Monday 28 April 2014

Re: [wanabidii] Kutawala mazuzu raha sana

Afadhali yako Ansbert unaona ukweli na kuueleza kwa wazi. wapo wenzetu ambao sababu yao ya kuamini muundo wa serikali moja au mbili sijui zinatoka wapi?

Watu wanakalia tu hoja nyepesi ati no wasomi wamezungumza. Usomi ni pamoja na kubainisha dyanamics za nyakati. Wakati uliopo serikali tatuhaxikwepeki sababu nyakati ndo zinataka hivyo.

Huyu Nyerere tunaye mfanya reference tena vibaya kwani yeye alikua rigid? mbona alipoina sera za kijamaa hazitekelezeki mbona hakupinga mtazamo wa kibepari? hakupinga isipokuwa alijaribu kuwa mshauri wa karibu kwa viongozi ili wasiingie kichwakichwa. Lakini ukweli hakupinga kuwa nchi isiadopt kama ambavyo alikuwa makini muungano usife.

Vivyohivyo nyakati hizi zimebadilika zinalazimisha mabadiliko ya muundo wa serikali.

Anyway tuipe muda tu hoja hii tutauona mwisho wake mchana kweupe.


'Ansbert Ngurumo' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Hilde,

Hoja ya Serikali tatu si ya WARIOBA. Si ya Warioba. Si ya Warioba. Hata kama ungependa kuiita hoja ya Tume ya mabadiliko, bado utagundua kwamba Tume ilifanya tu uchambuzi wa maoni. Ni Tume na sekretarieti yake, wakiwamo watumishi waandamizi wa Serikali. Si Warioba. Yeye alikuwa Mwenyekiti, na aliwasilisha walichochambua. Ndio msimamo wa Tume na wananchi wanaodhani hapa tulipofikia, mwendo ni Serikali tatu. 

Wanaopinga hoja hii wanalazimisha iwe ya Warioba ili wapate fursa ya kumshambulia. Si suala la Warioba na Salim. Na hapa walipolifikisha suala hili, naona njia ya kuzuia Watanganyika kudai utambulisho wao ndani ya Muungano ni mtutu tu au kufuta NCHI ya Zanzibar ili tuzungumze NCHI moja, jambo ambalo katu Wazanzibari hawawezi kukubali. 

Ansbert Ngurumo
Existential Philosopher, Musician, Journalist & Media Manager
Vox Media Centre & Free Media
Tanzania

On 29 Apr 2014, at 1:40 asubuhi, "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Hilder Ukifanya hivyo utawanyima waqnanchi nafasi ya kuwajua viongozi wao. Wacha tuwajue ili kama tulifanya kosa kuwachagua tusirudie kosa

On Tuesday, April 29, 2014 1:19 AM, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:
Lakini itakuwa busara hawa wakubwa wetu, badala ya kutumia vyombo vya habari kubishana na kulaumiana na mmoja kutoa maelezo ya kupinga mwingine alivyosema na kutoa tahadhari kwa wananchi na viongozi-kabla ya yote wangeitisha kikao cha faragha cha viongozi wa juu kuonyanya na kupeana hizo fafanuzi. Haipendezi kuona leo anasimama huyu katika TV au kipindi cha radio au kutumia gazeti. Kesho mwingine anajieleza! Kesho kutwa mwingine wa tume au mstaafu fulani. Unakwenda kanisani au msikitini unaropoka. Si uandikiwe hotuba-omba msaada!! Mtondo sembuse Mh Rais anatoa fafanuzi ya masuala hayo hayo. Why?

Ingefaa, ipigwe marufuku kwa kiongozi wa Kisiasa au wa nchi au wa kuchaguliwa kwa kura za wananchi kutumia mahekalu, shule na maeneo mengine kuelezea masuala ya utawala wa nchi kama inavyofanyika sasa. Mtu anaalikwa kanisani, msikitini, shuleni, kwa bodaboda anaanza kuhutubia masuala ya bunge au siasa kujibu hoja za bunge n.k.

Wakati mwingine wanaohutubiwa suala hilo kiwango chao cha kuelewa masuala hayo ni mdogo sana-mfano katika kufungua shule ya msingi unaongea habari za muungano eti kwa vile wazazi na viongozi wengine wapo hapo!!

Kaeni kikaochenu cha ndani cha tume ya ushauri/marekebisho na maadili, msutaneeeee bila ya vyombo vya habari kuwepo, mrekebishane mbona kamati hizo za maadili zipo? Likivuja la siri atakayeliandika ktk vyombo vya umma amtaje aliyempa siri wote wafukuzwe kazi.

Kisha mkae ktk bunge la katiba mmalize kazi mliyopewa na mipangilio yake mje mtuambie kinachotufaa kama nchi za muungano aina gani, kwa sababu zipi na mfumo wa aina hiyo mnayopendekeza, mmalizie na masuala mengine ya katiba.

Hatari iliyo mbele yetu si ya jeshi kuvamia nchi kuitawala bali ni wananchi kuchoshwa na mipasuko na malumbano, misuto bunge la katiba na kuamua kulivamia bunge kuwatimua humo na vibaka wakitangulia kujichukulia pochi za posho. Nani asiyetaka laki 3 per day? Twazisaka hatuzipati kiurahisi na posho za mafuta juu!!*8-| rolling eyes

Mungu tusaidie tusifikie uzuzu kamilifu unaosemwa wa malumbano yasiyoisha ya viongozi wa juu. Tunataka  sasa Malumbano haya yapigwe marufuku. Vyombo vya habari visishabikie malumbano haya.

Tayari magazeti wameanza lingine jipya la kuleta malumbano kusema-Mh Warioba anataka Salim M. Salim awe Rais was serikali ya Muungano ktk mfumo wa serikali 3(Mwanahabari April 28, 2014-Jaji Warioba amlengeshea Salim Urais wa muungano-front page-page 2). Kumbe nia ya Mhe warioba ya S

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment