na kama tungekuwa na utaratibu wa wazi wa wananchi kutoa maoni yao, nahofia, kuna baadhi ya viongozi na watendaji, ama wangewasilisha barua za kujiuzulu au kukataa uteuzi ili wapate muda zaidi wa kutekeleza azma zao binafsi kama vile biashara au kilimo kwa vile wangeelewa ugumu wa kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja na kwa kipato halali cha serikali.

2. Mlinzi wa Lowassa atimuliwa

Hii ni habari inayochukua nafasi ya pili kwa ukubwa kwa mujibu wa mtandao wa mjengwablog.com. Ni habari yenye kuhusiana na masuala ya kiusalama. Edward Lowassa amepata kuwa Waziri Mkuu na akahama chama kugombea urais kupitia upinzani. Imeandikwa gazetini leo, kuwa alitaka kuendelea kuwa mlinzi wa Lowassa, lakini, kuna vitu alishindwa kuvitekeleza kwa ufasaha, kitendo cha kuondolewa kimepelekea apeleke taarifa gazetini na ni kinyume na taratibu za kiusalama.

3. Kardinali Pengo alazwa Muhimbili

Mwadhama Kardinali Pengo ni kiongozi wa kanisa Katoliki lenye wafuasi wengi. Habari za kuugua kwake na kulazwa hospitalini zimevuta hisia za wengi hata wasio Wakatoliki. Si ajabu, kiongozi mkuu wa nchi kumtembelea kumjulia hali. Kama akiendelea kubaki hospitalini, yumkini viongozi wengine wa kitaifa ikiwamo wa madhehemu mengine watakuwa njiani kwenda kumjulia hali. Ni habari inayopewa nafasi ya tatu kwa uzito na mtandao wamjengwablog.com kwa siku ya leo.

Usikose kusoma habari kubwa ya michezo kwa siku ya leo, na katuni bora kwa siku ya leo. Ni kwenye http://mjengwablog.com

Maggid Mjengwa
Mchambuzi / mjengwablog/kwanzajamii
0754 678 252


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment