Monday 28 April 2014

Re: [wanabidii] Siungi Mkono Adhabu ya Kifo

Lessian Mollel,
Uko sahihi kabisa, adhabu zote tumwachie Mungu, tukipigwa shavu la kushoto tugeuze la kulia. Umenena mkuu.

Nakuunga mkono maana hata hawa wezi wanaohukumiwa kifungo tuwasameheni, tuwatoe warudi mitaani maana huko tunawanyima uhuru wa maisha, tunawanyima nafasi ya pili kujaribu.
Na wale wauaji wasihukumiwe kifungo cha maisha maana Mungu amesema tusamehe 7*70,  tuwaache huru. Mungu atawaadhibu mwenyewe siku ya mwisho.

Logic yangu ni hii, 6+4=10, 5+5=10. Yote majibu yake 10. Zoote kuanzia kufungwa siku 2, kufungwa maisha, na kunyongwa zote ni adhabu kisheria (penalty)!!!
Ina maana tunajipa mamlaka ya kumgawia Mungu madaraka ya sheria kutumia kifungu kipi? Ni kifungu kipi katika biblia yako kinasema Mungu huchukua roho za wanadam?

Anaeua ni shetani that mean mwovu huyo amevuna alichokipanda!! Tena ukipata bahati ya kunyongwa mshukuru Mungu umejua siku yako ya kifo utubu dhambi zako maana hakuna mwenye bahati ya kuijua siku roho yake itakapotoka.

Amin nawaambia muombe Mungu niishike kamba ya farasi huyu Tanzania, nitakuwa dikteta mzuri sana ila mwenye uzalendo na mpigania maslahi ya wananchi wake. Hao Human rights watchers kama hawataki sheria za kunyongwa wakaanze kuwatetea wale wananchi maskini kabisa wanaonyonywa na viongozi wao, (mtu anajishindilia kila kitu tumboni kwake anaacha watu wanakufa!!) kabla ya kuwatetea hao viongozi watakaostahili kula kitanzi.


"...by citizenship am a Tanzanian, nationality African..."

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment