Sunday 3 January 2016

RE: [wanabidii] TUKARIBISHE 2016 TUKIMSHUKURU MUNGU MUWEZA KWA KUMLETARAIS MAGUFULI HALI ILIKUWA MBAYA

Mpombe,
Hifadhi haya maneno yako hadi 2020 ndo uyalete hapa. Ni mapema mno kuanza kumsifia Rais. Ana mengi ya kufanya, sio tu kuleta maendeleo bali pia kurekebisha maadili ya watu.

Au ninyi mnamsifia kama mbinu ya kukuza kichwa aendelee? Maana CCM mna mbinu nyingi!

From: 'mpombe mtalika' via Wanabidii
Sent: ‎03/‎01/‎2016 23:01
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] TUKARIBISHE 2016 TUKIMSHUKURU MUNGU MUWEZA KWA KUMLETARAIS MAGUFULI HALI ILIKUWA MBAYA


Mwaka 2015 umemaliza na sasa tupo mwaka 2016 tunapaswa kumshuru mungu kwa hilo, tumeuga mwaka 2015 kwa sherehe za sikukuu ya Maulidi kwa waislam na siku iliyofuata tukasheherekea sikukuu ya Krismas pamoja na mwaka mpya.

Mahubiri yote ya sikukuu hizo hususani ya kidini wahubiri wametumia muda mwingi kuwataka waumini kuliombea taifa na kumuombea Rais Dk. Magufuli ili mwenyezi mungu amlinde na kumuwezesha kutumbua majipu na kupigania haki na usawa kwa wanyonge wote nchini bila kujali dini, kabila rangi wala jinsia yake ilimradi ni mtanazania awe wa bara au wa visiwani.

La muhimu kwa waumuini na wasiokuwa waumini ni kumshukuru Mungu kwa kuanza mwaka mpya wa 2016 tukiwa na serikali mpya chini ya Dk. John Pombe Magufuli huku tukijiuliza maswali haya.

Kwanini kama taifa tuna ulazima wa kumshukuru Mungu kwa kulijaalia Taifa hili kumpata kiongozi mpya aina ya Dk. Magufuli? Hilo ndilo swali la msingi kila muunini wa dini yeyote ile anapaswa kujiuliza.

DK. Magufuli ametokea wapi? Ujasiri huu alioanza nao katika kuliongoza taifa hili ameutoa wapi? Je Taifa hili lingemliza mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016 likiwa na hali gani kama Mungu muweza asingefanya makusudi yake ya kumleta mtu huyu anayeitwa Dk. Magufuli?

Serikali hii mpya ya Tanzania ingekuwa Seriakli ya namana gani kama Mungu asingemleta Dk. Magufuli?
Hali ndani ya Ccm na vyama vingine vya upinzani ingekuwaje kama angetokea mwingine wa chama kingine akamshinda Dk. Magufuli?

Maswali haya na mengineyo mengi tu, yanapaswa kumfikirisha kila mtanzania anayejitambua na kuitambua misingi ya nchi, hii ambayo kwa namana moja au nyingine imeliwezesha taifa hili kujitofautisha na mataifa mengine ya ukanda huu wa Afrika na duniani kwa ujumla.

Ili kufahamu kwanini maswali haya ni muhimu hebu turejee kwenye kipindi kilichopita cha michakato ya uteuzi ya vyama vya siasa kwa wagombea wa nafasi ya urais ilivyokuwa, ambao tuliwaona aina wanasiasa walioshiriki mchakato huo, nia zao na dhamira zao.

Hamasa kubwa ilianzia ndani ya Ccm amabapo makada 42 walichukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi hiyo ya urais, katika makada hao walikuwepo wenye sifa na wasiokuwa na sifa na vile vile sio wote walikuwa na nia njema katika kushika nafasi kubwa ya juu kabisa hapa nchini.

Katika mkada hao 42 wengine walikuwa hawapati coverage kabisa kwenye media na wengine kutokana na mitandao yao walikuwa wanapata coverage tena front page kwa muda takribani mwaka mzima kabla ya mchakao kuanza mpaka ikapelekea kuanza kampeni kabla ya muda na Ccm ikawapa adhabu na kuwafungia baadhi ya makada.

Kama ingekulikuwa utashi wa binadamu tusingempata Dk. Magufuli bali tungekuwa na Rais mwingine ambaye kwa utashi wa binadamu tulikuwa tunamuona anafaa kutokana na pesa na coverage ya media aliyokuwa akiipata.
Ni wazi kwamba kama tungempata rais anayetokana na utashi wetu na si wa Mungu tungempata rais wa hovyo hata serikali yake ingekuwa ya hovyo kabisa, ingekuwa serikali yenye muelekeo na utashi huo huo wa kibinadamu.

Uhovyo huo tungeanza kuonekana katika muundo wake kwa kuwa na serikali ya kishikaji zaidi, na madaraka yangegawanywa kwa marafiki kwa kupeana kama peremende kwa sababu tu walioiwezesha serikali hiyo ni binadamu na mapesa yao, tena kila mmoja angetakiwa kulipwa fadhila kulingana na mchango alioutoa.
Lakini Tunamshukuru mungu kwa kuingia 2016 kwa kutuletea Dk. Magufuli kwa kuwa, Magufuli ni tiba kwa nchi na Ccm, wengi wetu tunaamini kuwa kama ataendelea na kasi yake hii hadi mwaka 2020 hatokokwa najasho lingi kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment