Hapiness katabazi hongera sana kwa kuliona hilo kosa na kulizungumzia hapa. Ila nakushauri uende mbele zaidi kwa maana ya kuujulisha uongozi wa vituo hivyo rasmi ili warekebishe hilo tatizo.Ni kweli kupotosha hasa kwa mambo yanayohusu sheria au katiba si jambo zuri lakini hata hivyo nadhani ni kosa ambalo halikukusudiwa. Jambo la msingi la kuangalia ni nia ya mtoa taarifa. Nadhani nia yake ni nzuri tu ya kulinda haki ya kuishi ya alowataja katika tangazo lake na hivyo makosa yaliyofanyika katika ufikishaji wa ujumbe huo yanaweza kurekebishika kwa njia ya kuwakumbusha kuwa walikosea wapi na kwa nini.Hata Mawakili hutokea wakakosea katika kunukuu vifungu mbalimbali wanapopeleka hoja au mashauri kadhaa mahakamani lakini kwa muda mwafaka wanaweza kuiomba mahakama husika kurekebisha makosa hayo na mahakama inapoona kuna haja ya kufanya hivyo huwaruhusu ili kuto defeat justice. Kwa hiyo ili jamii isiendelee kuamini kuwa haki ya kuishi inalindwa na ibara ya 2 ya katiba ya nchi bali hulindwa na ibara ya 14 ya katiba hiyo basi naomba uchukue initiatives zako kuwajuza viongozi wahusika arekebishe hiyo hali maana sina uhakika kama wote watapata hii concern yako/yetu kupitia mtandao huu.
Ila na wewe mdogo wangu rekebisha sna sarufi (grammer) na hata literature yako maana unachapia sana katika maandishi yako utadhani wewe si Mtanzania. Au wewe ni Mganda? Maana hata hao ndugu zangu wahaya wa Kagera sidhani kama wanachapia sana kama wewe. Unaweza kuwa na ujumbe mzuri sana kwa jamii lakini jamii husika ikashindwa kukuelewa kwa sababu tu ya kuchoshwa (Bored) na jinsi ya uwasilishaji wa hoja yako. Vinginevyo kwa leo kwa hili nakupa big up kwa asilimia zote za kimantiki isipokuwa matumizi ya Lugha tu.Niliwahi kushawishika kukupigia na kuongea na wewe kuhusu hilo ukaniambia eti ni haraka haraka ndo inakufanya uandike hivyo lakini nakueleza kuwa huo siyo utetezi wenye mashiko kama ambavyo umesema vividly kuwa ignorance of law is not an excuse. Sijui ni excuse gani uliyomaanisha hapa lakini mimi ninamaanisha kuwa haraka haraka zako si kinga kuhalalisha Lugha mbaya sana unayoandika na inasomwa na watu wengi na wasomi wa wenye uweledi wa aina mbalimbali na hasa weledi wa Lugha maana wakisoma maandishi yako wale wasio wavumilivu wanatamani kulia na wengine hawaendelei kabisa kusoma ulichoandika hata kama kina mantiki kiasi gani kwa kuwa kinakuwa ni kama chakula kinachoonekana kimepikwa vizuri lakini hakina radha nzuri ya kuliwa.
Take my advise Katabazi ingawa naamini wewe ni mgumu sana kupokea ushauri tena wa bure. Watu wengine tukiwapa ushauri hupaswa kuulipia.
Adios,
Leonard.
On Wednesday, March 25, 2015 3:52 PM, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
CHANEL TEN,MAGIC FM TANGAZO LENU HILI LINAPOTOSHA KATIBA YA TANZANIA N a Happiness Katabazi BINAFSI ni mtazamaji na msikilizaji wa televisheni ya Chanel Ten na Magic Fm kwa lengo la kupata habari na kujifunza mambo mbalimbali. Kwa siku kadhaa nimekuwa nikilitazama,kusikiliza tangazo moja linalorushwa na vituo hivyo vya utangazaji . Tangazo hilo ambalo linaonyesha picha za sura za ndugh zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Maudhui ya tangazo hilo linataka mauji ya albino yakome kwani albino ni binadamu kama sisi na na tangazo hilo likasema eti ibara ya Ibara ya 2 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatoa haki ha kuishi. Binafsi muda wangu mwingi napenda kusoma baadhi ya Sheria ikiwemo sheria Mama ambayo ni Katiba ya nchi kwaajili ya kujifunza mambo mengi ya kisheria kuepuka kutenda makosa. Baada ya kusikiliza tangazo hilo nimebaini tangazo hilo limekosea kunukuu ibara hiyo ya pili kwani ibara ya pili ya Katiba ga nchi haizungumzii kabisa haki ya kuishi. Ibara ya pili ya Katiba ya nchi inazungumzia mambo haya ,naninanukuu kama ibara hiyo inavyosema: 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo. (2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge: Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo". Na kwa faida ya vituo hivyo vya utangazaji niwarahisishie kazi kuwa haki ya kuishi inapatikana katiba ibara ya 14 ya Katiba ya nchi na siyo ibara ya pili kamamlivyoupotosha umma kupitia hilo tangazo lenu kuwa eti ya kuishi inapatikana katika ibara ya pili ya Katiba ya nchi. Ibara ya 14 ya Katiba ya nchi inasomeka hivi,na ninanukuu: " Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake,kwa mujibu wa sheria". Waswahili wanamsemo mmoja usemao ' Muungwana asifiwi ushenzi'. Naamini vituo kwa kosa hilo vitawaomba radhi watazamaji na wasikilizaji wake kwa makosa hayo ya kunukuu vibaya ibara ya Katiba ,kisheria tunaita ' wrong citation' , na kisha iiende kulifanyia marekebisho tangazo hilo kwa kuweka ibara sahihi ya Katiba ili jamii isizidi kujifunza na watu waache kuua albino. Wito wangu kwa vyombo vya habari yaani magazeti ,redio,televisheni viwe makini katika hasa kunukuu baadhi ya vifungu vya sheria kwani vikinukuu kimakosa vikae vikijua umma ambao ni wavivu wa kutotaka kufanya utafiti yale yanayotangazwa na kuandikwa katika vyombo vya habari unaamini na kusadiki katika upostoshaji huo. Nimejiuliza hivi Chanel Ten,Magic Fm haina Mwanasheria wake ambae hasa katika tangazo hilo angeusishwa kikamilifu atoe mchango wake wa kitaaluma ya sheria? Lakini hata huyo naye aliyekubali kutia sauti yake katika tangazo lile naye kabla ya kwanza kukubali kuweka sauti yake katika tangazo lile ,alishindwa kabisa kutafuta Katiba ya nchi kuisoma ili ajilidhishe ibara ya pili anayoitangaza katika tangazo hilo kweli inasema hivyo? Ikumbukwe kuwa makosa kama hayo yanashusha heshima ya vituo vya utangazaji na vyombo vya habari kuwa havipo makini na kazi zake na kusababisha baadhi ya watu wapoteze imani na taarifa zenu. Lakini hata hiyo Idara ya Katiba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina maana halikulisikia au kuliona tangazo hilo ambalo limenukuu ibara isiyo sahihi? Ikumbukwe kuwa kifungu cha 8 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , inasema kutofahamu sheria siyo kinga kutoa adhibiwa. Nashauri katika habari au matangazo yanayo husisha taalamu kama udaktari, sheria na fani nyingine mbali na taaluma yenu ya uandishi wa habari basi wahusisheni kwanza wanataaluma hao ili wawape utaalamu katika eneo la fani yao ili msiendelee kuwa vichekesho au kupotosha jamii. Mungu ibariki Tanzania. Chanzo: Facebook: Happy Katabazi Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com 0716 774494 Machi 25 mwaka 2015.. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment