Tuesday 29 April 2014

Re: [wanabidii] Siungi Mkono Adhabu ya Kifo


Hivi kwa nini Mungu mwanzoni alikuwa akiadhibu watu kwa kuwaua-kuleta gharika, wakazama, akamtuma Nuhu kujenga safina na kuchukua pair ya wanyama wa kila aina. Safina imetafutwa na wana archeologists na wanasayansi wengine wameipata ipo Iran. Imefungiwa na kuwekewa ulinzi mkali ili eneo hilo lisiwe mahala pa kuabudu kama ilivyo huko Yerusalem Israel. Kwa nini alikuwa anatuma moto akachoma sodoma na goroma kwa kutokana na madhambi tu ya ulawiti na akasema walawiti (katika Biblia limeandikwa-ashakum-Wafiraji) hawatouona uwingu. Mke wa Luti akageuka jiwe kwa kuangalia nyuma akikumbuka maraha miji ikiwaka moto alikiuka maagizo, mume akasonga mbele bila yeye. Wakati Musa anawavusha Waisrael Bahari ya Sham (Red Sea kutoka Misri) si aliwateketeza akawazamisha baada ya kukaa miaka 40 jangwani njaa n.k mpaka baadhi wakaanza kuabudu sananu. Mwisho Mungu akaacha kuua akaleta Mtume Issa au Yesu kuelimsha watu, kuokoa na kufa yeye kwa ajili yetu. Ziko adhabu nyingi watu waliuliwa na mtenda maovu yatamrudia mwenyewe na muuaji hatouona uwingu hiyo ni dhambi ya mauti atakwenda kuchomwa moto-motoni. Kwa nini anayechinja kwa makusudi asiuawe?
Wanaharakati hushabikia haki za binadamu kwa maandamao wakati mwingine ili waonekane ili wapate pesa. Wengine hawatendi haki. Wamekaa ktk mashirika hayo ya haki toka yaundwe ni wakurugenzi hawabadiliki mpaka kufa. Nje ya ofisi zao kuna vitoto vidogo visichana na vivulana na wadada wengine wasomi wanajiuza. Huwaoni kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwatafutia misaada wajukwamue. Huwaoni kwenda hapo jangwani kinyesini kuelimisha watu wahame wanatesa watoto katika uchafu huo haki ya afya bora inakosekana. Ila utawaona hapo Meck Sadik -RC Dar na timu yake wakienda kubomoa waliorudi kutoka mabwe pande etc kukaa tena kinyasini au kulala vituo vya mabasi ya mwendo kazi kuwa expose watoto katika ubakwa na kufanyiwa uovu mwingine. Hapo utawaona wanaandamana kutetea haki za binadamu kuwa hao wanaoondolewa wanaonewa. Njaa kali inatufanya tuwe hatueleweki hata kama ni NGOs-tunashabikia issues mara nyingi badala ya kufanya grassroots participatory development. Tunakuwa usiasa zaidi na ushabikiism.

Anayeua kwa makusudi-afe. Asipewe muda eti atajirekebisha na amechukua bunduki anawatungua kila apitae. Amevamia shule amechoma watoto 500 na kuwakata mapanga wakichupa madirishani. Wapo wanaosamehewa na kutolewa baada ya muda anakamatwa katika uharifu mkubwa wa ujambazi na mauaji. Wapo wanaokuja kukiri-tulivamia pale tukaua, tukaenda kule, ajali ile na uvamizi ni sisi na mali tukipeleka kwa mu huyu na magari tuliyoteka na kuua madreva yapo yard fulani akibadili rangi etc na kuuza. Watu wameuawa, magari hayo yanakutwa kwa tajiri uwani hapo, akiuza na kuishi kwa raha na akijua wahusika waliua wakamletea. Uwaache hawa wote ili watu wasio hatia wazidi kuuawa? Kim-hawa budi WAFE  sio wale wa maandamano ya kisiasa.


On Tuesday, 29 April 2014, 10:55, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:
Nicolaus,
Umekuja na wazo zuri kaka mkubwa. Do you mean tuige utawala ule ule wa kina Sauli?! Kumbuka wakati Sauli anafanya yale ilikuwa chini ya uongozi wa nani na alikuwa anayafanya kwa favour ya nani thats why hakuguswa mwanzoni!!
La pili, unaposema tuwape watu nafasi ya lili unamaanisha nini?? Kusiwe ma adhabu kwa mkosaji lengo liwe kumpa nafasi ya mabadiliko??
"...by citizenship am a Tanzanian, nationality African..."
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment