Friday 30 October 2015

[wanabidii] RE: [Wanazuoni] Neno La Leo: Mabadiliko

Patrick!
Sema wewe na unaowajua walichagua chaguo lisilosahihi na siyo wananchi. Wananchi wameshinda kwa kuchagua mabadiliko ya kweli siyo mabadiliko ya kuhama chama ili uitwe kijana hata kama wenye macho tunajua umehoka na unadanganya watu.

..........................................................................
"Ni bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu, lakini ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa kimya".

Baba Nouman,
Bongonyika, East Africa

From: Pater Patrick ppaternus1@gmail.com [Wanazuoni]
Sent: ‎30/‎10/‎2015 16:05
To: Wanazuoni@yahoogroups.com
Cc: mabadilikotanzania@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [Wanazuoni] Neno La Leo: Mabadiliko

 

Kaka Majid
Sifa moja ya reconsilition ni ukweli! Bila ukweli hakuna uhuru. Daima vita vitatawala, unafiki utatawala, ulagai na kinyongo vitatawala. Uhuru wetu na umoja wetu umejengwa katika ukweli wa kuunganisha moja na moja kuwa mbili si tatu na kuua moja kwa manifaa ya moja.
Wanasema ukiujua ukweli nao utakuweka huru.
Kweli tunaweza kama wanazuoni sema wananchi walichagua viongozi wao wakaheshimiwa?  Sema wana madaraka ya kuchagua na si kuweka viongozi. Ukweli mkubwa unejionesha katika uchaguzi huuu. Wazi wazi kupokonywa na kuporwa nia,dhamili na matamanio yao wananchi.
Hivi eti kusaini karatasi za majibu na wakara inalipa nguvu zoezi kuwa la huru na haki? Kwanini tuwe na auditor sasa katika matumizi na mapato yetu?kwani hiyo kazi haijafanywa na muhasibu ambaye amebalance mahesabu?
Lets we put knowledge in practice tusikurupue ufahamu baana.
Wasalaam
Pater

On Oct 30, 2015 9:24 AM, "Maggid Mjengwa mjengwamaggid@gmail.com [Wanazuoni]" <Wanazuoni@yahoogroups.com> wrote:
 
[Attachment(s) from Maggid Mjengwa included below]


Ndugu zangu,

Uchaguzi umeshapita. Tunafungua sasa ukurasa mwingine. Lakini, haina maana ya kuacha kufanya tathmini yakinifu ili tuweze kujifunza.

Tumeona, kuwa dhana ya mabadiliko ilitawala uchaguzi wa mwaka huu. Ni sahihi, kuwa mwanadamu, kwa asili, ni kiumbe mwenye kutamani mabadiliko. Ni kuanzia kwenye mavazi, chakula na mengineyo.

Tumekuwa wavivu sana wa kutafakari kwa kina juu ya tunamaanisha nini tunaposema tunataka mabadiliko katika nchi. Bahati mbaya, baadhi ya wanasiasa wameonyesha udhaifu mkubwa katika kuielewa dhana ya mabadiliko, ikawa kama wimbo wa taarab tu.

Ikafika mbali, kuwa waliosimama majukwaani kuhubiri mabadiliko hawakujua kama walifanya kazi pia ya kumhujumu mgombea ama wagombea wao wenyewe.

Sifa moja kubwa ya Watanzania ni dhamira na utayari wao wa kukataa kudharauliwa. Ilipofika mahali, watu wazima wanaojiita viongozi wakasimama majukwaani na kutamka; " CCM imechoka, nendeni mkachague hata jiwe!"

Huko ni kuwadharau Watanzania. Ni kauli kama hiyo ndio iliyowafanya Watanzania wengi waviache vitanda vyao alfajiri na mapema siku ya Uchaguzi Mkuu, waende kuhakikisha wanazuia 'mawe' yasipite. Maana, haikuwaingia akilini kuwa kwa miaka 54 CCM haikufanya chochote na kwamba imefika wakati wa kufanya mabadiliko kwa kuyaweka ' mawe' na CCM kuichimbia shimo kabisa. Kwenye siasa kauli zinaweza kupelekea kupanda au kuanguka kwa chama na mwanasiasa.

Na tuendelee kuitafakari dhana ya mabadiliko.

Ni Neno La Leo.

Maggid,

Iringa.

__._,_.___

Posted by: Pater Patrick <ppaternus1@gmail.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (5)

Check out the automatic photo album with 1 photo(s) from this topic.
0.jpg


.

__,_._,___

0 comments:

Post a Comment