Saturday 31 October 2015

[wanabidii] RE: [Wanazuoni] Neno La Leo: Rasilimali Akili.. [1 Attachment]

Ni kweli Mjengwa!
Kijana mwenye elimu bora hujitambua, huthamini uhai wake na uhai wa wengine. Na kwenye ushiriki wake wa chaguzi za kidemokrasia, husimama kwenye misingi na kuchagua mtu atakayemfaa yeye na wananchi wenzake. Hawezi kusukumwa na chaguo la taharuki na mihemko ya chuki za wanasiasa. Kijana mwenye elimu bora hawezi kuhamasishwa kuandamana na kutumika kuharibu mstakabali wa maisha yake na ya wananchi wenzake kwa ajili ya kutetea kikundi cha watu wachache wenye uchu wa madaraka. Kijana mwenye elimu ya msingi iliyobora hawezi kusubiri watu wachache wafikiri kwa niaba yake. Na katika vigezo vya elimu bora kulingana malengo ya milenia, inasemwa kuwa moja ya sifa ya mtu aliyeelimika ni kupunguza maovu katika jamii yake kama ujambazi, ngono zisizo salama, na kuwa na non-violence behaviour. Elimu inasaidia kijana kujuwa wajibu wake, kabla ya kuwawajibisha wengine. Tofauti za nchi zetu za kiAfrika na wenzetu katika zao la elimu ni kwamba, sisi bado tunazalisha wimbi kubwa la wafanya fujo wanaosubiri maelekezo ya jinsi ya kufanya fujo kutoka kwa wanasiasa, wakati wenzetu wanazalisha wimbi kubwa la vijana ambao ni creative na productive. Elimu yetu bado inazalisha destructive group wakati ya wenzetu inazalisha productive group. Lakini bado tunayo nafasi ya kurudi katika misingi ya maana ya kuelimika, ingawaje uchaguzi huu umetoa taswira ya asilimia ya vijana wanaojitambua na kujua kiongozi na viongozi wanaotufaa kama taifa.

..........................................................................
"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".

Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa

From: Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com [Wanazuoni]
Sent: ‎01/‎11/‎2015 08:58
To: mabadilikotanzania; wanabidii; Wanazuoni@yahoogroups.com
Subject: [Wanazuoni] Neno La Leo: Rasilimali Akili.. [1 Attachment]

 
[Attachment(s) from Maggid Mjengwa included below]


Ndugu zangu,

Tumepokea habari za matokeo ya ufaulu kwa Darasa la Saba. Na hakika, Maendeleo yetu kama taifa hayatawezekana bila uwepo wa maendeleo kwenye elimu. Nchi inahitaji watu wenye akili. Na akili ndio rasilimali muhimu nchi inahitaji kuwekeza kwa watu wake.

Dunia nzima watu wamekubaliana juu ya umuhimu wa elimu. Elimu ina manufaa kwa jamii, inachangia kuinua uchumi.

Hata kwa mtu mmoja mmoja, mwenye akili ya elimu ya darasani na uzoefu wa maisha ana nafasi nzuri ya kupata ajira, kujiongezea kipato. Kuridhika na kazi yake, hata kufurahia muda wake wa mapumziko. Ni mwenye kuwa nafasi zaidi ya kuwa na siha ( afya) njema. Ni nadra akawa mhalifu, ni mwenye kuwa na moyo wa kujitolea.

La mwisho ni lenye kuhusiana na zoezi tulilolimaliza juzi tu, mwenye akili ya elimu ya darasani na uzoefu wa maisha, ni mtu mwenye kujitambua, kujiamini na kuthubutu. Ni mtu ambaye, zoezi la kushiriki kupiga kura, kwake atalichukulia kuwa ni wajibu wake wa kikatiba na kizalendo kwa nchi yake, bila sababu za msingi, mtu huyo hawezi, ' kutoroka' zoezi la kupiga kura.

Hivyo, tuwekeze kwenye akili za watu wetu. Ndio, rasilimali akili.

Ni Neno La Leo.

 ( Pichani nilipoalikwa kama mgeni rasmi. Mwanafunzi wa darasa la saba, Lucy Boaz, akinisomea risala ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba shule ya msingi Ibigi, Katumba, Tukuyu Mbeya, mwezi uliopita.)

Maggid,

Iringa.

__._,_.___

Attachment(s) from Maggid Mjengwa | View attachments on the web

1 of 1 Photo(s)


Posted by: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)

Check out the automatic photo album with 1 photo(s) from this topic.
0.jpg


.

__,_._,___

0 comments:

Post a Comment