Thursday, 1 October 2015

Re: [wanabidii] Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki

Fadhil,
Hakuna hilo. Toa ushahidi kuwa Chadema imetumia vibaya hela za ruzuku ndipo uje hapa kubwabwaja. M4C imefanikiwaje kufikia nchi nzima kama
si matumizi ya uangalifu ya mapato ya chama. Acha hizo. Na huwezi kutufundisha demokrasia ndani ya chama wakati rais wenu anakuja kwenye mkutano
mkuu akiwa na majina ya wagombea anaowataka yeye mfukoni.
]em

2015-10-01 12:49 GMT-04:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:

Mama Nkya

Hata matumizi mabovu ya ruzuku na kuminya demokrasi ndani ya chama ni ufusadi tosha sio mpaka muongoze serikali.

On Oct 1, 2015 7:07 PM, "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Ninamheshimu na kuheshimu kazi za uandishi  za Johnson Mbwambo. Lakini ninapingana na miwani yake ya uchambuzi ilichoona   kuhusu jambo moja;chanzo cha ufisadi  uliosababisha nchi yetu kuwa na mafuriko ya mamilioni ya wananchi masikini.

Kadhalika napingana na Mbwambo  kwamba serikali ya Dr Magufuli (serikali ya CCM)  ufisadi wake utakuwa ni poa (afadhali) kuliko ufisadi wa serikali Lowassa (serikali ya CHADEMA-UKAWA).

Kimsingi kwa  vile wagombea Urais wote wawili Dr Magufuli na Lowassa  wamelelewa katika chama fisadi,  ni afadhali Lowassa aliyeondoka kwenye chama kinacholea na kunufaika na ufisadi --na sasa anaomba Urais kupitia  chama ambacho hakijawahi kuunda serikali na serikali yake (mlizi) ikawa fisadi--mwizi (mfano wizi EPA,Richmond,Tegeta escrow).

Zaidi ni afadhali serikali ya Lowassa (serikali ya UKAWA)  kwa sababu chama kilichomsimamisha kugombea Urais (chadema) ilani yake inasema wataweka misingi ya kuzuia serikali (mlizi) kuwa mwizi-- kwa kuandika Katiba Mpya inayotokana na mamoni ya Wananchi.

Chama anachogombea nacho  Urais Dr Magufuli --CCM hata kama Magufuli angekuwa ni mtu msafi kama malaika na mwenye dhamira njema kabisa ya kukomesha ufisadi--hawezi kufurukuta--hawezi kuleta mabadiliko yoyote endelevu--sana sana ataishia kuumizwa na mfumo wa kifisadi wa chama chake.

Serikali yake ya CCM  itaendelea kuwa mwizi kwa sababu chama chake CCM kinanufaika na ufisadi vinginevyo watueleze ni kwa nini hasa chama CCM ilikataa Katiba  Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ambayo ingejenga misingi ya kuzuia serikali (mlinzi wa mali za nchi) iwe ni ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR -Mageuzi au chama chochote kile isiwe serikali fisadi?

Tukumbuke--tatizo lolote katika nchi-linaondolewa kwa kuweka misingi ya utatuzi wa tatizo. Watu wa kutekeleza misingi hiyo hupatikana kulingana na misingi  iliyowekwa. Tanzania ya Dr Magufuli bila misingi ya kuleta mabadiliko ya kukomesha ufisadi--ni janga la taifa. Kama CCM ilivyo janga la taifa hivi sasa kwa kuzalisha mafuriko ya maskini tukubali tukatae--time will tell iwapo Dr Magufuli atachaguliwa--janga litakuwa mara dufu maana mfumo uliopo utahitaji serikali ya Dr Magufuli ifanye ufisadi mkubwa zaidi ili CCM iendelee kubaki madarakani.

Kwa hiyo, ili kukomesha ufisadi nchini ni afadhali Watanzania wamchague Lowassa, vyama vilivyomsimamisha Urais viandike Katiba Mpya--kuweka misingi ya kukomesha serikali zijazo zisiwe fisadi--kuepusha nchi yetu kuendelea kuzalisha mafuriko ya wananchi masikini.


 Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Thu, 10/1/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] Magufuli atashinda lakini mabadiliko hayaepukiki
 To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
 Date: Thursday, October 1, 2015, 1:20 PM





 NIANZE kwa
 kuwaomba radhi wasomaji wangu kwamba sitaonekana tena katika
 safu hii kuanzia
 toleo lijalo hadi mwanzoni mwa Desemba mwaka
 huu.


 Sababu
 yenyewe ni kwamba narejea kijijini kwangu wiki hii kwa ajili
 ya shughuli zangu
 za kilimo. Msimu wa kilimo utakapomalizika nitarejea tena
 Dar kuendelea na
 shughuli za uandishi wa habari.


 Nimeona
 niyaweke wazi hayo kwa sababu kutoweka kwangu ghafla kwenye
 safu hii (bila
 maelezo) kunaweza kutafsiriwa vibaya mitandaoni. Uongo
 unaweza kutembezwa
 mitandaoni kwamba nimehongwa fedha ili nisiendelee kuandika
 kwenye safu hii
 hadi uchaguzi mkuu umalizike.


 Kwa wiki
 kadhaa sasa nimekuwa nikiitumia safu hii kuweka msimamo
 wangu bila kificho
 kuhusu mgombea urais John Magufuli ambaye, kwa mtazamo
 wangu, naamini ndiye
 anayeweza kuaminika kukabidhiwa dhamana ya kuiendesha nchi
 yetu kwa kipindi cha
 miaka mitano ijayo.


 Johnson Mwambo

 Walio nje ya
 taaluma hii ya uandishi wa habari pengine walishangaa kuona
 mwandishi wa safu
 (Mbwambo) anamuunga mkono moja kwa moja mgombea urais wa CCM
 na kumkosoa wa
 Chadema. Hiyo ilikuwa tu katika kutekeleza wajibu wangu –
 yaani kuchangia
 katika juhudi za kuepusha nchi yetu isitawaliwe na mtu
 mwenye tuhuma za miaka
 mingi za ufisadi.


 Napenda
 kuitumia fursa hii kuwafahamisha wasomaji wangu ya kwamba
 mwandishi wa safu
 kumuunga mkono mgombea fulani wa urais ni jambo la kawaida
 kabisa duniani
 katika taaluma hii. Wanafanya hivyo kule Uingereza,
 wanafanya hivyo kule
 Marekani, na hata hapa Afrika ni hivyo hivyo.


 Gazeti au
 mwanasafu wa gazeti anaruhusiwa kabisa kuunga mkono mgombea
 fulani wa urais
 (endorse a candidate) ili mradi tu afanye hivyo wazi bila
 kificho, na wasomaji
 waelewe msimamo wa huyo mwanasafu au hilo gazeti tangu
 mwanzo kabisa.


 Kwa mantiki
 hiyo, napenda pia nifafanue kwamba bodi ya wahariri ya
 gazeti la Raia Mwema
 haikupewa maagizo yoyote na wamiliki wa gazeti hili ya
 kumuunga mkono mgombea
 yeyote wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Na badala
 yake wahariri wetu
 wamepewa maelekezo ya kuwatendea haki wagombea wote kwa
 kuzingatia zile kanuni
 kuu za habari zinazofuatwa kote duniani.


 Kwa ufupi,
 Raia Mwema halina rasmi mgombea urais wake – yaani
 haliku-endorse yeyote - awe
 Magufuli, Lowassa, Mama Anna Mghwira nk. Hata hivyo, kwa
 wanasafu wanaoandika
 maoni binafsi wa Raia Mwema, wao wana uhuru huo wa
 ku-endorse mgombea urais
 wanayemtaka. Na kama nilivyoeleza, hicho ni kitu cha kawaida
 kabisa katika
 tasnia yetu duniani.


 Ni kwa
 sababu hiyo nimekuwa nikiitumia safu yangu hii ya Tafakuri
 Jadidi kuwaeleza
 Watanzania maoni yangu binafsi kwamba Edward Lowassa hafai
 kuwa rais wetu mpya
 kwa sababu, licha ya kuandamwa na kashfa za ufisadi kwa
 miaka 20, hana jipya
 ambalo hakuweza kulitenda katika miaka yake zaidi ya 20 ya
 uongozi serikalini.


 Wakati huo
 ndio msimamo wangu binafsi, wanasafu wenzangu wengine nao
 wamekuwa wakitumia
 safu zao kwenye gazeti hili hili kuwahamasisha Watanzania
 wamkatae Magufuli na
 CCM yake na wamchague Lowassa. Narudia tena; yote hayo ni
 mambo ya kawaida
 kabisa katika uendeshaji wa magazeti duniani.


 Baada ya
 ufafanuzi huo, niseme kwamba ninaondoka Dar es Salaam kurudi
 kijijini nikiwa na
 imani kuwa mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli
 ataibuka mshindi katika
 Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Nisichokuwa na uhakika nacho ni
 ushindi wake
 utakuwa ni wa asilimia ngapi.


 Matokeo ya
 utafiti wa hivi karibuni wa asasi za TWAWEZA na IPSOS
 (SYNOVATE) yanaweza
 yasiwe na usahihi wa asilimia 100, lakini ukweli ni kwamba
 yanaakisi ukweli wa
 mambo ulivyo na utakavyokuwa Oktoba 25.


 Sina lengo
 la kurudia hoja nilizokuwa nikizitoa kwa zaidi ya mwezi
 mmoja katika safu hii
 zinazonifanya niamini kuwa Magufuli atambwaga Lowassa katika
 Uchaguzi Mkuu wa
 Oktoba 25. Itakuwa ni kuwachosha tu bure kurudia hoja
 hizo.


 Hata hivyo,
 jambo la msingi la kukumbuka ni kwamba CCM kimejiandaa
 mapema kwa uchaguzi huu
 kuliko Chadema, na kinaendesha kampeni zake kisayansi;
 ilhali Chadema ni
 mbwembwe
 na usanii
 tu.


 Hata uamuzi
 wa Chadema wa hivi karibuni wa kuongeza angani idadi ya
 helkopta za kampeni ni
 sehemu tu ya hizo mbwembwe. Kuna wakati kwenye uchaguzi wa
 serikali za mitaa
 kiliwahi kutumia helkopta tatu lakini kikaambulia ushindi
 kwenye kata tatu tu!


 Vyovyote
 vile, ubashiri wangu ni kwamba Magufuli atashinda. Ubashiri
 wangu mwingine ni
 kwamba kuhamia kwa Lowassa katika Chadema na kampeni ya
 urais aliyoifanya
 hakutaleta mabadiliko makubwa kwa chama hicho kwa maana ya
 kuongeza viti vya
 ubunge.


 Kwa hiyo,
 kwa upande wa Chadema, ujio wa Lowassa utakuwa
 umekidhoofisha tu chama hicho
 kiutendaji kiuliko kilivyokuwa huko nyuma. Baada ya Oktoba
 25, hali ya Chadema
 itakuwa mbaya, na kama nilivyopata kusema awali, sitashangaa
 ACT Wazalendo
 kikiziba baadaye pengo la Chadema kama chama kikuu cha
 upinzani nchini. Ni
 suala la muda tu hilo kutokea.


 Na hili
 linanikumbusha maneno ambayo (sina hakika na ukweli wake)
 niliyoambiwa hivi
 karibuni na swahiba mmoja wa karibu wa Lowassa kwamba
 mheshimiwa huyo alipoamua
 kujiunga na Chadema ili agombee urais alijua fika kwamba
 hatashinda urais huo
 kupitia chama hicho!

 Kwa mujibu
 wa maelezo yake aliyodai kaambiwa na Lowassa mwenyewe,
 swahiba huyo anasema
 Lowassa aliamua kugombea urais kupitia Chadema ili
 'kukiadhibu' chama hicho kwa
 kumchafua kwa zaidi ya miaka tisa kuwa ni fisadi
 mkubwa.


 Lakini pia
 aliamua kugombea urais kupitia chama hicho ili kupata fursa
 maridhawa ya
 kulipiza kisasi kwa Rais Kikwete ambaye aliweka kando
 uswahiba wao na kumtosa
 wakati ule alipoandamwa na kashfa ya ufisadi ya Richmond
 kiasi cha kumlazimisha
 kujiuzulu uwaziri mkuu.


 Swahiba huyo
 wa Lowassa aliniambia ya kwamba 'adhabu' ya kwanza kwa
 Chadema ni huo
 mparaganyo uliosababisha Katibu Mkuu wa chama hicho
 aliyeshiriki sana
 kukijenga, Dk. Slaa kujiuzulu nafasi yake. Si siri kwamba
 mpaka sasa Chadema
 kinapwaya kwa kumkosa mtu wa sampuli ya Dk. Slaa kukaimu
 nafasi hiyo.


 Adhabu ya
 pili au tuseme pigo la pili la Lowassa kwa Chadema ni hilo
 la 'kuwalazimisha'
 kina Mbowe na Lissu ambao walikuwa vinara wa kumwita fisadi,
 kuyameza matapishi
 yao wenyewe kwa kumsafisha wakati wa kampeni za urais kuwa
 si fisadi.


 Kwa mujibu
 wa swahiba huyo wa Lowassa, hakuna jambo linalomfurahisha
 mgombea urais huyo wa
 Chadema hivi sasa zaidi ya kuwaona Lissu na Mbowe wakihaha
 jukwaani kujaribu
 kuuaminisha umma kuwa walikosea kumwita Lowassa fisadi.
 Yaani anafurahi kuwaona
 wakimeza matapishi yao wenyewe!


 Kwa mtazamo
 wake, hiyo ni adhabu kubwa kwa kina Mbowe na Lissu kwa
 sababu heshima yao,
 weledi wao, uungwana wao, uadilifu wao na uaminifu wao kwa
 wanachama wa Chadema
 sasa uko shakani kwa sababu ya 'kumeza' matapishi yao
 hayo.


 Kwa maana
 hiyo, Lowassa anajiona 'kalipiza kisasi' kwa vinara hao
 wa Chadema waliomwita
 fisadi, na kwa Chadema yenyewe ambayo anaamini
 itasambaratika baada ya Uchaguzi
 Mkuu wa Oktoba 25!


 Kuhusu
 kulipiza kisasi kwa Kikwete, swahiba wake huyo alinieleza ya
 kuwa kwa kugombea
 urais kupitia Chadema, Lowassa amepata fursa maridhawa ya
 kulipiza kisasi kwa
 kumpaka matope Kikwete wakati wa kampeni kuwa utawala wake
 wa miaka 10 ulikuwa
 hovyo kabisa, na kwamba ndiye aliyemlazimisha kuutia saini
 mkataba wa kifisadi
 wa Richmond. Fursa hiyo
 asingeipata kwa kiwango anachopata hivi sasa wakati wa
 kampeni za urais.


 Kama hayo
 aliyonieleza swahiba huyo wa Lowassa ni ya kweli, basi
 inamaanisha kuwa tangu
 mwanzo Lowassa alijua ya kuwa hatashinda urais kupitia
 Chadema, na alichokifanya,
 hivyo basi, ni kutafuta tu fursa ya kulipiza visasi kwa
 Chadema na Kikwete.


 Bila shaka
 anafanya hivyo kwa sababu hana cha kupoteza. Sitashangaa
 baada ya Oktoba 25
 akajirudia Monduli kustaafu kabisa mambo ya siasa; maana
 atakuwa amemaliza
 'kuwashughulikia' waliomwita fisadi kwa miaka
 tisa.


 Kwa hiyo,
 imani yangu ya tangu mwanzo kabisa kwamba Lowassa hana na
 hatakuwa na faida
 yoyote kubwa kwa Chadema baada ya Oktoba 25 imeimarishwa na
 kauli hiyo ya
 swahiba wake huyo.


 Tukirejea
 kwa CCM, ni kweli kuwa Magufuli atashinda lakini mambo
 hayawezi kubakia
 vilevile katika chama hicho na katika uendeshaji wa serikali
 yake. Kwa maneno
 mengine, mageuzi hayataepukika baada ya Oktoba 25 labda kama
 CCM kinataka
 kuishia vilikoishia KANU cha Kenya na ZANU cha
 Zambia.


 Kwa maneno
 mengine, kampeni zilizoendeshwa na zinazoendeshwa na Lowassa
 na Chadema yake,
 ni maandiko mengine ukutani ambayo CCM lazima itakuwa
 imeyaona na kuyasoma
 vyema kwa sababu ya ukubwa wa herufi zake! Itakuwa imeweza
 kuyasoma hata kama
 ina makengeza!

 Na maandiko
 hayo ukutani yanasomekaje? Yanasomeka hivi: "Ni wakati wa
 mabadiliko.
 Tumeichoka CCM kiasi kwamba hata shetani tuko tayari
 kumpigia kura aingie
 Ikulu".


 Huo ni
 ujumbe mzito na unaotisha, na ni chama-mfu tu cha kisiasa
 ndicho kinachoweza
 kuudharau ujumbe wa namna hiyo. Watu wakishafikia hatua ya
 kukata tamaa
 kimaisha kiasi cha kusema kwamba hata kama ni shetani wako
 tayari kumwingiza
 Ikulu, ni lazima CCM kijiulize; kulikoni?


 Na ujumbe
 huo si mtupu (hollow). Ni ujumbe unaoendana na hali ambayo
 imekuwa ikionekana
 katika mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa – yaani
 maelfu ya vijana waliokata
 tamaa ya maisha hufurika katika mikutano yake
 kumsikiliza.


 Hata hivyo,
 kitakachoikoa CCM na kumfanya Magufuli ashinde urais Oktoba
 25 ni kwamba,
 tofauti na Chadema, chenyewe kina muundo na mtandao wa hadi
 ngazi za vijiji na
 kata uliokiwezesha kuhahakikisha kila mwanachama wake
 amejiandikisha kupiga
 kura na siku ya kupiga kura kuhakikisha anajitokeza kupiga
 kura.

  

 Chadema
 hakina muundo huo, na pia hakina mtandao huo wa hadi ngazi
 ya vijiji na kata.
 Kwa hiyo, kinabakia tu na imani (potofu!) kuwa vijana wote
 wanaofurika kwa
 maelfu katika mikutano ya kampeni ya Lowassa wamejiandikisha
 kupiga kura -
 kumbe ukweli ni tofauti kabisa na huo. Kasoro hiyo ndio
 iliyomwangusha Dk. Slaa
 mwaka 2010, na ndio itamwangusha Lowassa Oktoba
 25.


 Lakini
 Chadema na ACT Wazalendo nk haviwezi kukubali kubakia na
 udhaifu huo huo kwenye
 uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020. Bila shaka navyo
 vitajitahidi kuweka ofisi na
 mitandao ya hadi ngazi za vijiji na kata, na hivyo uchaguzi
 mkuu mwingine wa
 mwaka 2020 unaweza kuleta matokeo tofauti kabisa na
 tutakayoyapata Oktoba 25
 mwaka huu.


 Na ndiyo
 maana nasema ya kwamba kama CCM kinataka bado kuendelea
 kukamata dola, ni
 lazima baada ya Oktoba 25 kifanye mageuzi makubwa
 yatakayoipa serikali yake
 mwelekeo mpya wa kutatua kero ambazo kwazo zilifanya vijana
 wafurike katika
 mikutano ya kampeni ya Edward Lowassa wakiwa na mategemeo
 kwamba ndiye
 atakayetatua matatizo yao.


 Yaani kama
 kama tatizo ni ajira, basi serikali ijayo ya CCM ni lazima
 ionekane kweli kweli
 ikitatua tatizo hilo. Kama tatizo ni maji, basi lazima liwe
 historia ifikapo
 mwaka 2020. Au kama tatizo ni kilimo duni na ukosefu wa
 masoko kwa wakulima,
 serikali ijayo ya CCM lazima ilitatue hilo kabla ya mwaka
 2020. Na kama tatizo
 ni kutamalaki kwa ufisadi nchini, basi lazima janga hilo
 liwe limemalizwa
 ifikapo mwaka huo.


 Vinginevyo,
 CCM kitakwenda na maji ifikapo 2020! Safari hii kitashinda
 uchaguzi kwa taabu,
 lakini safari ijayo kisipojirekebisha kitashindwa kiurahisi.
 Ndiyo maana
 naamini ya kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Lowassa
 ameisaidia/ataisaidia mno CCM kujiona kilivyo, na ndio
 sababu naamini kwamba
 baada ya Oktoba 25 'kitajivua gamba' lake la
 zamani.


 Vyovyote
 vile, kwa kuwa hii ndiyo makala yangu ya mwisho kabla ya
 Uchaguzi Mkuu wa
 Oktoba 25, napenda nirudie kile ambacho nilikisema huko
 nyuma. Kitu hicho ni
 kwamba wagombea wote wawili wa urais – Lowassa na Magufuli
 wana mapungufu ya
 wazi.


 Niliandika
 huko nyuma kwamba pamoja na wote kuwa na mapungufu makubwa
 kuna mmoja ambaye ni
 nafuu kidogo kuliko mwenzake (a lesser devil). Ombi langu ni
 lile lile: Kwa
 kuwa wote wana mapungufu makubwa tutajitakia balaa kama
 tutampa lesser devil
 wetu wingi wa wabunge wa chama chake bungeni. Yaani
 akivurunda tutakuwa hatuna
 njia ya kumdhibiti bungeni kwa sababu atakuwa na wingi wa
 wabunge.


 Kwa hiyo,
 salama yetu ni kwamba yeyote tutakayempigia kura – awe
 Lowassa au Magufuli,
 tusimpigie kura mgombea ubunge wa chama chake. Kwa mfano,
 kama kura ya urais
 unampa Lowassa, basi kura ya ubunge mpe mgombea wa CCM au
 ACT Wazalendo. Na
 kama kura yako ya urais unampa Magufuli, basi kura ya ubunge
 kipe Chadema au
 ACT Wazalendo.


 Kwa namna
 hiyo, tutajipa matumaini (japo kidogo) kwamba yeyote
 atakayeshinda urais kati
 ya hao wawili, Bunge litaweza kumdhibiti kama ataongoza nchi
 hovyo. Lakini kama
 akiwa na wingi wa wabunge wa chama chake bungeni (kama
 ilivyokuwa kwa CCM kwa
 miaka mingi), hatutaweza kumfunga 'gavana' hata kidogo
 kama akivurunda.


 Na mwisho
 kabisa nawatakia uchaguzi mwema na wa amani Oktoba 25.
 Nikirejea Desemba
 nitaendelea kuandika makala za kumkosoa (kwa hoja) mtawala
 wetu mpya bila
 kujali ni Magufuli au Lowassa; maana hiyo ndiyo kazi
 niliyojitwisha katika fani
 hii ya uandishi wa habari.


 Sikuingia
 katika fani hii ili kuwaremba na kuwasifu watawala wakiwa
 madarakani.
 Nitawasifuje watawala kama wanatekeleza kile ambacho
 wananchi walikitarajia
 wakati wanawapa kura zao?

 Nimeingia
 katika fani hii kuwakosoa watawala wanapovurunda ili
 wasilale usingizi; ilhali
 wananchi wanateseka. Kazi hiyo nitaendelea nayo bila kujali
 rais mpya ni
 Magufuli au Lowassa.


 Vyovyote
 vile, rais akichapa vyema kazi hakuna 'habari' hapo.
 'Habari' ni pale rais
 anapokuwa mvivu, mlevi, legelege, fisadi nk. Kwenye taaluma
 yetu ya habari tuna
 msemo maarufu; mbwa akimng'ata binadamu hakuna habari.
 Habari ni binadamu
 akimng'ata mbwa.


 Kwa maana
 hiyo, nitaendelea kuwakosoa watawala wetu, na sitajali ni
 Magufuli niliyempigia
 kura yangu au Lowassa. Nitamkosoa (kwa hoja) yeyote kati ya
 hao wawili
 atakayefanikiwa kuingia Ikulu Oktoba 25; maana hakuna
 'habari' katika kumsifu.
 Tafakari.





 --

 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

  

 Kujiondoa Tuma Email kwenda

 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
 kudhibitisha ukishatuma

  

 Disclaimer:

 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

 ---

 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.

 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment