Friday 30 October 2015

Re: [wanabidii] RE: [Wanazuoni] Neno La Leo: Mabadiliko [1 Attachment]

Kaka Mjengwa,


Nimesoma makala yako na ningependa kuchangia kidogo kuhusu machache uliyosema. Umeandika kuwa watanzania wamekuwa wavivu wa kutafakari kwa kina kuhusu ni mabadiliko ya namna gani tunayoyahitaji, nadhani hapa ndipo ninaposhindwa kukuelewa vyema. Kwenye nchi masikini kama ya kwetu hakuna kitu rahisi kama watu kujua mabadiliko wanayohitaji. Watu wanahitaji huduma bora za afya kaka Mjengwa, wanahitaji elimu bora na sio bora elimu. Wanahitaji kula vizuri, wanahitaji kupeleka watoto shule, wanahitaji umeme, wanahitaji kuwa comfortable kwenye maisha yao kama wewe na wanasiasa tunaowashabikia. Umetembea sana kwenye vijiji vingi vya Tanzania na ulikuwa ukituwekea picha za maeneo mbalimbali vijijini. Hali halisi unaijua na kusema kwamba watu ni wavivu wa kufikiri kuhusu mabadiliko wanayohitaji ni jambo la kushangaza sana haswa kusikia toka kwako kaka. Watanzania wengi hawapati hizi huduma na ndio mabadiliko wanayohitaji. Kama wakipata hizi huduma kwanini watalalamika? kwanini watataka mabadiliko?


Naungana na wewe kuwa watu wanaposema " CCM imechoka, nendeni mkachague hata jiwe!" sio kitu kizuri na ni kuidharau CCM na dharau si jambo zuri. Ni kweli kwa miaka mingi CCM imekuwa ikijaribu kuleta maendeleo kwa namna nyingi, CCM imedumisha amani, baadhi ya mambo wanayofanya CCM yanaonekana na yanahitaji kupongezwa. Lakini kuna mengi pia yanafanya watu wajiulize ni kwanini CCM bado iko madarakani? Watanzania kaka Mjengwa wanataka kwenda kwenye next step, hii next step itafanya mtoto wa mwanakijiji aweze pia kupanda ndege na kwenda kusoma hata kozi fupi ulaya. Hii next step itafanya watu waweze kufikiria taifa zaidi kuliko wao binafsi. Hii next step inahitajika na ni muhimu kama tunataka hama hatutaki, kitu unachotakiwa kujiuliza ni kwanini watanzania wengi hawaamini kuwa hii next step italetwa na CCM? Wapi ilifika watanzania wakapoteza imani na chama kilichokuwepo madarakani kwa miaka mingi sana? kwanini and nini kifanyike? 


Kwa umbali wangu na nchi yangu (kuishi abroad kwa muda mrefu) nimefuatilia uchaguzi kwa kiasi nilichoweza. Kitu ninachojitahidi kujiuliza kila mara ni je CCM wameshinda uchaguzi kwa mgongo wa Magufuli ama bado chama kina umakini na uwezo mkubwa wa kushinda uchaguzi? Je bado chama kina influence kama zamani? Nimeongea na watu wengi na kugundua pia wanamuamini sana Magufuli zaidi ya CCM. Wanaamini kuwa Magufuli ni mtu safi na anaweza kuleta maendeleo kwa watanzania. Kusema ukweli kabisa kutoka moyoni mwangu, Magufuli was the best option we had kwenye huu uchaguzi. Wengi tunaamini kuwa ataleta mabadiliko tunayohitaji lakini hatuamini kwenye CCM. Mimi binafsi nafikiri he can be the best and he can transform nchi yetu ingawa sijasahau kuwa mwisho wa siku siasa ni siasa na mwanasiasa ni mwanasiasa. Wamarekani weusi wengi wana msemo "nothing good for communities has come out of politics".


Tuombee nchi yetu isogee, tuombee nchi yetu ipate maendeleo tunayohitaji, tuombee nchi yetu yenye rasilimali zinazotafunwa sana na wachache isogee kidogo. Tusiwe watu wa upande mmoja kila mara. Tujaribu kuwaelewa wengine wanasema nini na kwa nini wanasema wanayosema. Kaka Maggid umeshuhudia waandishi hapo mkoani kwako wakipigwa na polisi hadi kufa. Haya yote yanahitaji kutafakari pale tunaposhabikia siasa za vyama badala ya maendeleo na uhuru wa taifa. Taifa ni zaidi ya chama.





2015-10-30 4:47 GMT-04:00 Surumedia <majiydsuru@gmail.com>:
Uko sahihi ndugu Mjendwa!
Wakati wa kampeni nilipata taabu sana kuhusu matumizi ya neno mabadiliko. Kiasi kwamba neno hilo lilikosa maana halisi ya neno lenyewe. Ilinishangaza hasa pale mwandishi mwanazuoni anaposahau kawaida ya matumizi ya maneno kwa makusudi.  Ilifikia baadhi ya wanazuoni walitumia neno mabadiliko wakimaanisha kuhama chama, kuacha ukweli, kupotosha, kujikataa, kujidharau na kufuata upepo wa ufisadi. Iliandikwa wakati fulani kwamba, wananchi ni wale tu watakaoweza kuchagua waliohama chama tawala, wanaokataa ukweli, wanaopotosha, wanaojikataa, wanaodharau, wanaobeza na wanaofuata upepo wa ufisadi unakoelekea. Ilichukuliwa kwamba, watakao chagua wasiohama chama tawala, wanaosema ukweli, wasiopotosha, wasiojikataa, wasiotudharau, wasiotubeza na wasiofuata upepo wa ufisadi kwamba hao siyo wananchi. Kwa Ujumla neno mabadiliko na neno wananchi wamepotoshwa sana katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu 2015. Tunayo nafasi ya kujirekebisha na kurejesha ufahamu wetu na Uanazuoni wetu.
Wakatabahu!

..........................................................................
"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".

Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa

From: Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com [Wanazuoni]
Sent: ‎30/‎10/‎2015 09:24
To: mabadilikotanzania; wanabidii; Wanazuoni@yahoogroups.com
Subject: [Wanazuoni] Neno La Leo: Mabadiliko [1 Attachment]

 
[Attachment(s) from Maggid Mjengwa included below]


Ndugu zangu,

Uchaguzi umeshapita. Tunafungua sasa ukurasa mwingine. Lakini, haina maana ya kuacha kufanya tathmini yakinifu ili tuweze kujifunza.

Tumeona, kuwa dhana ya mabadiliko ilitawala uchaguzi wa mwaka huu. Ni sahihi, kuwa mwanadamu, kwa asili, ni kiumbe mwenye kutamani mabadiliko. Ni kuanzia kwenye mavazi, chakula na mengineyo.

Tumekuwa wavivu sana wa kutafakari kwa kina juu ya tunamaanisha nini tunaposema tunataka mabadiliko katika nchi. Bahati mbaya, baadhi ya wanasiasa wameonyesha udhaifu mkubwa katika kuielewa dhana ya mabadiliko, ikawa kama wimbo wa taarab tu.

Ikafika mbali, kuwa waliosimama majukwaani kuhubiri mabadiliko hawakujua kama walifanya kazi pia ya kumhujumu mgombea ama wagombea wao wenyewe.

Sifa moja kubwa ya Watanzania ni dhamira na utayari wao wa kukataa kudharauliwa. Ilipofika mahali, watu wazima wanaojiita viongozi wakasimama majukwaani na kutamka; " CCM imechoka, nendeni mkachague hata jiwe!"

Huko ni kuwadharau Watanzania. Ni kauli kama hiyo ndio iliyowafanya Watanzania wengi waviache vitanda vyao alfajiri na mapema siku ya Uchaguzi Mkuu, waende kuhakikisha wanazuia 'mawe' yasipite. Maana, haikuwaingia akilini kuwa kwa miaka 54 CCM haikufanya chochote na kwamba imefika wakati wa kufanya mabadiliko kwa kuyaweka ' mawe' na CCM kuichimbia shimo kabisa. Kwenye siasa kauli zinaweza kupelekea kupanda au kuanguka kwa chama na mwanasiasa.

Na tuendelee kuitafakari dhana ya mabadiliko.

Ni Neno La Leo.

Maggid,

Iringa.

__._,_.___

Attachment(s) from Maggid Mjengwa | View attachments on the web

1 of 1 Photo(s)


Posted by: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)

Check out the automatic photo album with 1 photo(s) from this topic.
0.jpg


.

__,_._,___

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
Omar Kaseko
Kali TV Founder/Producer
http://www.kalitv.com
240-374-2192

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment