Wednesday 30 April 2014

Re: [wanabidii] Mwanafunzi wa chuo afia chumbani wakati akijaribu kutoa mimba


Ndaki, kama umefanikiwa kusoma ulaya, chuo kinaweza kuwa kikubwa kikajaa mji au kidogo. Mabweni yakawa machache na ya categories mbali mbali. Kuna kuwa na taarifa ya nyumba binafsi za kupangisha za class mbali mbali pia. Priority unapewa mwaka wa kwanza au undergraduate tu. Tanzania mijini siku hizi ina nyumba za kupanga nyingi kwa wanachuo watu wameingia biashara hiyo. Kule ambako hakuna mabweni na hata panapokuwa mabweni wakipanga wanaamua kuoana. Wanafunzi wa shule za kata wanapangiwa nyumba na wazazi na kupewa hela, nimewahi kukuta wameamua msichana na mvulana kuishi kama mume na mke kuchangia kula na mengineyo. Wengine wanakuwa changudoa kwa tamaa zao.

Fika vyuoni uone vijana baada ya kupokea mkopo wa masomo-wanashindana kununua magari ya kusotasota. Mpaka vyuo vimeweka sheria ya parking na kuweka vibao kwa walimu wasikose parking. Mwanafunzi anatoka bwenini hapo chuoni hatembei anakwenda na gari Noah darasani wanapark hovyo au kuwahi na kuziba nafasi magari ya walimu, faculty yanakosa parking. Sheria zikawekwa na minyororo kufungwa. watokao mbali na gari-parking public zimewekwa.

Fika Mikumi Town-wanafunzi wa Morogoro hujaa kujiuza mbali na eneo la university na colleges nyingine na wale watokao Dodoma-wapo Morogoro. Wanafunzi wa UDSM-fika eneo la kakobe, kuelekea sinza, ustawi wa jamii na LHRC uone wanafunzi wa vyuo changudoa usiku. Wana maeneo yao zaidi ya haya.

Ukisema uhaba wa mabweni ni moja lakini hata mabwenini wanaoana na cases zipo wanafunzi kushitakiana mmoja analeta bwana au bibi na analala naye chumba kimoja na anaochangia nao, mimi anabaki humo kupika chakula. hivyo unaleta wako nami wangu, hakuna adabu bali overload ya weight wa watu kwa jengo, chumba cha watu 2 wanalala wanne; increased water demand, power use, sewage and waste disposal.Mabweni yanafurika maji na vyoo kuziba na maghorofa yanatitia. hata mabweni ya ulaya hupitishaga sachi usiku. Mwingine hana chumba anamlipa hela za kodi mwenzake analala humo chuo hakijui. Mwingine kamaliza chuo chumba harudishi anapangisha wajao anakula kodi anajifanya bado anaendelea na shule. Inataka usimamizi makini.

Vyuo vyote vya elimu ya juu vina zahanati na vina elimu ya afya na ukimwi na wana peer educators, free condoms lakini wanataka kavukavu ndio eti unaonyesha penzi na uaminifu. wana orientation ya kuelimishwa sheria, afya, ukimwi, stadi za maisha na vipeperushi kibao. Kutoa elimu ni muhimu bali sio final solution kuwa mtu atabadilika au kuzingatia. Ataona kifo cha kutoa mimba, atasikia, atamzika jirani au friend afae kwa ukimwi, ni dokta au nurse anayaona hayo kazini lakini hatotumia condom kwa matakwa yake binafsi. Kuona, kusikia, kufundishwa, kushuhudia, kupewa condom ni nyenzo na viwezesho tu, kinachotakiwa ni matendo ya kuzingatia uambiwalo lenye manufaa. Ndio maana hata police anakutwa kuwa jambazi, JWTZ jangili, hakimu kaiba, dokta na nurse wamekufa kwa HIV ambayo 80% inatokana na ngono sio salama. Kwani mjeshi au hakimu hajui madhara ya kukiuka sheria-mbona anakiuka? matakwa na tamaa binafsi.

Kukosa mabweni, mzazi kuwa mazikini iwe kigezo cha wewe kujilinda ili ufanikiwe ujikwamue. Mkopo uutumie vizuri ukupe elimu na maendeleo. wapo watoto wadogo wanajisomesha kwa kuuza mboga, ukuli na kazi ndogondogo. Ulaya wenzetu wanafanyakazi kuosha vyombo kafeteria, kufagia nyumba, kupanga vitabu maktaba, kuuza magazeti asubuhi, kutawanya barua za posta, taxi usiku na anajisomesha degree mpaka Phd anakuwa bell boy hotelini na kugawa chakula cafeteria ya chuo kikuu muda ule ambao haingii darasani. Sisi hapa bongo-msomi hata wa secondary hawezi kujituma hivi, chuo ndio kabisa!!!-Malezi, masikini tajiri. Na akirudi home akila mezani housegirl aondoe vyombo hawezi kuondoa na kuosha-msomi. Akirudi kijijini-anauza sura, sio amlimie bibi bustani aamkie shamba daily. TUBADILIKE.

Watoto wetu waliowengi ni tamaa, kutaka kuonekana. Mwaka wa kwanza kaja kavaa vizuri baada ya muda msomi anaingia darasani matiti kayapaisha juu, suruali kijana ipo chini chupi juu-aonekane na kutwa hela za mkpo yupo mwenge na makumbusho ananunua used clothes za gharama sio apeleke home hela afyatulishe matofari ya udongo saruji aboreshe nyumba yao. Likizo harudi analala kwa rafiki, kutafuta mama lea au mabwana anakaa mujini sio akasaidie wazazi shambani kwao. Darasani hataki tabu bali kuandikiwa alipe inkind.

 Msomi mtoto wa kichaga anauza duka la babake na anasoma degree, wengineo wanajiuza wao-hawana ujasiriamali bali kuuza mali asilia ya maumbile.

Simuhurumii huyo aliyetoa mimba na kufa, kama ni wangu-namzika na kesho nakwenda kazi. Nina usugu wa roho mbaya kwani mbona-angeizuia!!
 

On Tuesday, 29 April 2014, 16:55, "hosea.ndaki@gmail.com" <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:
Hilde, pamoja na kuwatuhumu mabinti kuwa ni viherehere lipo tatizo katika maisha ya chuo kwa watoto wetu wengi, matatizo ya ukosefu wa ada, pesa ya matumizi, kuahidiwa ndoa/uchumba, kuonja raha ya maisha na kuzidiwa tu na mihemuko ya ujanani/kubalehe.

Vyuo vingi vinaamini wanafunzi wao ni watu wazima ni jukumu lao kujisimamia. 6ivyo ipo haja ya kutizama mfumo mzima wa uendeshaji vyuo, iweje sekondari wanalazimishwa wawe na madarasa na mabweni lakini kwa vyuo sivyo.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, April 29, 2014 2:47:35 PM GMT+0100
Subject: Re: [wanabidii] Mwanafunzi wa chuo afia chumbani wakati akijaribu kutoa mimba

Huna mpango wa kuzaa lakini kutumia condom tatizo, kula dawa na kujichokonoa na vijiti utoe m,imba ndio tija? Hata wasomi hatufundishiki sio tu kuhusu mimba bali hata UKIMWI. kama iliingia mimba-ukimwi jee? Kwani kinga haikutumika. Pamoja na kumsikitikia hili ni funzo kwa wengine.Wanawake, wachukue jukumu la kujikinga na ujauzito wasioutaka. Mimba ikuue kwa bahati mbaya lakini sio kwa kuichononoa. RIP.


 

On Monday, 28 April 2014, 13:51, Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com> wrote:

Mwanafunzi wa Eden Hilling College aliyetajwa kwa jina la Atu Gabriel amefariki akidaiwa kujaribu kutoa mimba kwa kunywa vidonge.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani (RPC), Orech Mtei, katika kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema Jumamosi April 26 mwili wa Atu ulikutwa katika chumba cha mwanaume aliyefahamika kwa jina la Hafidhi ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake.Kamanda Mtei ameeleza kuwa polisi walikuta mwili wa marehemu ukiwa karibu na vidonge alivyotumia huku akitokwa damu nyingi sehemu za siri na kwamba polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa Hafidhi ambaye alidaiwa kukimbia baada ya tukio."Ni kweli tukio hilo limetokea Jumamosi Aprili 26 mwaka huu eneo la Kwa Mfipa baada ya jeshi letu kutaarifiwa kuwepo kwa mwili huo na polisi walipofika na kufanya uchunguzi wake tulibaini marehemu alifariki dunia kaika jaribia la utoaji wa mimba.....hata hivyo mwili bado upo Hospitalini Tumbi kwa ajili ya uchunguzi zaidi," alisema Kamanda Mtei.
Kamanda Mtei alisema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, kijana aliyetajwa kwa jina la hafidhi ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake alitokewa eneo la tukio na jeshi hilo kwa sasa linamtafuta kwa ajili ya mahojiano zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.
"Baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia na hadi sasa bado haijulikana alipo, jeshi letu linaendelea kumtafuta popote alipo na mara baada ya kumpata tutamuhoji na baadae atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheri," alisema Mtei.
Secretary wa Eden Hilling College ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa mwanafunzi huyo aliaga chuoni hapo siku ya Alhamisi kuwa anakwenda katika hospitali ya Mwananyamala kumuuguza wifi yake na kwamba wamesikitishwa sana na habari ya kifo cha mwanafunzi huyo.

"Aliaga vizuri tu siku ya Alhamisi kwamba anauguliwa na anakwenda kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini Jumamosi ndio tukapokea taarifa za kifo chake! Hii inaonyesha huyu mwanafunzi aliudanganya uongozi wa Chuo kitu ambacho hakikuwa sawa kabisa," Alisema.

Alisema hivi sasa uongozi wa Chuo unawasiliana na wazazi wake waliopo Makambaku kwa ajili ya kuja kuuchukuwa mwili wa marehemu.

Kwa undani wa habari hii na kusikiliza alichokisema RPC wa Pwani, ndugu na jamaa wa marehemu na majirani katika nyumba aliyokutwa wakisimulia tukio hilo, usikose kusikiliza Hatua Tatu ya 100.5 Times Fm Leo (April 28) katika kipengele cha Habari Ndio Hiyo na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr na Dj R Guy.

Kipindi cha Hatua Tatu kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita kamili na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr. na Dj R Guy.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment