Monday, 4 January 2016

Re: [wanabidii] Elimu ya Awali-Chekechea

Ninavyoelewa-kila shule ya msingi inatakiwa iwe na darasa la chekechea au shule ya chekechea. Mwongozo wa darasa au shule hizi ulikuwepo na upo Wizara ya Ustawi wa Jamii zamani ambapo baadae iliunganishwa na Wizara ya Afya. ndio ilikuwa na vyuo vya kufundisha walimu wa shule ya Chekechea. Bila ya Shaka shule hizi bado zipo chini ya ustawi wa jamii mojawapo ni ile ya Mwanga inayofundiwa awlimu wa walimu wa shule za chekechea na walimu wa chekechea na kuwapeleka field work ktk shule hizo. Pia, Ustawi wa jamii inafundisha maofisa katika vyuo vyao wa kusaidia walio na kesi mahakamani-deski lao mahakamani; walimu wa shule za walemavu (Yombo vituka Folk Dev College yao ya vilema). Hapo wakisomea typing, ufundi kushona charahani, kushona viatu na kuwasaidia lkupata ajira, kujiunga vikundi kupata misaada na kushona. Wakipewa hapo tender za kushona magwanda ya watumishi wa serikali. Ninazungumzia uzoefu wangu huu wa miaka mid 1980s to mid 1990. Ustawi wa jamii walichukua na kusimamia kambi za wazee, watoto yatima na vilema na wenye ukoma. Baadhi ya kambi hizi zamani ukoloni zilikuwa chini ya makanisa. Mfano Kanisa Katoliki lilikuwa na kambi ya wazee na watoto yatima na leprosariants (wenye ukoma). Katika kambi ya watoto yatima kulikua na wenye ulemavu wa ngozi (zeruzeru) ambao aidha walitupwa na familia zao au waliuawa na baadhi ya ndugu waliwasalimisha kambini hapo. Pia kanisa likisaidia wazee waliokuwa hawana ndugu kuwapa chakula na nguo za mitumba. Mitumba ilianza kuletwa kutoka ulaya na makanisa kuwapa hao watoto kila aina ya nguo-sweta, chupi, viatu etc na kuvisha kambi zote. Yatima waliolelewa walisoma kuanzia pre-school mpaka sekondari na makanisa yalikuwa na vyupo vya ufundi seremaala, gari, ujenzi, kushona nguo, mifugo na majosho yake; kufuma masweta masista wakifundisha, kutengeneza magodoro (ya sufi ndani); kufuma vitambaa na mapambo, mapichi-keki za aina aina etc..
Enzi hizo kuanzia madarasa ya chekechea kusoma ni kiingereza na kusali kanisani shule mnaitwa majina kama ulisali au hapana.

Shule ya Chekechea inatakiwa iwe na vitu vya lazima-chumba cha chakula, choo cha watoto na wengine ni vilema, chumba cha kulala na kupumzika muda fulani na kulala watoto wagonjwa mpaka mzazi aje kumchukua. Maeneo ya michezo ya kubembea au kukimbiakimbia na kucheza mpira. Ndio utaona kwa mfano UDSM campus kuna shule ya msingi na ya chekechea lakini ya chekechea darasa lake linakuwa mbali kidogo linatengwa na madarasa ya kawaida ya std 1-VII kutokana na kuhitaji space ya privacy niliyotaja hapo juu. Eneo lao la kusoma na kucheza na safety withing the school compound linakuwa na fence na huduma zake. Hii inapunguza watoto/wanafunzi wakubwa kuwaonea. Kupunguza wizi wa watoto kunatakiwa kuwe na picha ya mlezi/mzazi anayekwenda kumpeleka na hasa kumchukua kwani anaweza akapelekwa akatelekezwa na pia akachululiwa akaibiwa.

Walimu wa chekechea wanaosoma vyuo vya ustawi wa jamii mojawapo ya mafunzo yao nilivyoona ni kujifunza kuchora na kuandaa michoro ya kufunsishia, kujifunza kufuma na kutengeneza midoli ya kuchezea watoto; kutengeneza kwa vifaa asili vibango vya kuhesabia kwa shanga, mbegu za matunda ya miti, vijiwe na maumbile mengine mengi ambayo pia ataweza kuwafundisha watoto ubunifu wa kutengeneza vitu vya kujifunza hesabu etc. Kila stage ya kuanza kuna jinsi ya kufundisha kuanzia anapoanza age 3, 3-5 hadi 6 akiandaliwa kuingia std 1 akiwa na miaka 7. Kwa sasa TZ inatoa kipaumbele kuandikisha watoto waliopitia chekechea na akimaliza chekechea ana vyeti vyake pia. Pia anakuwa na kadi yake ya Afya kwa kuzingatia Tanzania School Health Program na akiandikishwa Chekechea anakwenda na kadi ya hospitali ya kuzaliwa kama anayo ili waelewe matatizo yake kiafya na wanapimwa mashuleni.


Wazazi hiitwa vikao vya shule vya chekechea na kuelekezwa usalama wa watoto na majukumu. Baadhi ya wazazi hukataza watoto wasiende shule au hawawapeleki shule siku ya kutoa dawa za minyoo; kuwasindikiza watoto shule mzazi anaweza akamuacha mpaka kiza kinaingia.

Kusoma chini ya Miti
Vijijini watoto husoma chini ya mti kutokana na umbali wa shule au darasa la chekechea lilipo hapo shule ya msingi ni kilometa tano. Mzazi anakwenda shamba au kujitafutia riziki. Kitongoji kingejenga darasa na kumchagua kijana apate mafunzo na maelekezo ya muda mfupi na kujitolea kufundisha watoito ambao wazazi wangewaacha home kutwa au kwenda nao mwendo mrefu shamba na kuwa unhealthy kutokana na mwendo na kushinda njaa. Unakuta-pamoja na kuwa kijiji kina kila arslimali na hata kuwa waanchoma na kuuza tofari za udogo-kujenga daraza na kulisakafia kwa gypsum ambapo ipo hapo kijijini na mawe yake na nyasi zipo za kuliezeka vizuri, mafundi wapo-wanaona si kazi yao ni ya serikali! Watoto wapo kutwa kucheza mazingira machafu, wengine kuwinda ndege kutwa porini na kaka zao kuokota matunda. baadhi ya watoto huachwa kwa bibi kizee au nyumba maalum yenye wali ndani ambao hupewa mchele, unga, maharage wakae nao na kuwapikia wale. Usiku baba na mama wanakuja wamelewa mbwiii wanawachukua kwenda nao home, kesho tena ni hivyo. Wazazi wanaweza na wanashauriwa kama kijiji ni kikubwa (na vipo vikubwa hasa vya radius kwenda katikati ya kijiji 5-30 kms) bajeti ya vijiji iendayo kata wilaya iwe na mipango ya kuja huko mbele kijiji kiwe na shule zaidi ya moja kwa baadhi ya vitongoji watoto wasiende kilometa 5-10 kwenda shule. Vijiji vikubwa sana watoto hawaendi shule hata hawasomi. Watoto vilema-hawawezi kutembea mwendo huo kuanzia akiwa chekechea. Pia, kuna ubakaji wanaume watu wazima huwabaka na hawawaambii wazazi-wanaowabaka wanaawtishia na wazazi wakali wanakuwa tata kuwapiga au kuwakataza wasiseme-aibu. Tumetibia watoto wengi STDs wanaobakwa njiani wakienda-kurudi shulke, shamba na majumbani, watoto kutumika kilabuni kuuza karanga etc katika umri miaka 5-10 ambapo anatakiwa awe darasani.

Vijiji vingine waliopewa power tiller wanaitumia na kitoroli chake kama gari ya usafiri ya kupeleka wanafunzi shule, wakulima shamba badala ya kutumia kitoroli kubebea mazao. Darasa la awali linamfanya mtoto apende shule, aanze mapema kujifunza misingi ya afya na kuacha michezo hatarishi; kugundua watoto wenye mahitaji maalum; kuboresha asha ya awtoto kupitia mradi wa GVT wa afya mashuleni ambao upo nchi nzima; kugundua wenye vipaji na wengine ikifika umri wa miaka 6 anaruhusiwa kuanza std 1 kutokana na natural braind na intelligence aliyonayo ktk umri mdogo.

Ila, kuna wazazi pumba sana sana. Wanapeleka watoto wadogo wa miaka 3 boarding eti international school. Aidha wanataka kula maraha au misifa tu kuwa yupo international school au ugomvi mume au mke anamkomoa mwenzake asije kila mara hapo kumuoan mtoto. Anampeleka mbali boarding ambako kuna shule moja sitaitaja jina nilikuwa watoto wadogo mno momoja akimwita kila mwanaume aliyepita (baadhi ya wazazi) Baba. wakiwachanganya kulala na kushinda vijana wa kiume wakubwa (form 1-4) na hao watoto wadogo wa Chekechea. Very dangerousa kwa sababu ya vijana wakubwa huonea na kulawiti wadogo shule za boda na zisizo za boda pia.

Elimu ya chekechea ikifutwa ni kuwacha watoto washinde magulioni na mama/walezi wao, kushinda magengeni kuuza karanga, kuwinda ndege na digi digi etc, kushinda vilabuni na wazazi wao walevi na mwisho kupenda kuzurura hovyo kuchukia shule kwa kuzoea kushinda mapamba nje. Darasa la awali au chekechea linasaidia kutayarisha vijana kupenda shule, kuwajenga ktk morals za jamii kwani hata huko shule kuna watoto wa chekechea wana matusi, adabu mbaya, wagomvi, wakorofi, wezi kuiba vya wenzao na kuwaonea-shule inawarekebisha na wazazi kuitwa. Wengine wana matusi sana kwa kuwa wanaona uovu wa wazazi wao. Tuhangaikie kuboresha hayo madarasa ya awali mbona wazazi wana uwezo; boresha vyuo vya walimu wa madarasa ya pre-school na wasaidie kupata vifaa kwa sasa vingi private sector inavileta toka ulaya na waseremala tunao na misitu ya miti mbao ni wazazi wanaoikata na kuharibu mazingira badala ya kutengeneza madeski na meza za watoto/wanafunzi wao.

Kukiwa na uji na chakula shuleni mpaka watoto wasiofika umri na waliopita umri wa chekechea wanapenda kuwepo shuleni kupata uji-wanakwenda kudoea.

Siku hizi watoto wadogo badala ya kuwa chekechea wapo kijijini mabanda ya sinema yanayoonyesha filamu kwa kutumia betri au solar. Wengine hukaa huko mpaka usiku wa manane wazazi wala kujali. Wengine ni humo ndani kama anaonyesha video au wazazi huangalia pamoja na watoto bila ya kujali maadili. Wakitoka hapo watoto hao wadogo husimulia wenzao mambo mengi na kuonekana wa ajabu na kufukuzwa kwa majirani wasicheze na watoto wao.

Kama kawa



--------------------------------------------
On Sun, 3/1/16, 'Sylvanus Kessy' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Elimu ya Awali-Chekechea
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 3 January, 2016, 21:32

Kwangu Elimu ya Chekechea ni muhimu sana. Elimu hii
huanzia miaka 3 hadi 4 na inafuata mtindo wa Montessori.
Yaani mtoto anajifunza kufanya kitu kadiri ya mazingira
yake. Na ndio maana mtindo wa montessori ni vitendo zaidi.
Mtoto anawekewa vitu vingi mbele yake. Kuchora, kupanga
vitu, kuunganisha picha au vitu mbali mbali, kuhaulisha maji
 kwenye chupa bila kumwaga chini, kucheza nk. Hapa mtoto
anaanza kufikiri kufanya kitu. Darasa hili kipaji cha mtoto
hujulikana kirahisi. Pia hujifunza silabi rahisi na
kuhesabu. Kwa mfano kuruka na kuhesabu 1,2, 3... Kuanzia
miaka 5 hadi 6 mtoto anafundishwa kusoma na kuandika na
kuhesabu. Mwaka wa 7 aende moja kwa moja darasa la
kwanza. 
Mtoto akiwa na shule nzuri ya chekechea darasa la
awali halihitajiki. Naona Darasa hili ktk shule zetu, halina
mwalimu wala chumba. Mara nyingi watoto hufundishwa chini ya
mti. 
Mie napendekeza Darasa la awali lifutwe kama tuna
shule nzuri za chekechea. Sababu ya msingi ya kufuta darasa
la awali, hakuna waaalimu wala vifaa vya kufundishia wala
vyumba vya madarasa. 




From: 'Athanas S.
MACHEYEKI' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
To: Mabadilikotanzania
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>;
"mabadilikoforum@googlegroups.com"
<mabadilikoforum@googlegroups.com>

Sent: Sunday,
January 3, 2016 6:20 PM
Subject: [wanabidii]
Elimu ya Awali-Chekechea

Wana
Mabadiliko,

Mimi huwa
ninafikiria sana juu ya umuhimu wa kuwa na elimu ya
chekechea hasa ktk nchi yetu. Hivi ni kweli kwamba
tunaihitaji elimu hii kwenye sekta ya elimu? Je, ikiondolewa
itaadhiri nini kitaaluma kama Elimu ya Msingi itatolewa
ipasavyo?

Naomba
kuwasilisha.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment